Amani Msumari
JF-Expert Member
- Aug 21, 2016
- 1,830
- 976
Waungwana, na ijulikane leo kuwa mimi binafsi nimekataa kuwa sehemu ya Watanzania watakaosema tusamehe Magufuli, hatukujua kuwa wewe ni mtu muhimu kwetu Watanzania.
Anyway, hivi mnakumbuka hali ilikuwaje kipindi cha Kikwete? Wengi wa wapiga ramli walifikia mpaka hatua ya kutabiri kuwa CCM itamfia Kikwete mikononi mwake. Nadhani pia hamjasahau lawama za ugumu wa maisha zilizokuwa zinamiminwa kwa hayati Rais Mkapa.
Leo hii wapinzani wanawasifu Mkapa na Kikwete kwa sifa ambazo hawakuwahi kuwapa kipindi wanatawala. Waliwalaumu sana na kelele zilikuwa nyingi mno. Wapo waliosema I am sorry Mkapa, I am sorry Kikwete. Leo hii viongozi hawa wanaonekana ni mashujaa.
Tuache mambo mengi aliyoyafanya Magufuli ambayo yanaongelewa sana, hebu tuseme haya machache ambayo hayasemwi sana lakini yenye umuhimu sana kwenye maisha ya kila siku ya Watanzania.
Serikali ya Magufuli imefanya jitihada kubwa kwenye kudhibiti mfumuko wa bei na kupunguza kodi ya mshahara (PAYE) kwa wafanyakazi. Mambo haya yanagusa maisha ya Watanzania moja kwa moja. Haya sio mambo madogo, ni makubwa mno.
Hebu kaa uchunguze bei za vitu mbalimbali tangu alipoingia Magufuli. Achana na hujuma za sukari, angalia nauli, bei za vifaa vya ujenzi n.k. Ikumbukwe kuwa kilio cha kutaka punguzo la Kodi mpaka kufika single digit kilikuwepo muda mrefu.
#2020 kura zote kwa John
Amani Msumari
Tanga