Miradi ya Hayati Magufuli inavyowakosesha amani wapinzani. Hata baada ya kifo chake Bado kivuli chake kinawatesa

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,502
4,408
Kila Kona ya nchi Sasa ni mtetemo na mtikisiko ikienda sambamba na tabasamu la kumalizika Kwa miradi iliyoanzishwa wakati wa utawala wa Hayati Magufuli. Ni juzi tumeambiwa mtambo namba 8 wa kuzalisha umeme katika bwawa la JNHPP umewashwa na kuwashwa huko tatizo la umeme litapungua Kwa 85% ,hii ni habari njema na ya matumaini makubwa. Hamu inaendelea kuwa kubwa endapo mitambo yote 9 ikiwashwa na kuanza kuzalisha umeme ,Je matokeo yake yatakuwaje?

Hilo likiwa halijakauka ,habari njema zaidi ni kuanza Kwa majaribio ya SGR kutoka Dar mpaka Moro, majaribio ambayo yamefanyika Kwa mafanikio. Kuanza kufanya kazi Kwa SGR uchumi wa Tanzania utafunguka Kwa kiwango kikubwa.

Miradi hii ,wa kufua umeme na SGR ni pigo litakaloikumba upinzani na Kwa sababu hawaoni wataendelea kuona watanzania wanataka maandamano. Watanzania wanataka maendeleo na maendeleo yanayoletwa na Serikali ya CCM ni ya vizazi Kwa vizazi.

Miradi mikubwa yote ambayo hapo kabla ili " white elephant projects" na wapinzani Sasa imekuwa miradi yenye matokeo mazuri kwenye uchumi. Miradi hiyo itautesa upinzani Kwa miaka mingi sana na kama upinzani wataendelea kuzurura bila ajenda ,sioni mwisho kwao.

Mwenyezi Mungu mpe pumziko jema mja wako , matokeo ya kazi ngumu Kwa nchi hii tumeanza kuyaona Sasa.
 
Mungu amenipatia mtoto wa kiume usiku wa kuamkia leo, nimemuita jina la Magufuli

Potelea mbali, nataka nimlee kama alivyolelewa JPM, nami nitadhulu chato hasa kuongea na mzazi wa JPM kunielekeza jinsi ya kulea mwanangu ili siku moja aje kuwa kama alivyokuwa JPM
 
MUNGU MUREHEMU HAYATI MAGUFULI KWA MEMA ALIYOTUTENDEA WALANIWE WOTE WANASIASA UCHWARA KAMA AKINA LISSU,LEMA, MBOWE NK wale wanaomtukana kila siku bila hata aibu hakika Mungu umetupa funzo kutupa MAGUFULI NA KUTUONDOLEWA MAPEMA KWANI TULIMHITAJI ZAIIDI AJENGE NCHI YAKE KWA FAIDA YA WANANCHI WAKE.RIP MAGUFULI
 
Back
Top Bottom