Mikopo ya Hayati Magufuli tumeuiona je mikopo ya Rais Samia iko wapi

Mdude_Nyagali

Member
Dec 11, 2022
60
1,237
Magufuli kwa miaka 5 aliyokaa madarakani alikopa trillion 37 akajengea SGR, bwawa la Nyerere, akanunua ndege, Kijazi interchange ubungo na 6 way mpaka Mbezi mwisho.

Magufuli hata kama aliiba lakini angarau alionyesha matokeo ijapo aliwadanganya wananchi kuwa matokeo hayo ni pesa zetu wenyewe wakati zilikuwa za mkopo.

Samia kwa miaka mitatu kakopa trillion 30 pesa kapeleka wapi? Miradi aliyoiacha Magufuli mingi ni kama imekwama.

SGR yenyewe inasua huku wafanyakazi wakifanya migomo kwa kutolipwa mishahara yao. Upande wa pili tren yenyewe ya SGR imechakachuliwa, tumeletewa tren iliyotumika kwenye movie ya Escape From Sobibor mwaka 1987 tukaambiwa ni tren ya mwendokasi. Ni juzi tu kwenye majaribio yao kutoka Dar mpaka Morogoro tren hiyo ilitumia takribani masaa manne sehemu ambayo ilitakiwa kutumia lisaa limoja. Kwa ufupi ni kwamba ukitaka kufika haraka ni heri upande Ngorika kuliko hili tren la Escape From Sobibor.

Sasa kwa mazingira haya ya utawala wa Samia wa kukopakopa na pesa zinaishia kuibiwa kwanini tusimuambie ajiuzulu? Binafsi naona Samia uwezo wake wa kiutendaji ni mdogo fikiria naye analalamika pesa zinaibiwa na yeye ndio mwenye mamlaka kikatiba kulinda pesa za umma na rasilimali za taifa.

Sasa ni muda wa kumlazimisha Samia ajiuzulu kupitia maandamano.

Asante.

Mdude Mpaluka Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.

GridArt_20240316_080959492.jpg
 
Kwa mtu ambaye amezoea kucheza kwenye matope ya uyole huko mbeya hawezi kuelewa, hasa kama akili yake nzito kama tope la.masika la huko Uyole.

Magufuli alikuwa anajiingiza katika miradi mikubwa kwa kukopa kidogo kidogo, anakopa ajenge reli mpaka morogoro, lakini anakopa kwanza reli ilfike mkoa wa pwani, lakini mkataba unasoma morogoro, kwa hiyo mkandarasi anajua ana kazi ya morogoro, halafu JPM ana hela ya kujenga mpaka pwani.

Hata Stiglers, amekopa kopa kwa vipande vipande, lakini kwenye karatasi inasomeka gharama ya mradi kwa jumla. Kwa hiyo SSH lazima aonekane kakopa upya, kumbe amekopa kwenye mkataba ambao ngombe kama Mdude zinajua hela zake zipo
 
Magufuli kwa miaka 5 aliyokaa madarakani alikopa trillion 37 akajengea SGR, bwawa la Nyerere, akanunua ndege, Kijazi interchange ubungo na 6 way mpaka Mbezi mwisho...
ungeakua na ka credibility kidogo hata mie ningekuskiza na pengine kukuunga mkono,

hivi kupuliza umeacha kabisa saivi 🐒

wewe kama ni mwanaume kamili kweli, unaejielewa na kujitambua, sio mtu wa kupuliza cha Arusha au wa kutumwa tumwa na kubebwa bebwa ung'ombe 🐒

wewe ni chadema au sauti ya waTanzania 🐒
 
Kwa mtu ambaye amezoea kucheza kwenye matope ya uyole huko mbeya hawezi kuelewa, hasa kama akili yake nzito kama tope la.masika la huko Uyole...
Mkuu Swali la Mdude ni Muhimu sana ukalijibu badala ya kujikita kwenye Matusi na personal attack.......aidha watu watamwamini Mdude kuliko wewe unayemwaga maneno matupu.

