Miradi ya kimkakati Tanzania yawa chachu kwa vijana kuchangamkia kozi zote zinazohusu Reli, Meli na Anga zinazotolewa NIT

LAZIMA NISEME

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
232
260
Dhamira njema iliyooneshwa na serikali katika kukazania kujenga miradi ya kimkakati imetoa hamasa kwa Watanzania wengi kuchangamkia fursa ya kusoma kozi za huduma za usafiri wa reli, meli, bandari na anga katika chuo cha usafirishaji tanzania (NIT) Kwa Mujibu wa Mkuu wa Chuo
PHOTO-2022-06-07-21-19-26 2.jpg
PHOTO-2022-06-07-21-19-26.jpg
PHOTO-2022-06-07-21-26-22.jpg
PHOTO-2022-06-07-21-27-41.jpg
PHOTO-2022-06-07-21-29-46.jpg

IMG_2994.JPG
IMG_2884.JPG
IMG_2957.JPG

amesema awali kozi hizo hazikuwepo na chache zilizokuwa zikifundishwa vyuoni, zilikosa uungwaji mkono baada ya sekta hizo kufifia hali iliyosababisha Watanzania wengi kukwepa kusoma taaluma hizo kwa kuhofia kukosa kazi.
Na ukweli ni kwamba kudorora kwa sekta hizo kulisababisha watu waliokuwa tayari ni wataalamu wakate tamaa kujishughulisha na masuala hayo na kujikita kwenye shughuli nyingine ikiwemo siasa

Profesa Mganilwa anasema kuwa baada ya sekta hizo kuzorota zaidi ya meli 36 ziliharibika, fursa ya ajira ilishuka. Lakini, kufuatia serikali kuona umuhimu wa sekta hizo na kuanza kuwekeza wananchi wamechangamkia kusomea taaluma hizo.

Anaeleza kuwa mara baada ya Shirika la Taifa la Uwakala wa Meli (NASACO) na TACOSHIRI

kuporomoka katika uendeshaji, ilikuwa pigo la hali ya juu kwa uchumi wa bluu ambao kabla ulikuwa ukichangia kwa kina kwenye Pato la Taifa.

“Tuna kozi ya wasanifu wa meli, baada ya serikali kuanza ujenzi wa meli, wahandisi wa meli kozi mpya iliyoanza mwaka huu 2022 na kozi ya ‘Automobile Engineering & Mechanical’ nao wanahusika katika ujenzi na uungaji wa meli kwa kuwa ni wataalamu wa injini na uungaji,” anasema Profesa Mganilwa.

Upande kwa wanafunzi wanaosomea usimamizi wa bandari na mashirika ya meli, mkuu huyo wa chuo cha NIT anasema huu ni mwaka wa pili tangu wajiunge na chuo akimaanisha kwamba nchi inatarajia kujipatia wahitimu wa kwanza wa kozi hiyo mwaka 2023.

kwa upande wa usafiri wa anga pia kimekuwa kinatoa mafunzo katika uhandisi na ufundi ndege.

Profesa Mganilwa anasema matarajio ya chuo kabla ya kufika Desemba, mwaka huu, kuanza kufundisha kozi za urubani ambapo kwa mwaka ada itakuwa sh. milioni 70 badala ya sh. milioni 200 zinazotozwa katika vyuo vya nchi za nje.

Anachanganua kuwa katika ada hiyo, sh. milioni 21 ni gharama za kozi ya urubani kwa masomo ya awali na kiasi kinachobaki ni gharama ya kuruka angani saa 50 wakati wa mafunzo yatakayofanyika katika hatua mbalimbali.

Profesa Mganilwa anasema mwanafunzi wa ngazi ya awali akihitimu na kupata leseni ya kurusha ndege za watu binafsi, atapaswa kuendelea na masomo kwa miaka miwili na nusu (miezi
30) ili kukamilisha sifa ya kupata leseni ya biashara ya CPL hivyo kufanya gharama ya kozi hiyo jumla kuwa sh. milioni 70.

Anasema baada ya mwanafunzi kusoma na kutunukiwa leseni ya CPL ataweza kurusha ndege kwa saa 200 na kufanya masomo ya hali ya hewa, baadaye ndipio muhitimu ataruhusiwa kuajiriwa katika mashirika ya ndege ya kibiashara akitakiwa na ndege ndogo zinazobeba abiria 70.

“Baada ya hapo atatakiwa kusoma tena ili apate leseni inayoitwa ATPL akipata hiyo anaweza kuendelea kusoma zaidi hadi kufikia hatua ya kuendesha ndege kubwa aina ya Dreamliner,” anasema Profesa Mganilwa.

Anasema kuhusu mchakato wa kupata ithibati ya kozi ya urubani kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA), wameshafikia hatua ya nne inayowataka wawe na ndege ambazo tayari serikali imenunua ndege mbili zinazogharimu sh. bilioni 2.4 na wameshalipa nusu ya fedha hizo.

NIT mbali ya kufundisha kozi kongwe za udereva wa magari, masoko na mawasiliano ya umma, utawala na nyinginezo, pia chuo hicho kimekuwa kinawanoa wasanifu, wahandisi na wasimamizi wa meli, ndege na bandari na wapo mbioni kuanza kufundisha kozi ya urubani

Uwepo wa vifaa vya kisasa vilivyonunuliwa na serikali kama Injini za pistoni na jeti,kituo cha kisasa cha kufundishia uhandisi wa Ndege kumewezesha wanafunzi 23 kuwa zao la kwanza la wahandisi kuhitimu mwaka 2023 chuoni hapo kukiwa na wasichana 3 .
Wanazuoni wanasema ni mapinduzi makubwa ya kila sekta ya rasilimali watu..Wanamsifu raisi Samia Suluhu Hassan kwa kuzidi kuboresha Chuo hiki cha kimkakati
 
Back
Top Bottom