Misaada ya EU imerudi kwa masharti yaleyale, japo.... | Page 4 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Misaada ya EU imerudi kwa masharti yaleyale, japo....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by gillard, Apr 21, 2017.

 1. gillard

  gillard JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2017
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 227
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 60
  Kwanza nianze kwa kusema, naunga mkono juhudi za Rais wetu kutaka Tanzania ijitegemee. Ni mtazamo wa watanzania wengi tu na hata vyama vya upinzani wameliongelea sana suala hili.

  Misaada ambayo Rais wetu amepokea juzi toka kwa umoja wa ulaya imerudi kwa masharti yaleyale, The Citizen linaripoti. Kwa mujibu wa gazeti hilo licha ya msimamo wa Rais kuhusu misaada toka nje, ilikuwa vigumu kwa bajeti ya 2016/2017 kutekelezeka kama mchezo wa paka na panya ungeendelea.

  Ukweli ni kwamba watu kutoka serikalini walikuwa wanafanya jitihada nyuma ya pazia kuokoa jahazi kwani ilikuwa bayana kwamba misimamo wa kisiasa wa Rais wetu ulikuwa haumsaidii yeyote.

  Wakati Rais Magufuli akiendelea kutuaminisha wananchi masikini kwamba wahisani hawana tena nafasi ya kutupangia masharti, inaelezwa kuwa wawakilishi wa serikali walijadiliana mpango ambao kimsingi utamfanya mkuu wa nchi aendelee kuyaishi masharti yaleyale ambayo alijinasibu huko nyuma kuwa hatoyakubali asilani.


  Naishauri serikali na Rais wetu, ukimya nao una busara zake katika kufanya maamuzi na kuweka mambo sawa, "tusitukane mamba kabla hatujavuka mto", tusipende kuongea sana kwa kufurahisha genge, “twende strategically” tutafika. Kwa madhara yaliyotukuta safari hii kwa bajeti yetu ya 16/17 kupumulia mashine hili liwe fundisho kwetu sote.

  Ushauri kwa wasomi wetu, acheni kujipendekeza, mwambieni Mh. Rais ukweli, ongeeni ukweli kwa faida ya Taifa letu na vizazi vijavyo. Msiongee kumpendezesha Mh. Rais ili tu muonekane.


  Mwisho, shukrani za pekee kwa bosi wa zamani wa Africa Development Bank Ndg. Donald Kaberuka kwa kuongoza mazungumzo yaliyofanikisha misaada tuliyoshuhudia ikirudi wakati Rais wetu alipokutana na Balozi wa Umoja wa ulaya.


  Mungu ibariki Tanzania
   
 2. k

  kabombe JF-Expert Member

  #61
  Apr 21, 2017
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 17,028
  Likes Received: 9,824
  Trophy Points: 280
  Bavicha mnajitekenya na kucheka wenyewe.
  EU waliamua kusitisha misaada,si Rais,Makamu wala waziri yoyote aliefunga safari kwenda kuwalamba miguu.
  Zaidi tuliwaona chadema wakiwa kwenye bunge la ulaya,wakishindilia fitna eti tusipewe misaada.
  Haiingii akili serikali eti ikubali misaada kwa masharti wakati ilishaamua kufa na tai.
  Hapa bavicha mnatakiwa mjadili matunda ya ziara zenu kwenye bunge la EU,na mualiko mliompa balozi wa EU Tanzania pale bungeni zimezaa nini?
   
 3. gillard

  gillard JF-Expert Member

  #62
  Apr 21, 2017
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 227
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 60
  Sio kila anaeandika hapa ni bavicha mkuu.
  Nimekuwekea link hapo ya habari kamili si usome? Acha kupotosha watu kama huna facts, muulize waziri Mpango atakuelewesha.
   
 4. Mwelewa

  Mwelewa JF-Expert Member

  #63
  Apr 21, 2017
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 2,341
  Likes Received: 2,612
  Trophy Points: 280
  Masharti yote ya EU ni muhimu kwetu kama nchi.
   
 5. onkoko

  onkoko JF-Expert Member

  #64
  Apr 21, 2017
  Joined: Aug 23, 2016
  Messages: 470
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 80
  Hawa wanyarwanda tunaowapandikiza katika nchi hii bila kutazama madhara yake baadaye itakuja kutugharimu kama inavyo wagharimu wakongo ambao waliwapa nafasi hadi jeshini na ndicho kinacho wagharimu mpaka leo na kwa jinsi inavyosemekana hata Joseph kabange ndezira kabila ni mnyarwanda. Watanzania tuweni makini tuache tabia ya kupiga makofi bila tafakuri.
   