Nyangali amesema Dr JPM alikopa na miradi michache imeonekana kwa macho.

Sasa wajibu wako ni kuonesha muradi iliyojengwa kutokana na mikopo ya kipindi cha Dr Samia.

Hii inatosha kueleza uwezo wako wa kujadili jambo.
 
Wewe hunaga akili inayofanya kazi.wewe ni jinga jinga tu usiyejitambua. Wewe si ndio ulikuwa ukimtukana muda wote matusi ya kila aina na hata alipokufa ulishangilia na kufurahia sana kifo chake? Yaani wewe kukosa malezi ya mama yako tokea udogo wako kumekufanya uwe kama taira na uliyekosa adabu kabisa.ndio maana muda wote unafanya kazi ya kuropoka ropoka na kutukana matusi kama kichaa au mwendawazimu.

Ukome kabisa kutoa maneno yako ya kijinga jinga kwa Mheshimiwa Rais .usifikiri unaogopwa au una nguvu sana.huna akili kabisa wewe

Bwawa la Mwalimu Nyerere liliachwa likiwa katika hatua za mwanzo kabisa ambapo Mheshimiwa Rais Samia angeamua hata kulitelekeza angeweza kufanya hivyo kwakuwa lilikuwa bado linahitaji fedha nyingi sana.lakini kwa ujasiri ,uimara,uhodari, ushupavu na umadhubuti wake alifanya kazi kubwa sana kuhakikisha kuwa linakamilika lote.ambapo mpaka sasa lipo ukingoni kabisa.na tayari megawati 235 tayari zimeiva kutoka mtambo namba tisa.na pia muda siyo mrefu zingine tena megawati 235 zitapelekwa kuunganishwa katika grid ya Taifa na kufanya kuwa megawati 470.kiwango kikubwa ukilinganisha na kile kinachopatikana kutoka mabwawa mawili ya Mtera megawati 80 pamoja na kidatu megawati 204.

Ukija kwenye reli ya SGR nako umefanya upotoshaji mkubwa sana kwa kusema kuwa kuna wafanyakazi wamegoma kufanya kazi.jambo hili ni uzushi na uongo mkubwa sana.kwa sababu kazi inaendelea kwa kasi kubwa sana na kufika mwezi wa sita kazi itakuwa mbali sana katika kukamilika kwake.ndio maana majaribio ya treni yalifanikiwa vyema sana.

Lakini pia kusema kuwa treni iliyonunuliwa ni ya zamani.nalo pia ni uongo mkubwa sana kwa sababu treni yetu na mabehewa yake ni ya kisasa kabisa yanayokidhi ubora unaohitajika.umeongea tu kwa kuropoka kama kawaida yako kutokana na kukosa kwako akili kichwani.

Ni wakati wa Rais Samia tumeshuhudia ujenzi wa vituo mbalimbali vya afya hapa nchini, hospitali za wilaya,mikoa ,kanda pamoja na rufaa .hii ndio sababu tunaona hata ripoti zikitoka juu ya kuongezeka umri wa kuishi kwa mtanzania kutokana na kuboreshwa kwa huduma za afya.kwa kuwa ndani ya muda mfupi wizara ya afya kumewekezwa zaidi ya Trilioni sita kama ilivyo kwa ofisi ya Rais TAMISEMI.

Ukienda katika Secta ya Elimu nako ni mapinduzi makubwa ambako shule mpya pamoja na madarasa ya kutosha kwa shule zilizokuwepo vimejengwa ,hii ndio sababu kwa sasa wanafunzi wote wanaripoti kwa wakati mmoja tena wengine wanafuatwa majumbani ili waende shule kusoma bure kabisa baada ya kuwa serikali ya Rais samia inatoa Billion 33 kila mwezi kugharamia Elimu bure.

Mbeya kwenyewe kunakwenda kujengwa barabara ya njia nne kutoka igawa mkoani Mbeya mpaka Tunduma mkoani Songwe yenye urefu wa kilomita 237.9 .ambapo kila kitu kipo tayari ikiwepo pesa za kazi hiyo.

