Misaada ya EU imerudi kwa masharti yaleyale, japo....

Misaada kutoka nchi za Ulaya imerudi kwa gharama. Taarifa za ndani ni kwamba nchi za Ulaya zilikataa kabisa kutoa misaada kwa Tanzania. Tukalazimika kumtumia mtu wa kati, Rais Mstaafu wa Benki ya Afrika Donald Kaberuka, kutuunganisha na nchi za Ulaya.

Misaada inarudi kwa masharti ambayo tumeridhia:
1) Kuheshimu demokrasia, pamoja na kuruhusu vyama vya siasa vifanye kazi bila vipingamizi vya serikali
2) Utatuzi wa mgogoro wa Zanzibar
3) Utawala wa sheria
4) Uhuru wa maoni
5) Uhuru wa vyombo vya habari
...Aiseee kumbeee!!
 
Sitaki kumsingizia mchawi, Ila tuna shida ya jinsi tunavyo fikiria, hayo uliyo ainisha ni aibu kuhimizwa kuyatekeleza. Yanatakiwa kuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku.
....JK alivyokuwa anayatekeleza hayo hawa walioingia sasa wameishia kumkejeli.
Shida kubwa ni kuropoka bila uchunguzi bila mipango,fikiri kabla madhara na faida
 
Hata ikitokea tusifanikiwe, suala la kuendelea na kubuni namna ya kujitegemea si la kubeza na wala si lelemama. Sioni kosa la raisi as long as anachokifikiria ni kuona siku moja walau tunajitegemea 70%. Kwa mwanaume yeyote sidhani kama atafurahi kupangiwa aishi vipi na hata ikatokea akapoteza uhai wake kwa kulipigania hili itatosha kumpa heshima yake na kukumbukwa daima. Hata Nyerere ilifika sehemu akashindwa lakini hatuachi kumkumbuka na kumuenzi.
 
Kama kawa tunaficha kichwa kichakani tukijifariji kuwa adui hatuoni.
 
Chaza, mimi sidhani kama awamu hii ilikuwa na mkakati au hata agenda ya kujitegemea. Kilichotokea ni kuwa awamu hii ilirithi nchi ikiwa na hali mbaya kimapato, madeni mengi na ahadi za uchaguzi lukuki zenye kuhitaji fedha nyingi. To add insult to injury, MCC ikafuta sehemu kubwa msaada wake huku wahisani wengine wakinuna na kulalamikia kufutwa kwa uchaguzi Zanzibar. Mazingira haya ndiyo yaliyozaa ile political rhetoric kuwa nchi hii ni tajiri na inaweza kujitegemea! Good idea but certainly siyo leo wala kesho. Hivyo kila mmoja wetu alijua hayo ni maneno ya kufurahisha baraza.
Kweli tupu mkuu
 
Tanzania kwenda bila misaada ni uongo, haiwezekani. Magufuli chunga kauli zako, na utake usitake utapangiwa tu kwasasbabu nchi yako ni masikini, watu wako ni masikini, na mbaya zaidi wewe mwenyewe unachukia matajiri.
 
Hawa wanyarwanda tunaowapandikiza katika nchi hii bila kutazama madhara yake baadaye itakuja kutugharimu kama inavyo wagharimu wakongo ambao waliwapa nafasi hadi jeshini na ndicho kinacho wagharimu mpaka leo na kwa jinsi inavyosemekana hata Joseph kabange ndezira kabila ni mnyarwanda. Watanzania tuweni makini tuache tabia ya kupiga makofi bila tafakuri.
Sasa kama unashinda kwenye keyboards za computer na kuporomosha matusi unategemea Rwanda wakusubiri wewe na uzezeta wako
 
Tunajidhalilisha wenyewe. Hili la EU lilitarajiwa. Ni sawa sawa kutegesha alarm kwenye saa; muda ukifika itapiga kelele. Somo tunalopata ni kuwa tunao viongozi wa ajabu kiasi kwamba hata baada ya miaka 20 ya demokrasia ya siasa ya vyama vingi bado wao wanadhani wanaweza tu kufutilia mbali mfumo huo ili wapate urahisi wa kutawala (siyo kuongoza) kwa matakwa yao binafsi. Lakini cha kushangaza zaidi ni watu hao wanaojiita viongozi kutotambua ukweli kuwa nchi hii ni tegemezi sana kwa nchi tajiri ambazo zimedhamiria kutumia ukarimu wao kudumisha na kuendeleza hiyo demokrasia na mambo yanayoambatana nayo. Kutoliona hili ni kasoro kubwa sana kwa watu wanaojiita vongozi. Ndiyo maana mwanahabari mmoja nguli alionya: kama huna uwelewa wa kutosha kuhusu historia ya utawala duniani basi kamwe usitafute uongozi.
 
Nimetulia.....
 
Back
Top Bottom