Mimi Masudi Kipanya na safari yetu ya miaka 100

KUTOKA DHUHR HADI ALASIRI NA MASUDI ''MTU SPECIAL'' KIPANYA

Leo ilikuwa siku makhsusi yaani special sana kwangu kwa kuwa katika chumba kimoja na Masudi Kipanya na vijana wake ''sharp'' wa Clouds Plus.

Hiki kwa hakika si chumba kwa maana ya chumba kama tulivyozoea bali ni Maktaba ya Elite Bookstore Mbezi Samaki.

Masudi Kipanya alinikaribisha ndani ya Maktaba hii nadhifu sana si kwa kuangalia na kusoma vitabu bali kwa ajili ya kufanya kipindi cha televisheni.

Mvua kubwa iliyonyesha kipindi cha adhuhuri kwa kiasi cha saa moja hivi ilitosha kunionya kuwa ile ilikuwa tahadhari kwangu kwa mfano wa ''thunder and lightning,'' (radi na kimulimuli) katika mchezo wa Mcbeth kuwa mchana wangu hautakuwa wa kawaida.

Kwa muda wa saa mbili Masudi Kipanya akitembea katika mengi niliyopata kuandika katika historia ya Tanganyika alinirudisha nyuma miaka 100 hapa hapa Dar es Salaam ya 1920s akitaka kujua maisha ya wazee wangu waliosukuma gurudumu la historia ambayo si wengi wanaifahamu.

Masudi Kipanya kama ni mchezo wa masumbwi nitamwita, ''South Paw,'' kwa jinsi alivyonitaabisha na maswali ya kushtukiza na wakati mwingine kunibana nisema nisiyopenda kusema na wakati mwingine kunitoa kwa haraka katika niliyodhani yangefaa kusemwa.

Muda ulikwenda kwa haraka sana jua likazama nikiwa sina habari na hatujamaliza safari yetu ya miaka 100.

View attachment 1755166
Kumbe bado kijana!
 
Huyu mzee ni baharia kweli af watu wanamchukuliaga labda ustaadh flan ao ukisikia wazee wa kitengo kitambo ndio hao sio fala huyu Mzee nashangaa kuna madogo wanamchukuliaga poa

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
Dude...
Nakusoma katikati ya mistari.

Akili yako inakataa kukubali kuwa unachosoma kinatoka kwa mtu aliyepata elimu ya juu
Kumbe bado kijana!
Kolola,
Wallahi nacheka peke yangu.
Mimi ni mzee nina miaka 69.

Mama yako hapa nikikosea jambo nasema mie nishazeeka nisameheni jibu lake ni, "Una uzee gani unatufanyia karaha unasingizia uzee!"

Ngoja nitakuwekea picha ya ujana wangu In Shaa Allah.

Studio za BBC Glasgow, Scotland 1991.

20210418_195154.jpg
 
View attachment 1755714
Kumbe 69 mie 70 ujue! Nilikuwa nakuita mzee nilifikiri Upo kati ya 85-90
 
Oto...
Sina kawaida ya kumkejeli mtu wala kujaribu kumfanya ajihisi si lolote si chochote.
Hapakuwa na haja ya hiyo ''kwikwikwi.''

Hakuna radio mashuhuri duniani ambayo haijanitafuta kufanya mahojiano na mimi.

View attachment 1755319
Hapa niko BBC Glasgow, Scotland 1991

View attachment 1755320

Hii ni V o A Washington 2011

View attachment 1755324
Radio Iran, Tehran 2007

View attachment 1755325
Hawa ni TBC 7 April 2021

View attachment 1755326
AZAM TV 2015
Mungu akujaalie umri mrefu na afya yenye faida na we. Ilikua haina haja hata ya kujielezea kwa watu wasiofuatilia maswala ya nchi yetu ilipotoka na inapokwenda (Watu wanaoendeshwa na kejeli badala ya kuendeshwa na kutafuta elimu).

