figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,895
Rais Wa Jamhuri Samia Hassan, naomba umpangie kazi nyingine Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, Simon Simalenga sababu anakudhalilisha na kukuharibia. Anafanya watu wakuone kwamba huna maamuzi hata mteule wako anapoenda kinyume na maadili. Ni moja ya watu wanaoamini Mwanamke hawezi kuongoza Nchi. Pamoja na madhaifu mengine, naomba ufuatilie, kama kweli ukikuta kaingia kwenye mkumbo wa kujadili saa uliyovaa, hafai kuwa msaidizi wako.
Mkuu wa Wilaya unatakiwa Uwe upande wa mtu aliyekuteua hataka kama kakosea. Ni jambo la lawaida kimaadili. Sio umshushue.
Kumbuka Kawafukuza Waandishi wa habari kwamba wasimuingilie kwenye majukumu. Hataki kuhojiwa chochote kuhusu Wilaya yake. Anataka akuandalie taarifa akupe sio wewe umuulize swali au Ufafanuzi.
Kwakuwa ameonesha kutokutaka kushirikiana na Mhimili wa nne vyombo vya habari, ana haja gani ya kuendelea kukalia hicho kiti. Kwanza hakuna Mwandishi ambaye angemuuliza mambo ya Saa, watu walikuwa wanafuatilia kikao cha District Consultative Council (DCC).
Pia kashindwa kuwasaidia Wachimbaji wadogo. Licha ya Waziri wa Madini, Anthony Mavunde kuagiza Wachimbaji wadogo wa dhahabu katika Mgodi wa Ikinibushiu, wilayani Bariadi mkoani Simiyu wapewe leseni na wasiondolewe wala kunyanyaswa ikiwemo kuhakikisha haki zao zinalindwa, Hadi leo hajawasaidia kwa chochote na wachimbaji hao wanalamikia vitendo vinavyofanywa na watu waliyopatiwa leseni za kumiliki eneo hilo kwa kutaka kuchukua maduara yao na kuwaondoa. Mkuu wa Wilaya yupo Kimya.
PIa TAKUKURU imchunguze