Mambo 10 kuhusu Gerald R. Ford (CVN-78), Meli kubwa zaidi ya Kijeshi inayomilikiwa na Marekani

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,120
Hii ndio Meli inayotajwa kuwa ya Kisasa na Kubwa zaidi kati ya Meli zote za Kijeshi duniani kote. Meli hiyo imepewa jina la aliyewahi kuwa Rais wa 38 wa Marekani, Gerald Ford

Iliingia kwenye Kikosi cha Meli za Jeshi la Wanamaji wa Marekani Novemba 14, 2009 ikiwa ndio Meli inayotumika kubeba Ndege hatari kabisa za Kivita za Jeshi hilo.

1. GHARAMA
Meli hii iliundwa kwa gharama ya Tsh. Trilioni 33.30 na kuifanya kuwa Meli yenye thamani kubwa kuliko zote duniani. Kwa tafsiri rahisi ni kuwa, gharama ya Meli hii ni sawa na Bajeti nzima ya Serikali ya Tanzania kwa mwaka 2019/20

2. UKUBWA WAKE
Meli ya Gerald R Ford ina urefu wa Mita 333, ambayo ni zaidi ya Viwanja Vitatu vya Mpira wa Miguu, Urefu kutoka ndani ya Maji hadi eneo la juu ya Meli ni Mita 76, eneo la juu ambapo Ndege zinaweza kutua na kupaa lina upana wa Mita 78 huku ikiwa na uzito wa Tani 100,000.

3. KASI YAKE (SPEED)
Kwa mujibu wa nyaraka zilizochapishwa, Gerald Ford inaweza kusafiri kwa Kasi ya Maili 35 kwa Saa (MPH sawa na Kilomita 56 kwa Saa au kwa Lugha ya Kibaharia inaweza kwenda kwa zaidi ya 30 Knots.

4. UWEZO WA KUBEBA NDEGE
Hili dude linatajwa kuwa na uwezo wa kubeba Ndege za Kijeshi zaidi ya 75 hadi 90 kwa mara moja na wakati huo bado ikibaki na nafasi ya Uwanja unaowezesha Ndege hizo kupaa wakati ikiwa safarini.

5. MFUMO WA KUJIENDESHA
Meli ya Gerald Ford imewekwa Propela 4 ambazo kila moja ina uzito wa Tani 30. Zina ukubwa wa Futi 21 au Mita 6.1 na zimeundwa kwa Madini ya Bronze au Shaba.

6. KUNA MADUKA NA MIGAHAWA YA STARBUCKS NDANI
Ukiwa ndani ya hii Meli ni kama uko Mtaani tu, unaweza kupata huduma ya Kahawa safi kabisa na haiuzwi, hutolewa bure. Ila tu huduma hiyo imewekwa maalumu kwaajili ya Wanajeshi waliopo ndani ya Meli pekee.

7. GHARAMA ZA UENDESHAJI
Inaelezwa kuwa, matumizi ya jumla ya Meli hii kwa mwaka ni zaidi ya Tsh. Trilioni 10

8. RANGI ZILIZOTUMIKA KUIPAKA
Jumla ya Galons 200,000 za Rangi sawa na Lita 757,082 zilitumika kupaka eneo la nje la Meli hii. Yaani ni kwamba rangi hizo zinaweza kutumika kupaka Majengo ya Ikulu ya Marekani, White House kwa kurudia mara 350.

9. MFUMO WA UMEME NA SILAHA
Meli hii hii inaendeshwa kwa Umeme unaozalishwa na Vitendanishi vya Nyuklia yaani (A1B nuclear reactors), Ina Mfumo wa Umeme Sumaku wa kurusha Ndege za Kivita yaani EMALS, Inabeba Ndege zenye uwezo wa kushambulia bila kuwa na Rubani, Helkopta, Ndege za Ufuatiliaji na Uchunguzi wa Anga pamoja na Ndege aina ya F-35C na F/A-18 zinazotajwa kuwa Ndege hatari zaidi za mashambulizi ya Anga.

Pia, Meli hii ina Mifumo ya Ulinzi yenye uwezo wa kupangua au kutungua Mabomu yanayotumwa kushambulia Meli au eneo la jirani yaani, ESSM, RIM-116, CIWS na DBR.

10. IDADI YA WATU
USS Gerald Ford inaweza kubeba Wafanyakazi wapatao 5,000
 
Wapo Mbali Sana Hao, Sisi Hata Tukipewa Bure Hatuna Uwezo Wa Kuweka Mafuta
Yaani Hao Wapo Mbali Kwa Technology Siyo Sisi Tunaotumia Singe Nyama Italala
Tunapowaambia bado hajazaliwa wa kumsumbua Us watu waelewe
 
Sisi bado tupo kwenye teknolojia ya kuunga unga mabati na vyuma chakavu......sijui ni lini ngozi nyeusi watatambua kwamba matumizi yao ya akili ni duni sana na kuacha mambo ya ubinafsi, uchawa, upendeleo na kuanza kutoa kipaumbele kwa watu wenye vipawa vya akili kwenye kila nyanja ya maendeleo.​
 
Back
Top Bottom