Sisi tunao kufahamu, japo ni wadogo na hatujafikia umri wa miaka 30+, hatuhitaji maelezo kuhusu uwezo wako wa historia na ulioyaandika na kuyafanya. Tunakufahamu Mohamed Said kupitia vitabu na makala zako zenye madini ya kila aina, na tunatambua uwezo wako mungu aliokujaalia. Mashaallah.

Ramadhan Kareem.
 
Huyu mzee ni hazina ya taifa katika Historia yetu. Niliwahi kumsikiliza akitoa mhadhara katika Chuo Kikuu cha Northwestern kule Chicago. Yuko vizuri sana na msimchukulie poa...Ndiyo ameegemea kwenye Uislamu lakini pia ni vigumu kuwatenga wazee wake na Historia ya awali ya Nyerere na ukombozi wa Tanganyika na wazee wake Waislamu akina Sykes na wengineo.
 
Ila Mzee BBC Scotland unasema ilikua 1991 wakati picha inasema 2007!

Ufafanuzi tafadhari!
Mg,
Wakati napiga picha hii 1991 camera zetu zilikuwa za kuweka Kodak Film kisha unasafisha negative.

Zilipokuja digital camera nikawa nacopy picha zangu ili nizihifadhi katika computer.

Hiyo ndiyo sababu umesoma tarehe hiyo kwenye copy ya picha niliyopiga 1991.
 
Huyu mzee ni hazina ya taifa katika Historia yetu. Niliwahi kumsikiliza akitoa mhadhara katika Chuo Kikuu cha Northwestern kule Chicago. Yuko vizuri sana na msimchukulie poa...Ndiyo ameegemea kwenye Uislamu lakini pia ni vigumu kuwatenga wazee wake na Historia ya awali ya Nyerere na ukombozi wa Tanganyika na wazee wake Waislamu akina Sykes na wengineo.
Shimba,
Kumbe ulikuwapo siku ile kwenye ukumbi wa Eduardo Mondlane!
 
Mungu akujaalie umri mrefu na afya yenye faida na we. Ilikua haina haja hata ya kujielezea kwa watu wasiofuatilia maswala ya nchi yetu ilipotoka na inapokwenda (Watu wanaoendeshwa na kejeli badala ya kuendeshwa na kutafuta elimu).

Sisi tunao kufahamu, japo ni wadogo na hatujafikia umri wa miaka 30+, hatuhitaji maelezo kuhusu uwezo wako wa historia na ulioyaandika na kuyafanya. Tunakufahamu Mohamed Said kupitia vitabu na makala zako zenye madini ya kila aina, na tunatambua uwezo wako mungu aliokujaalia. Mashaallah.

Ramadhan Kareem.
Alexander...
Amin.
 
Kwahiyo hii ni taarifa kabla ya habari au taarifa baada ya habari?

U met Masudi Kipanya in the library, so what? What have u two talked?

Isije kuwa ni ule uzushi wako na uongo uliozoea kuumwaga redio Nur, Iman na zingine za dini yako.

Kwa hapa hutaweza kutusokota nakuambia babu,

Sawa sawa???
Duh.
 
Oto...
Sina kawaida ya kumkejeli mtu wala kujaribu kumfanya ajihisi si lolote si chochote.
Hapakuwa na haja ya hiyo ''kwikwikwi.''

Hakuna radio mashuhuri duniani ambayo haijanitafuta kufanya mahojiano na mimi.

View attachment 1755319
Hapa niko BBC Glasgow, Scotland 1991

View attachment 1755320

Hii ni V o A Washington 2011

View attachment 1755324
Radio Iran, Tehran 2007

View attachment 1755325
Hawa ni TBC 7 April 2021

View attachment 1755326
AZAM TV 2015
🙏🙏🙏 Mohamed Said umenifunza busara.
Hongera mkuu
 
Back
Top Bottom