BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,023
PATHETIC! Shame on you.
Tundu Lissu hana huruma na Tanzania kabisa.
View attachment 1547398
====
Wistleblowers Investigation Worldwide (WIW) imeibua mapya kwenye barua yake ya wazi kwa rais wa JMT na waziri Kabudi kwamba ubia wa Amsterdam na TL nia yake ni kuivuruga Tanzania. WIW inasema ina ushahidi wa kiuchunguzi unaothibitisha mkakati wenye nia ovu kwa Tanzania baina ya Amsterdam, TL na baadhi ya taasisi za kimataifa za kuvuruga uchaguzi Mkuu wa 2020. Amsterdam aliwahi kufanya hivyo katika nchi za Togo (2010), Guinea (2010) na Taiwan (2018). Mwaka 2016 kituo cha habari cha Aljazeera kilitoa taarifa ya kuichunguzi kuhusu vurugu zilizochochewa na Amsterdam katika nchi hizo kwenye taarifa iliyopewa kichwa cha habari "the election parasite web" ambayo ilipigwa marufuku siku chache baada ya kuwekwa hadharani.
WIW imeenda mbali kwa kuandika kwamba kupigwa risasi TL ni mpango uliosukwa mwaka 2017 na yeye mwenyewe akishiriki. WIW inasema inao ushahidi wa TL kukutana na taasisi za Ulaya nchini Tanzania mwezi March 2017 na kupanga njama dhidi ya serikali ya JMT. WIW wanamuhakikishia rasi wa JMT kwamba yataibuka makubwa zaidi kuhusiana na njama hizo siku za karibuni.