Hayati Magufuli aliwezaje kuwa Waziri kwa miaka 20 bila kutumbuliwa?

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
3,510
7,755
Kwa watoto wadogo na wasiojua mambo wanadhani hayati Magufuli alianza kuwa mkali alipokuwa rais wa nchi tu wakati ukweli ni kwamba Magufuli alikuwa mkali na mfuatiliaji tangu akiwa naibu waziri, waziri na baadae rais wa nchi.

Katikati ya mafisadi wakubwa wa awamu za Mkapa na Kikwete lakini walimwogopa Magufuli na aliwashughulikia kila wizara aliyopelekwa, kwa waliokuwepo kwenye wizara ya uvuvi, aridhi na ujenzi enzi za waziri Magufuli watakwambia moto wake.

Swali la kujiuliza aliwezaje kutekeleza bila kutumbuliwa? Je kwenye baraza la mawaziri la sasa kuna waziri anayevaa viatu vyake? Hata baada ya kuwa rais na kufariki dunia mpaka leo miaka 2 imeisha si Chadema , ACT Wazalendo wala CCM waliokuja na ushahidi usiotia shaka juu ya ufisadi wake licha ya kwamba waliahidi pindi tu atakapotoka madarakani basi watakuja na mikataba ya ufisadi na rushwa kubwakubwa zilizosainiwa na yeye.

Mwezi march 2023 imetimia miaka miwili tangu atutoke duniani lakini mahasimu wake ikiwemo ,Lisu, Lema , Nape ,Makamba, Kigogo bado hawajawaletea watanzania ufisadi wa Magufuli.

kinyume chake wanaendeleza mafanikio na miradi ya awamu ya tano kwa kasi kubwa, walipinga kila kitu lakini sasa wanatumia kila kitu walichokipinga! Mbowe akimaliza kutukana anakimbilia kupanda ndege mpya ya Dreamliner impeleke KIA.

Walioahidi kuifunika legacy kumbe hawana uwezo kuifunika hata kidole chake tu!!

Muda utawaumbua zaidi.
 
Rest easy Mr. President 🙏🏿🙏🏿🙏🏿
IMG-20230317-WA0161.jpg
 
Ni kweli kabisa Hayati JPM alikuwa mkali tangu akiwa naibu waziri, alikuwa mkali sana na mfuatiliaji, hulka ya watanzania huwa hawapendi mtu mkali na mfuatiliaji kwasababu anawakosesha uhuru wa kuiba.

Tunawaomba viongozi wetu kuwa wakali na wafiatiliaji kwenye mambo ya msingi.
Kuna baadhi ya watendaji hawaendi bila mjeledi.

Tusioneane muhali Wala kuchekeana kwenye mambo serious ya nchi.

Tunamuombea Mungu Rais wetu azidi kuwa makini na mkali kwenye mambo ya msingi lakini pia wasaidizi wake wakuu, Makamu wake na waziri Mkuu lazima pia wawe wakali ili Ufisadi na ubadhirifu wa fedha za umma ukome.
 
Ajabu ni kwamba
wanasema alikua hafai hata kidogo

Ilihali miradi yake inadendelezwa.
sidhani kama mtu anaweza kusimama na kuwaambia wananchi magufuli alikua mbaya na wakamwelewa
zaidi na zaidi itamfanya aonekane mnafiki na kujijengea picha mbaya na wananchi watamchukia tu
Uwezo wa kiakili wa wananchi wengi ni mdogo
 
Benja kamlea na JK Mr born in town kamlea sana mpk kampatia KITI na kusema nimewaleteeni chuma kweli kweli. Baada ya hapo ETI kinyago walicho kichonga kikaanza kuwatisha. MUNGU FUNDI bhana.
 
Kuna mtu kaniuliza niulize kuhusu sakata la uuzwaji wa nyumba za serikali huko hali ilikuwaje kwa aliyekuwa na dhamana ya wizara?
 
ili udumu Tz hutakiwi ujitume kwenye kazi unatakiwa uwe chawa na uyafanye anayo yapenda boss wako, labda na yeye alifanya hivyo
 
Ni kweli kabisa Hayati JPM alikuwa mkali tangu akiwa naibu waziri, alikuwa mkali sana na mfuatiliaji, hulka ya watanzania huwa hawapendi mtu mkali na mfuatiliaji kwasababu anawakosesha uhuru wa kuiba.

Tunawaomba viongozi wetu kuwa wakali na wafiatiliaji kwenye mambo ya msingi.
Kuna baadhi ya watendaji hawaendi bila mjeledi.
Alipochukua mamlaka isiyo yake ya kutoa roho katika miili ya walioumbwa na Mungu, ndipo yote mema yalipofutika juu yake. Kamwe Mungu anapokuinua usijaribu kumpinga Kwa kutoa roho zisizo na hatia kisa tu wanapinga Kwa maneno matendo yako.
 
Back
Top Bottom