 6. K

  KASHOROBAN JF-Expert Member

  #65
  Apr 21, 2017
  Joined: Apr 7, 2017
  Messages: 442
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 80
  Hii ya uhuru wa mitandaoni lazima ni kweli kwani Siku hizi siwaoni TISS wakitugasi uku Facebook. Naona kidogo tunaanza kuheshimiana hasa kiheshimiwa
   
 7. K

  KASHOROBAN JF-Expert Member

  #66
  Apr 21, 2017
  Joined: Apr 7, 2017
  Messages: 442
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 80
  Duh hii ndo inaitwa nightmare. Wewe unayelia njaa ndo ukawasaidie wazungu. Wewe hata kujisaidia huwezi ndo uwasaidie wengine. Hili sahau over and ever
   
 8. K

  KASHOROBAN JF-Expert Member

  #67
  Apr 21, 2017
  Joined: Apr 7, 2017
  Messages: 442
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 80
  Ah ah ah... Umenichekesha kwi kwi kwi. ..
   
 9. K

  KASHOROBAN JF-Expert Member

  #68
  Apr 21, 2017
  Joined: Apr 7, 2017
  Messages: 442
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 80
  Sio sisi ni kapuku... Washauri wake toka CCM ndo kapuku pia vilaza mpaka anachukua viraka vya ACT ah ah ncheke mieeer
   
 10. kampelewele

  kampelewele JF-Expert Member

  #69
  Apr 21, 2017
  Joined: Oct 13, 2014
  Messages: 2,585
  Likes Received: 1,390
  Trophy Points: 280
  You are just a small boy! Hujui haya majambo. Dr kaberuka alikuwa president wa Afdb ambayo ni sawa na world bank ya africa. Kubali kuelimishwa young man. Maswali unayouliza yanaonyesha ulivyo
   
 11. iparamasa

  iparamasa JF-Expert Member

  #70
  Apr 21, 2017
  Joined: Nov 14, 2013
  Messages: 13,462
  Likes Received: 14,138
  Trophy Points: 280
  Kuna mmoja alikuwa jeshini na cheo kikubwa enzi za
  "Alikuwa" ni zamani

  Umemaliza darasa la saba?
   
 12. S

  Sandinistas JF-Expert Member

  #71
  Apr 21, 2017
  Joined: Jul 5, 2013
  Messages: 829
  Likes Received: 317
  Trophy Points: 80
  Huu ulikuwa mgogoro kati ya wahisani na serikali ya Tanzania. Msuluhishi alihitajika. Kaberuka is not just another Mnyarwanda. Alikuwa rais wa Benki ya Afrika na Tanzania ilifaidika sana wakati wa urais wake. Essentially, an outsider, neutral person with impeccable credentials was required.
   
 13. Mavipunda

  Mavipunda JF-Expert Member

  #72
  Apr 21, 2017
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 4,796
  Likes Received: 3,560
  Trophy Points: 280
  Kuna ule mchanga aliouzuia Bandarini nao utamtokea puani soon
   
 14. kampelewele

  kampelewele JF-Expert Member

  #73
  Apr 21, 2017
  Joined: Oct 13, 2014
  Messages: 2,585
  Likes Received: 1,390
  Trophy Points: 280
  Hata ukiwa na PhD lazima umalize darasa la saba. You seem to be naive am sorry lazima tuwaelimishe nyie watu.
   
 15. iparamasa

  iparamasa JF-Expert Member

  #74
  Apr 22, 2017
  Joined: Nov 14, 2013
  Messages: 13,462
  Likes Received: 14,138
  Trophy Points: 280
  Wewe ndiye unastahili elimu,mpaka sasa unaona ni sawa Mnyarwanda kuzunguka dunia nzima kwa nauli ya watanzania eti akituombea msamaha kwa wafadhili

  Makosa yenyewe ni ya kurekebisha tu sisi wenyewe,kuruhusu mikutano ya hadhara mpaka tushauriwe? Kuruhusu demokrasia mpaka tushauriwe?

