Naibu Waziri Kihenzile Apongeza na Kusifu Kasi ya Maendeleo Chuo cha Taifa cha Usafirishaji

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

NAIBU WAZIRI KIHENZILE ASIFU KASI YA MAENDELEO CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI (NIT)

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Mwakiposa Kihenzile amefanya ziara katika Chuo cha Taifa cha Usafirisha (NIT) ili kujionea na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya Serikali katika Chuo hicho.

Mhe. Kihenzile ametembelea Chuo cha Taifa cha Usafirishaji ( NIT) na kupata fursa ya kujifunza Shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Chuo hicho pamoja na mambo mengine na kusema kuwa amefurahishwa na kazi kubwa ya maboresho inayoendelea.

"Ndani ya kipindi kifupi Chuo kimepiga hatua kwenye kila Sekta, nimetumia nafasi hiyo kumshukuru Mkuu wa Chuo na timu yake pamoja na Bodi ya Chuo. Idadi ya wanafunzi imeongezeka kutoka takribani 3,000 mpaka 15,000 mwaka 2023. Kozi mbalimbali zimeongezwa ikiwemo kwenye urubani, utoaji huduma za ndege, meli na reli." - Naibu Waziri Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile

"Pamoja na kutembelea miradi hiyo kwaniaba ya Waziri wetu, Mhe. Prof. Makame Mbarawa, nimefikisha maagizo yake kuhakikisha miradi yote inayoendelea inakamilika ndani ya Muda uliopangwa na iwe na thamani halisi ili wananchi waweze pata huduma" - Naibu Waziri Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile

Mhe. David Kihenzile (Mb)
Naibu Waziri, Wizara ya Uchukuzi
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-09-30 at 16.05.06(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-30 at 16.05.06(1).jpeg
    288.3 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-09-30 at 16.05.04(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-30 at 16.05.04(1).jpeg
    36.3 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-09-30 at 16.05.04.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-30 at 16.05.04.jpeg
    39.6 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-09-30 at 16.05.03.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-30 at 16.05.03.jpeg
    40.3 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-09-30 at 16.05.05.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-30 at 16.05.05.jpeg
    29.9 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-09-30 at 16.05.06.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-30 at 16.05.06.jpeg
    48.2 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-09-30 at 16.05.09.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-30 at 16.05.09.jpeg
    155.8 KB · Views: 1
Back
Top Bottom