Zitto, Ludovic Utouh, Kipanya, Rosemary Mwakitwange, Aidan Eyakuze katika Mjadala wa Uwajibikaji na Bajeti ya 2023/24

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Leo Juni 19, 2023, Taasisi ya The Chanzo imeandaa tukio lilipewa jina la #TheChanzoSpecials, ambapo kunatarajiwa kuwa na mijadala mbalimbali itakayowakutanisha Wadau tofautitofauti.

Tukio hili linalenga kujadili masuala matatu muhimu, kwanza tufanye nini ili kujenga tamaduni ya uwajibikaji? Pili uchambuzi wa Bajeti ya 2023/2024 na tatu ni nini kifanyike ili mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri iwe na tija zaidi?

Mijadala yote hiyo inatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa PSSSF COMPLEX HALL

Baadhi ya wanaotarajiwa kushiriki na kuchangia mada mbalimbali ni:
Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT Wazalendo
Ludovic Utouh, Mkurugenzi Mtendaji wa Wajibu na CAG Mstaafu
Rosemary Mwakitwange, Mwandishi nguli na Mwanaharakati
Aidan Eyakuze, Mkurugenzi Mtendaji, Twaweza East Africa
Masoud Kipanya, Mtangazaji wa Clouds FM na mchoraji
Khalifa Said, Mwandishi wa The Chanzo
Richard Kayombo, Mkurugenzi wa Huduma kwa Mlipa Kodi wa TRA



Kipengele cha kwanza: Hali ya Uwajibikaji na namna ya kujenga Jamii inayowajibika
Ikiongozwa na Khalifa Said, hatua hii inahusisha michango ya Zitto Kabwe, Ludovic Utouh na Rosemary Mwakitwange.

Ludovic Utouh
Uwajibikaji upo katika kila sehemu na bila kuwapa elimu au kuwa na ufahamu kuhusu uwajibikaji wananchi au viongozi hawawezi kuwajibika.

Mamlaka ya Serikali yanatokana na Wananchi kutokana na katika yetu lakini Wananchi wengi hawajui hilo na mara nyingi Serikali inachukua hali hiyo kama faida na kutotimiza uwajibikaji.

Wananchi wana haki ya kuifanya Serikali yao itoe maelezo kuhusu mambo ambayo hawayaelewi, mfano ni kama kinachotokea kwenye Uwekezaji wa Bandari, wananchi wanapiga kelele kwa kuwa wanahitaji kufahamu.

Ilani ya uchaguzi ndio Sera ya Chama na ndio msingi wa makubaliano kati ya Serikali iliyopo madarakani na Wananchi kwa kuwa ndio ambayo ilitumika kuwashawishi wao waweze kuiweka madarakani.

Uwajibikaji unawekwa katika nguzo imara za Serikali, Bunge na Mahakama, ukisoma Katiba inaeleza inajitegemea lakini ukweli ni kuwa mhimili wa Serikali unafunika hizi nyingine, kutokana na kutokuwepo kwa usawa hali hiyo inadhohofisha muhimili mingine.

Mwananchi ana haki ya kumuwajibisha yule ambaye amempa madaraka, lakini je, uhalisi ndio huo?

Uwajibikaji unaendana na Utawala Bora, na bila kuwepo kwa Utawala Bora ni ndoto kufikia malengo, hii si kwa mtu binafsi au taasisi pekee, bali hata Serikali.

Hii tabia iliyovuma sana wakati uliopita ya kusema tunamshukuru sana Rais na wakati mwingine kumpiga magoti, haifai, Watanzania tuna tamaduni ya kushukuru lakini kama ni kushukuru tunatakiwa kuishukuru Serikali na si Rais au mtu mmoja-mmoja.

Sasa hivi imeingia hii tabia ya kujikomba, inaturudisha nyuma, tusiweke chumvi, kama ni ukweli tuuseme ukweli.

Wananchi wanayo haki ya kujua Serikali inatekeleza vipi lani ya uchaguzi kwa kuwa nimesema ile ndio kama mkataba uliopo kati ya Wananchi na Serikali.

Wananchi ndio wamiliki wa maliasili zote za Nchi, wana haki ya kuhoji pindi wanapotaka kujua, wao ndio wamewakabidhi viongozi kuongoza kwa niaba yao.

Ndio maana uwepo wa CAG ni sehemu ya mchakato wa uwajibikaji.

Tunatakiwa kujiuliza anachokishauri CAG kinatekelezwa au inakuwa ni ripoti tu kama nyingine ya kawaida?

Kazi kubwa ya Serikali ni kuwaletea Wananchi maendeleo kwa kutumia maliasili zilizopo.

Ukiangalia Ripoti ya CAG ya Mwaka huu, kuna maendeleo mazuri ya kupungua kwa rushwa kati ya Mwaka 2021 na 2022, inawezekana tunapiga hatua katika uwajibikaji

Kuna dhana ya viongozi wanajisahau kuwa maliasili wanazozisimamia ni za kwao binafsi, hata Rais mara kadhaa amesimika akiwaambia wateule wake kuwa wasipandishe mabega baada ya kuteuliwa.