Ajira zimetolewa kwa maelfu kwa vijana ndani ya muda mfupi.hakuna sehemu ambako utakwenda usikute uwekezaji na mikono ya Rais Samia .

Hapo sijazungumzia habari za ufanisi wa ukusanyaji mapato,kuongeza mishahara kwa watumishi wa umma,kujenga uchumi unaogusa maisha ya watu, demokrasia na mengine mengi sana,maana maendeleo ni yale yanayogusa maisha ya watu kitu ambacho kimefanywa kwa ufanisi na Rais Samia..

Punguza hiyo mibangi unayovuta kama kichaa au mwendawazimu jinga wewe.
 
ungeakua na ka credibility kidogo hata mie ningekuskiza na pengine kukuunga mkono,

hivi kupuliza umeacha kabisa saivi 🐒

wewe kama ni mwanaume kamili kweli, unaejielewa na kujitambua, sio mtu wa kupuliza cha Arusha au wa kutumwa tumwa na kubebwa bebwa ung'ombe 🐒

wewe ni chadema au sauti ya waTanzania 🐒

Jibu hoja zake au kaa kimya
 
Jibu
Kwa mtu ambaye amezoea kucheza kwenye matope ya uyole huko mbeya hawezi kuelewa, hasa kama akili yake nzito kama tope la.masika la huko Uyole...
Jibu hoja yake acha kutoa sababu zisizo sehemu ya mjadala!!, vinginevyo utakuwa shoqer uliyeathirika.
 
Wewe hunaga akili inayofanya kazi.wewe ni jinga jinga tu usiyejitambua. Wewe si ndio ulikuwa ukimtukana muda wote matusi ya kila aina na hata alipokufa ulishangilia na kufurahia sana kifo chake? Yaani wewe kukosa malezi ya mama yako tokea udogo wako kumekufanya uwe kama taira na uliyekosa adabu kabisa.ndio maana muda wote unafanya kazi ya kuropoka ropoka na kutukana matusi kama kichaa au mwendawazimu.

Ukome kabisa kutoa maneno yako ya kijinga jinga kwa Mheshimiwa Rais .usifikiri unaogopwa au una nguvu sana.huna akili kabisa wewe
Kaka Lucas umejibu hata hoja moja ya Mdude?

Kwanini maelezo mengi ya kufoka wakati ungetumia mistari miwili au mitatu kujibu Maswali yake?

Ndio Maana Dr Samia kawakataa Chawa mnamwaibisha.

Swali rahisi hilo. Onesha miradi iliyotokana na mikopo kipindi cha Dr Samia
 
Jibu swali la Mdude....Miradi iliyotokana na mikopo iko wapi? Ya Hayati Dr Magufuli inaonekana hata kama ina mapungufu.
siwezi ata kusoma,
heading inatosha kumuelewa ila sasa,
nataman kujua credibility yake kwanza maana tulipuliza pamoja, je mwezangu bado anaendelea 🐒

na yupo chadema au sauti ya waTanzania, akili na uwezo wake unafahamika ni bila kutumwa na kushikwa mno apo ni moshi wa Arusha TU 🐒
 
Credibility inajengwa na uzito wa hoja zake. Zisipijibuwa wewe ndio unakosa hiyo credibility sio yeye tena.
 
Kaka Lucas umejibu hata hoja moja ya Mdude?

Kwanini maelezo mengi ya kufoka wakati ungetumia mistari miwili au mitatu kujibu Maswali yake?

Ndio Maana Dr Samia kawakataa Chawa mnamwaibisha.

Swali rahisi hilo. Onesha miradi iliyotokana na mikopo kipindi cha Dr Samia
Kuna hoja gani kwa huyo mjinga asiyejitambua? Umesahau matusi aliyokuwa anamtukana hayati dkt Magufuli? Umesahau alivyosherehe hadi kifo chake? Sasa unaanzia wapi kumsikiliza huyo punguani?
 
Back
Top Bottom