Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,129
- 35,152
Kwanza kabisa napenda kuweka kumbukumbu sawa, mimi ni miongoni mwa member wa JF ambaye sikuwahi kumkubali Magufuli na mara zote (mpaka sasa hivi) nimepingana na siasa chafu na siasa za kikatili zilizokuwa zikifanywa na Magufuli na utawala wake, yaani mimi ni against Magufuli. Kwangu mimi rais Samia ni bora zaidi kuliko Magufuli, japokuwa wote wawili hawastahili kutuongoza sisi watanzania.
Kuna mambo kadhaa Magufuli (maono yake au maono ya waliomtangulia lakini yalikuwa yamekufa akayafufua) aliamua kuyaibua, kuyasimamia kwa nguvu kubwa, mengine ya kipuuzi kabisa lakini kwa bahati mbaya akafa kabla ya kukamilika, na aliyemfuata (Rais Samia) amepambana kuyatekeleza na mengine bado anapambana kuyatekeleza huku utawala huu wa Samia ukikwepa sana (kimakusudi) kumtaja au kumwagia sifa Magufuli katikati ya mambo hayo. Hii sio sawa, sio haki na wala sio heshima. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, Magufuli apewe heshima yake katika mema yake. Hapa chini nitataja baadhi ya maono ya Magufuli.
1. Kuhamia Dodoma.
2. Ujenzi wa Ikulu ya Chamwino
3. Ujenzi wa bwawa la umeme la Nyerere
4. Kukuza lugha ya Kiswahili
5. Ujenzi wa reli ya SGR
6. Ujenzi wa daraja/kivuko cha Kigogo Busisi
Nimesukumwa kuandika hapa leo baada ya kusikia kuwa kuna ujenzi utaendelea ndani ya Ikulu mpya ya Chamwino, Dodoma ambapo utahusisha jengo jipya na kubwa la kisasa ambalo litaitwa Samia Complex, binafsi sijafurahishwa na hilo neno. Kwa heshima kubwa ingepaswa hilo jengo liitwe Magufuli Complex kwa sababu kuu mbili kuu.
1. Kulinda heshima ya Magufuli aliyewekeza nguvu na akili zake ili kujengwa hiyo Ikulu, na akajilazimisha kuhamia moja kwa moja hata kabla ya Ikulu kukamilika.
2. Kwa sasa Magufuli ni marehemu, na ndio kipindi bora zaidi cha kutumia jina lake kwa yale yanayomstahili kumpa heshima yake kuliko wakati mhusika akiwa hai kwa kuwa huenda mhusika angebadilika na kuja na sifa nyingine mbaya ambayo ingeharibu taswira nzima ya vitu vilivyoitwa kwa jina lake.
Kama Rais Samia naye anataka au tunataka vitu fulani vya kudumu viitwe kwa jina lake ili kumkumbuka na kumpa heshima yake basi asubiri kwanza siku akitoka madarakani au akitangulia mbele za haki tutampa. Sio haki na busara kujipendelea wakati ukiwa madarakani, hata Magufuli alikosea sana kujipa majina ya vitu vya kudumu wakati akiwa bado madarakani, mfano wa stendi ya mabasi ya mikoani ya Dar pale Mbezi. Pia Magufuli alikosea sana kubeza, kufifisha, kufunika na kushindwa kutambua maono ya mtangulizi wake (Kikwete).
Kile kilikuwa ni kitendo kibaya sana na huenda hichi kinachoendelea sasa ni kisasi dhidi ya Magufuli kwa uovu ule alioufanya dhidi ya Kikwete.
Binafsi ninaona Kikwete alijitahidi zaidi kuutambua mchango wa mtangulizi wake (Mkapa) na pia alijenga msingi mzuri wa mipango endelevu kwa aliyemfuata (Magufuli).