Serikali yetu inapokea ripoti za CAG kwa mwaka mara moja, tunatakiwa kujiuliza kuwa tunaweza kuwa tupo sahihi na tunapata kitu ambacho tunakitarajia?

Madhara ya kukosekana kwa uwajibikaji ni kukosekana kwa kuaminiana kati ya Wananchi na viongozi, kuporomoka kwa maadili, kuongezeka kwa ubinafsi, kupandisha mabega kwa watumishi wa umma, kuongezeka kwa kiwango cha wenye nacho na wsionacjo

Kuwepo utashi wa kweli wa kisiasa kuanzia ngazi ya ju, kuongeza matumizi ya mifumo ya TEHAMA, tuachane na mifumo ya ‘manual’, wananchi kuwa na uwezo wa kudai haki zao na uwajibikaji katika rasilimali za Taifa, uwepo na utaratibu wa Serikali kutoa mrejesho , maafisa masuuli wapate elimu ya utawala, watumishi wa umma watende majukumu yao kwa kuzingatia taratibu.

Ni muhimu Serikali kuhakikisha kuna taarifa sahihi za mapato na matumizi ya fedha za umma.

Viongozi wawe ni mfano wa kutii Sheria na kuwa mfano kwa watumishi wengine.

Dhana ya uwajibikaji wa kweli inahitaji vigezo vitano; Mtoa dhama yaani wananchi, kuwepo na aliyepewa dhamana yaani Serikali, kuwa na kile kilichowekewa dhamana yaani madaraka, mtoa dhamana awe na uwezo wa kumuwajibisha aliyempa dhamana, na mwisho ni matokeo ya kutowajibika.
Fy-Ham3WwAI6-eV.jpg

Ludovic Utouh

Rosemary Mwakitwange
Sikubaliani na dhana kuwa Watanzania wengi hawajui hali yao kuhusu kudai uwajibikaji wa viongozi, leo kuna makundi mengi yanapambana kudai haki yao, hiyo inamaanisha wanajua haki zao.

Katika Nchi ambayo watunga Sheria wetu wawe wanaojua kusoma na kuandika tu kwa nini tunategemea makubwa?

Kwa nini tunawaruhusu Walimu wetu kutengeneza watu ambao asilimia kubwa hawawezi kuajirika?

Viongozi ndio hawajui kuhusu Uwajibikaji, wao ndio wanatakiwa waelimishwe na siyo sisi

Tunapozungumzia Uwajibikaji ni katika hatua ndogo kuanzia familia, labda niwaulize nani ana ule mkataba wa DP World ambao ni halisi? Maana kumekuwa na dhana mbalimbali kuhusu mkataba huo.
Fy-qOMtWIAAu5Of.jpg

Zitto Kabwe
Mwaka 2012 wakati Ludovic Utouh akiwa CAG alipotoa ripoti ilikuwa mbaya, tukamtaka Waziri Mkuu awajibike au mawaziri husika wa Wizara ambao Wizara zao zilikuwa na ripoti mbaya wawajibike.

Kilichotokea Mawaziri waliwajikiba , utamaduni huo ulipotea kuanzia Mwaka 2015, kwa kuwa Bunge halikutimiza majukumu yake vizuri tangu wakati huo.

CAG si Polisi wala TAKUKURU, kuna mambo ambayo akitaona anaweza kupeleka kwenye mamlaka, kazi yake ni kukagua na wajibu wa kufanya ni wa wengine.

Nikizungumzia kuhusu kutowapa watu heshima yao wale wanaofanya vizuri, ukweli ni kuwa hatuna mfumo mzuri wa kupongeza au kuwapa zawadi watu wanaofanya vizuri, taarifa za watu kuangushwa zinabebwa zaidi kuliko za watu ambao wanafanya vibaya.

Ni muhimu kuwapongeza watu wanaofanya vizuri, ndio maana sekta binafsi zinafanya vizuri kwa kuwa zinawapongeza watu wake wanaofanya vizuri.

Ludovic Utouh
Ripoti ya CAG haiwezi kutumika Mahakamani, kwa kuwa CAG hafanyi ukaguzi kwa 100%, anachukua ‘sample’, ndio maana ikitokea kuna mashtaka lazima ufanyike uchunguzi halisi.

Rosemary Mwakitwange
Katiba Mpya ambayo itatumika kupunguza nafasi za kudharauliwa ndio itakuwa suluhisho, unadhani utategemea kuteuliwa kwa kujipendekeza au kukumbukwa mpaka lini, usipokumbukwa ndio basi?

Fy-qOExaMAAuIap.jpg
Hatua ya Pili: Mjadala wa Bajeti ya 2023/24 kuelekea ukamilifu wa Dira ya Mwaka 2025

Masoud Kipanya

Vyombo vya habari vimefanya kazi kubwa sana kwa muda wote huo, kazi ya chombo cha habari ni kukueleza kisha wewe mwananchi ndio unatakiwa kukifanyia kazi

Mimi mwenyewe nafikiria kuacha kuchora katuni, nimeshafikirisha watu wengi sana, inafika kipindi unachoka.

