Miradi Mikubwa Inayotekelezwa na Awamu ya 6 Mkoani Kigoma

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,115
49,838
Nitakuwa natoa mfululizo wa makala za Miradi mikubwa ya Maendeleo inayotekelezwa Kila Mkoa.

Ninaanza na Mkoa wa Kigoma.Unaweza sema Kigoma imependelewa au inastahili ila Kwa Sasa ni Kati ya Mikoa michache sana ambayo Ina miradi Mingi sana ya Maendeleo.Ndani ya miaka 3 ya Rais Samia Mkoa huo umepokea zaidi ya Trilioni 11 kwenye sekta mbalimbali za maendelea

View: https://twitter.com/twendenamama/status/1754817745361699253?t=EF5vTb9eawu38wYC6e2qrQ&s=19

Baadhi ya miradi mikubwa ya Maendeleo inayoendelea na utekelezwaji Mkoani Kigoma ni hii ifuatayo,

  • Ujenzi wa Barabara Kuu za lami zaidi ya km 420 zikiwemo za Kibondo-Mabamba na Kibondo-Marongwe
  • Ujenzi wa Barabara za mitaa km 10 chini ya Tactic
  • Ujenzi na Ukarabati wa Bandari ya Lagosa,Kibirizi
  • Ujenzi wa meli Mpya na Chelezo ya Kuundia meli
  • Ukarabati wa meli za mv Sangara na Mv Liemba Ziwa Tanganyika
  • Ujenzi wa Station kuu ya Sgr Kigoma
  • Ujenzi wa SGR Tabora-Kigoma(Main Camp ni Uvinza-Kigoma)
  • Ujenzi wa Soko Kuu la Mwanga na soko la Kato ga via Tactic
  • Ujenzi wa Tawi la Chuo Kikuu Cha Muhimbili
  • Ujenzi wa Tawi la Chuo Cha Uhasibu TIA
  • Upanuzi wa Chuo Cha Taifa Cha Hali ya hewa na Ufungaji wa radar
  • Ujenzi wa Hospital ya Rufaa ya Kanda ya Magharibi
  • Ujenzi,ukarabati na upanuzi wa uwanja wa Ndege wa Kigoma (Gombe-Mahare International Airport)
  • Ujenzi wa njia kubwa ya kusafirisha Umeme wa Kv 400 Nyakanazi-Kidahwe
  • Ujenzi wa Tawi la BoT Kanda ya Magharibi(Usanifu unaendelea)
  • Construction of Katosha Dry Port
  • Ujenzi wa meli Mpya ya abiria na Mizigo
  • Ujenzi wa meli ya Abiria
  • Ujenzi wa Chuo Cha Umahili wa Tehama Buhigwe
  • Miradi kedekede ya Maji ya zaidi ya Bilioni 429
  • Ujenzi wa Malagarasi Hydropower Project

View: https://twitter.com/twendenamama/status/1754391576644645003?t=YOFmCjcfyuRjJJh2Ygan-A&s=19

My Take
Hiyo ni Baadhi tuu ya Miradi mikubwa ya mabilioni ya pesa iliyomwagwa Mkoani Kigoma na awamu ya 6.

Waswahili Wana msemo kwamba kawia ila ufike,Kigoma Sasa wamefika.Hongera sana.

Kumbe ChoiceVariable Ni Muha!!!!!
Kigoma hata mjenge hoteli zenye vyoo vya kukalia, siwezi kuitembelea Kigoma.
Bwege wewe, aliyekwambia Mimi Muha ni nani?

Pili Serikali haitekelezi miradi Mikoani Kwa msingi wa kufurahisha kabila.Kigoma Kuna Watanzania wa makabila tofauti hata kama Waha ndio wengi.

So wewe kenge utembelee au usitembelee unajikosha upepo tuu
 
Bora kua bwege kuliko kuja huko ambàko kila nyumba ya pili Kuna mchawi.
 
Nitakuwa natoa mfululizo wa makala za Miradi mikubwa ya Maendeleo inayotekelezwa Kila Mkoa.

Ninaanza na Mkoa wa Kigoma.Unaweza sema Kigoma imependelewa au inastahili ila Kwa Sasa ni Kati ya Mikoa michache sana ambayo Ina miradi Mingi sana ya Maendeleo.

Baadhi ya miradi mikubwa ya Maendeleo inayoendelea na utekelezwaji Mkoani Kigoma ni hii ifuatayo,

  • Ujenzi wa Barabara Kuu za lami zaidi ya km 420
  • Ujenzi wa Barabara za mitaa km 10 chini ya Tactic
  • Ujenzi na Ukarabati wa Bandari ya Lagosa,Kibirizi
  • Ujenzi wa meli Mpya na Chelezo ya Kuundia meli
  • Ukarabati wa meli za mv Sangara na Mv Liemba Ziwa Tanganyika
  • Ujenzi wa Station kuu ya Sgr Kigoma
  • Ujenzi wa SGR Tabora-Kigoma(Main Camp ni Uvinza-Kigoma)
  • Ujenzi wa Soko Kuu la Mwanga-Tactic
  • Ujenzi wa Tawi la Chuo Kikuu Cha Muhimbili
  • Ujenzi wa Tawi la Chuo Cha Uhasibu TIA
  • Upanuzi wa Chuo Cha Taifa Cha Hali ya hewa na Ufungaji wa radar
  • Ujenzi wa Hospital ya Rufaa ya Kanda ya Magharibi
  • Ujenzi,ukarabati na upanuzi wa uwanja wa Ndege wa Kigoma (Gombe-Mahare International Airport)
  • Ujenzi wa njia kubwa ya kusafirisha Umeme wa Kv 400 Nyakanazi-Kidahwe
  • Ujenzi wa Tawi la BoT Kanda ya Magharibi(Usanifu unaendelea)

My Take
Hiyo ni Baadhi tuu ya Miradi mikubwa ya mabilioni ya pesa iliyomwagwa Mkoani Kigoma na awamu ya 6.

Waswahili Wana msemo kwamba kawia ila ufike,Kigoma Sasa wamefika.Hongera sana.

Safi sana . Kigoma ilikuwa imepunjwa sana.

Nimeshafika Kigoma. Ina kaubaridi kazuri, ni "nchi" nzuri sana.
 
Kumbe ChoiceVariable Ni Muha!!!!!
Kigoma hata mjenge hoteli zenye vyoo vya kukalia, siwezi kuitembelea Kigoma.
Mkuu, usiichukulie Kigoma "poa!". Unaweza usitake kuitembelea, lakini ikakulazimu kwenda. Wewe unabagua pa kupatia "maokoto?"

Unaweza usivutiwe na utalii wa Kigoma, lakini ukavutwa na "maokoto" yake manono.

Kigoma ni miongoni mwa mikoa yenye fursa ambayo ambayo bado haijafichuliwa.

~ Ardhi kubwa inayofaa kwa kilimo
~ Vyanzo ya uhakika vya maji
~ Vivutio vya kitalii
~ Mapori yenye miti mingi
~ N.k.

Halafu, kuna tetesi kuwa huenda kuna mafuta kando kando mwa mto Malagarasi. Endapo hilo litatokea, unafikiri Kigoma itafanania wapi kama si kuuzidi mkoa wa Dar Es Salaam kwa maendeleo?

Kigoma ni mkoa uliojaa fursa kwa wenye "macho" yanayoona.
 
Back
Top Bottom