Miradi na mipango mikubwa ya kimkakati ni kaburi la siasa za upizani, hili la bandari ni mojawapo. Rais songa mbele matokeo ni mazuri

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,601
Hata nikiamshwa usingizini na nikaulizwa ni mambo yapi yamtambeba Rais Samia au mgombea yeyote wa CCM kwenye uchaguzi mkuu ujao kabla ya kupepesa jicho nitakuambia yafuatayo:

Kwanza, furaha na matarajio ya Wananchi. Hapa kuna masuala ya huduma bora, maslahi bora na maisha bora.

Pili, uzalishaji wa ajira kwa wingi. Kila kada imeguswa kwa ajira lukuki achilia mbali ajira za muda mfupi.

Tatu, miradi na mipango ya kimkakati ya uwekezaji. Hapa ndio yanaguswa zaidi mambo yenye maslahi mapana ya Taifa.

Nne, utawala wa Sheria na katiba. Hapa tunazungumzia mabadiliko na maboresho ya sheria na kuunda tume maalumu ya kutathmini mfumo wa haki jinai.

Mambo haya yote ni mwiba mchungu kwa siasa za upinzani kwa sababu zinaweka imani kubwa kwa siasa za Chama tawala.

Tukiachana na yote hayo ,leo nitajikitika zaidi kwenye suala la miradi na mipango mikubwa ya kimkakati ya uwekezaji ambayo imegeuka ni kaburi la siasa za upinzani.

Serikali ya awamu iliyopita ilitumia kwa kiwango kikubwa sana mbinu hii na matokeo yake yakaonekana kwenye uchaguzi mkuu wa 2020 na siasa za upinzani za kupinga utekezaji wa mikakati hii hazijaanza kwenye hili la bandari lipo enzi na enzi ila maamuzi ya Wananchi kwenye chaguzi ndio yanayothibisha siasa za upinzani zina hofu ya kukubalika kwa Chama tawala kuliko hofu waliyonayo kweli.

Faida ni nyingi sana kwa wananchi kuliko hasara na ndio maana kelele za wanasiasa ni nyingi kuliko Wananchi.

Hili la bandari ni kaburi la zege kwenye siasa za upinzani maana litaenda kukata pumzi ya upinzani kwa kipindi kirefu. Kila nikiangalia faida za utekelezaji wa makubaliano ya bandari na DP world naiona Tanzania mpya inakuja.

Kwa kuwa matokeo yatakuwa ni makubwa na mazuri ziadi ,nakutia moyo Rais wangu baada ya matokeo wanaopinga sasa nao watakuwepo mezani kushangalia na wengine wasiamini.

Miradi ya kimkakati ya uwekezaji ndio muafaka kwa Taifa kwa sasa na baadaye.
 
mwaarabu hana cha kupoteza ila watanzania
Hakuna cha kupoteza ndugu yangu. Faida ni nyingi sana ,bandari itachangia 67% ya mapato kutoka 37% maana yake Kodi nyingi zinazowagusa watu moja kwa moja zitapunguzwa ama kuondolewa.

Pia, Serikali itaondokana na utegemezi wa mikopo kwenye bajeti na inawezekana kabisa Tanzania kuwa na ' balanced budget' na hivyo kufanya deni la Taifa kutoongezeka.
 
Hakuna cha kupoteza ndugu yangu. Faida ni nyingi sana ,bandari itachangia 67% ya mapato kutoka 37% maana yake Kodi nyingi zinazowagusa watu moja kwa moja zitapunguzwa ama kuondolewa.

Pia, Serikali itaondokana na utegemezi wa mikopo kwenye bajeti na inawezekana kabisa Tanzania kuwa na ' balanced budget' na hivyo kufanya deni la Taifa kutoongezeka.
Naomba mgao
 
Back
Top Bottom