  Hivi vitu vilikuwepo tangu Nyerere akiwa hai, na yeye kama baba wa taifa aliona havina tatizo,sisi wa miaka hii tunajiona wajuaji,haya sasa,hospitali hazina dawa,na hata hizo hela za wafadhili haziji ghafla,ukitangaza sasa mikutano ya hadhara ruksaaaa,inakuja mia tano,bunge laivu,mia mbili,utaongea na maalim,inakuja milioni moja,unarekebisha sheria ya mitandao,wanakupa milioni mbili, ni piece by piece,hela inatolewa kwa action plan iliyowekwa na mzungu mwenyewe
   
 16. iparamasa

  iparamasa JF-Expert Member

  #75
  Apr 22, 2017
  Joined: Nov 14, 2013
  Messages: 13,462
  Likes Received: 14,138
  Trophy Points: 280
  Hapo ndio patamu,mkataba tumesaini wenyewe kuwaruhusu kupeleka mchanga,na wao wakasaini mikataba lukuki na kampuni nyingi zikiwemo za malori ili kusafirisha,meli, na kiwanda cha kuchenjua,yote imevunjwa!!!

  Na haya makampuni ya madini ni Multinational,unapo deal nayo fanya au assume unadeal na serikali ya nchi yalikotoka,iwe Canada,Marekani,Uingereza,yanabeba bendera ya nchi yaliyotoka,na yanaweza kulilia protection ya mother countries.

  Pia mengi hutumia mikopo ya mabenki makubwa makubwa duniani au taasisi kubwa kubwa duniani ambazo zinaweza kuwa na impact

  Ni sawa na Carl Peters alipokuja kutafuta makoloni,alikuwa na kampuni inaitwa Germany East Africa Company,machifu wakasaini mikataba wakijua wanasaini na mzungu mmoja tu,baada ya kusaini ndipo wakajua walikuwa wana deal na nchi ya ujerumani
   
 17. faru john junior

  faru john junior JF-Expert Member

  #76
  Apr 22, 2017
  Joined: Dec 26, 2016
  Messages: 907
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 180
  Nitajie mashrti matano tu tuliyokuwa tumepewa na inabdi tuyatekeleze
   
 18. iparamasa

  iparamasa JF-Expert Member

  #77
  Apr 22, 2017
  Joined: Nov 14, 2013
  Messages: 13,462
  Likes Received: 14,138
  Trophy Points: 280
  Na yalikuwa sehemu ya maisha yetu kwa karibu miaka thelasini,na hapakuwa na tatizo!!
   
 19. gillard

  gillard JF-Expert Member

  #78
  Apr 22, 2017
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 227
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 60
  Umeniamsha vizuri na nusu siku yangu.
  True, we needed someone with reputation and trustworthiness who would stand for professionalism and ethics without the fear of putting their political or government position in jeopardy.
   
 20. gillard

  gillard JF-Expert Member

  #79
  Apr 22, 2017
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 227
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 60
  Kama miaka yote hii hujui tunapokea misaada kwa masharti yepi unanitia mashaka sana kama kweli wewe ni Expert Member, na sina namna ya kukusaidia, you are a thinker, jiongeze.
  Hint: mtafute mpango, au hata Zitto Kabwe yuko vizuri, ukikwama kuwapata muone mstaafu Likwelile yeyote kati ya hao atakujuza.
  By the way hata kwenye uzi huu thinker wameainisha baadhi, usiwe mvivu kusoma mkuu.
   
 21. C

  CHAZA JF-Expert Member

  #80
  Apr 22, 2017
  Joined: Dec 21, 2012
  Messages: 6,795
  Likes Received: 2,255
  Trophy Points: 280
  Nami niweke neno kidogo. Awam ya tano iliingia ikiwa focused na kujitegemea,ni jambo jema sana. Lakini kila jambo lina hatua.Matamko ya kisiasa yalikua ni mengi bila ya kufanyika utafiti. Kwa mfano trend yetu ya makusanyo yalifahamika kwa miez mitatu ya kwanza kuwa ni Tsh 1.12 hadi1.3+Tn/- kwa mwezi. Hii trend tayari kwa mtu makini angejua tu hatuna hela za kutosha kuendesha nchi kwa 100%.Hivyo ilitakiwa kuchunga maneno ya kuongea. Kwa maana hiyo makusanyo kwa mwaka unaona kabiasa isingeweza kufika Tsh 15.5tn/- kwa mwaka. Sasa unapopitisha bajeti ya 29tn/- huku uwezo wako wa kukusanya ni nusu tu ya bajeti yako,basi jua bado utalazimika kuwa mtumwa wa IMF,WB,ADB na misaada ya Nchi za Magharibi ambao wao kamwe hawawez kutoa misaada ukienda nje ya matakwa yao. Hili ni somo kubwa la kujifunza.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...