Rais Samia ashiriki Hafla ya Kupokea Fedha za Msaada wa Bajeti ya Serikali kutoka EU, leo Julai 4, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Hafla ya Kupokea Fedha za Msaada wa Bajeti ya Serikali kutoka Umoja wa Ulaya (EU) katika Ukumbi wa Karambarage Hazina (Treasury Square) jini Dodoma.



===

IMG_7864.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa Nchini Mhe. Manfredo Fantl, wakati Balozi Fantl alipofika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma 04 Julai, 2023.

IMG_7865.jpeg
IMG_7866.jpeg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa Nchini Mhe. Manfredo Fantl, wakati Balozi Fantl alipofika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma 04 Julai, 2023.

====


Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshuhudia utiaji saini wa Mikataba 3 ya msaada wa maendeleo inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) wenye thamani va Euro milioni 179.35 sawa na Shilingi bilioni 455.09 za Kitanzania.

Aidha, Rais Samia ameshuhudia kutangazwa kwa fedha za msaada wa bajeti ya Serikali zilizotolewa na EU kiasi cha Euro milioni 46.11 sawa na Shilingi bilioni 117.036 za Kitanzania kwa mwaka wa fedha 2022/ 2023.

Fedha hizo zitaelekezwa katika sekta za maendeleo hasa katika uchumi wa Buluu, uwezeshai wananchi kiuchumi pamoja na uimarishaji mifumo ya ukusanyaji na usimamizi wa fedha serikalini.

Katika hafla hivo iliyofanyika ukumbi wa Hazina Rais Samia ameishukuru EU kwa kuwa msaada huo ni matokeo ya zara alivoifanya Brussels, Ubelgiji alipokutana na Rais wa Tume ya Ulaya Mhe. Ursula Von der Leven. Msaada huo uliotolewa kwa Serikali unaendana na mipango mkakati va kisekta na maendeleo nchini, hususan Mango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano, Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025 na Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2050.

Aidha, Rais Samia amesema Programu hizo pia zitaendana na kaulimbiu ya Mwaka wa Fedha wa 2023 / 24, kama ilivyopitishwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC): "Kuongeza kasi ya kufufua uchumi, kukabiliana na kupunguza mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuimarisha sekta zenye tija kwa maisha bora".
 
Ifikie wakati tuache kushangilia misaada.
Toka mwaka 1961 nchi inapata misaada.
Adui yenu mkubwa ni IMF, msipojua hilo tutaendelea kushangilia misaada.
Kila nchi ikikaribia kulipa madeni wanadevalue currency yao ili kuendelea katika circe.

imf sijui wb angalieni interest nchi masikini zinazochajiwa zikikopa na nchi tajiri interest compare uone.
 
Ifikie wakati tuache kushangilia misaada.
Toka mwaka 1961 nchi inapata misaada.
Adui yenu mkubwa ni IMF, msipojua hilo tutaendelea kushangilia misaada.
Kila nchi ikikaribia kulipa madeni wanadevalue currency yao ili kuendelea katika circe.

imf sijui wb angalieni interest nchi masikini zinazochajiwa zikikopa na nchi tajiri interest compare uone.
Adui yetu mkubwa ni mafisadi ya CCM na sio IMF
 
Hivi kwenye hotuba ya Waziri wa fedha. Waziri alianisha ni kiasi gani cha tozo kilikusanywa kwenye miamala ya simu kwa mwaka wa fedha uliopita. Na matumizi yake yalikuwaje?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Hafla ya Kupokea Fedha za Msaada wa Bajeti ya Serikali kutoka Umoja wa Ulaya (EU) katika Ukumbi wa Karambarage Hazina (Treasury Square) jini Dodoma.


Kumbe ni msaada,ok
 
Ila Bi Mdashi anavijisifa kidonda bado kibichiii na mtoki kwa mbaali,,,KakiTia maji ya betri kitapona lakini kwa maumivu Makali mnoo!!na kwa ubichii wa kidonda hicho na matibabu yanayoendelea kuna uwezakano kisipone,,,kitachukua muda mnoo kupona,,,Kikawa donda ndugu,,au kikasababisha kingdom cha mwili kilichodhurika na hicho kidonda kukatwa kwa lazima na pia kinaweza sababisha umauti kwa mwili wa mwenye kidonda,,LETI SII TUTATUA WAPI KWENYE ON TU ZE NEKSTI WANI!!
 
Ni swala la tengua, teua

Kuhudhuria mikutano na halfa

Sasa hivi tena kuhudhuria sherehe ya kupokea msaada wa budget

Muda si mrefu wataanza kumpa kazi ya kwenda kukata utepe wa miradi mipya.
 
Hivi Huko EU hatukusaini / Hatujasaini (Makubaliano) ya EPA ?!!

Naona kama mambo yanakwenda kwa Spidi ya 4G
 
Back
Top Bottom