Tunaweza kulaumu vyombo vya habari kwa kuwa Wananchi hawafanyi kile ambacho wanaambiwa na Vyombo vya Habari.
Aidan Eyakuze.jpg

Aidan Eyakuze

Aidan Eyakuze
Tunafanya vizuri katika ukuaji wa uchumi, lakini swali langu ni kuwa matokeo kwa Mtanzania wa kawaida yapoje? Ndio maendeleo?

Umasikini bado ni changamoto ya msingi, Tanzania imekuwa ikikuza uchumi kwa 6% lakini Mtanzania mwenyewe ambaye anaishi katika hali duni hali hiyo haimfurahishi.

Tunakuza uchumi lakini wanufaika ni asilimia ndogo ya wanaonufaiks, wengine ni watanzamaji, 80% hawafurahishwi na ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

Hakuna usawa, hali hiyo ikiendelea ndio inahatarisha amani ndani ya jamii. Hii ni changamoto ambayo ipo na tunatakiwa kuitafutia utatuzi. Sasa huu umoja wtu Watanzania unahatarishwa na hali kama hiyo.

Ubora wa Mtanzania ni tatizo, kawaid siku 1,000 za kwanza za Binadamu ndio msingi wa maisha ya Binadamu, anahitaji kupata lishe bora, maji bora na elimu bora, akikosa msingi mzuri hapo maisha yake yote yanaweza kuyumba au kuharibika na hali hiyo inaweza kuathiri pia hata kizazi chake.

Ukiangalia Bajeti ya 2023/24 inaeleza Matumizi ya Serikali ni 41%, unaweza kujiuliza hii ni Bajeti ya kimkakati au kimbinu? Ni kukuza uchumi tu? Ninavyoona hii ni Bajeti ya Kukuza uchumi.

Lakini nitoe mfano, Equatorial Guinea ina uchumi mzuri lakini asilimia kubwa ya Wananchi wake wana wakati mgumu na wana maisha duni.

Redempta Maira (PWC)
Kati ya vitu tunavyofanya ni kuwapa ushauri wateja kuhusu kodi, hivyo zaidi tunatoa elimu kwa mlipa kodi, sisi ni kama daraja kati ya Mlipa kodi na TRA.

Biashara nyingi si rasmi, kiwango cha VAT kimekuwa kutoka Tsh. Milioni 100 hadi 200, nadhani hiyo itasaidia watu wengi zaidi ambao siku za nyuma walikuwa wakificha sehemu ya mauzo yao ili kukwepa VAT?

Aidan Eyakuze
Kwa nini ukuaji wa uchumi hauendani na ukuaji wa kipato cha watu wengi? Mara nyingi shamba linapokuwa kubwa mwenye shamba anaweza kunufaika zaidi na mazao kuliko wale wafanyakazi ambao ndio wanaofanya kazi kwenye shamba, inabidi tubadilishe ili wanufaika wawe wengi.
Fy-fZmCaEAIcGqC.jpg

Masoud Kipanya
Fy-fZ7xaEAEWu5z.jpg

Richard Kayombo, Mkurugenzi wa Huduma kwa Mlipa Kodi wa TRA
Kwa nini TRA haitengenezi walipa kodi wapya? Miaka kadhaa ya nyuma TIN ilikuwa inauzwa, tulilifanyia kazi hilo.

Kwa watu wengine binafsi wanaweza kuomba TIN kupitia ‘online’, hali hiyo imeondoa usumbufu wa kukaa muda mrefu kama baadhi walivyokuwa walilalamika, pia imepunguza ‘vishoka’ waliokuwa wakisumbua watu.

Mteja akija kwetu anataka kufunga au kusitisha biashara yake cha kwanza tunamuuliza sababu za uamuzi wake huo, tukiona sababu zinahusiana na sisi (TRA) tunamshauri na kuzungumza naye njia bora zaidi za yeye kufanya biashara.

Ikiwa mteja anahama kwa sababu tofauti ambazo zipo nje ya uwezo wake hapo hatuna njia ya ziada.
 
Uwajibikaji hauwezi kuwepo kama wabunge wanafanya kazi za mawaziri bungeni. Badala ya kuisimamia serikali wao wanafanya kazi za serikali. Upitishaji wa mkataba wa bandari ni mfano mzuri, mawaziri hawakupata any challenge juu ya mkataba zaidi walisaidiwa kazi na wabunge.

Hata huko kwenye bajeti ni hayo hayo! Mbunge akikaliwa kooni na wananchi wake ndio wanalia! Mambo ya kitaifa wanageuka kuwa mawaziri badala ya kuwahoji.
 
Party caucus kwenye mazingira ya bunge kuwa na majority members wa chama fulani ni ujinga ambao lazima ufe.

Bora iwekwe kwenye katiba chama kitachokuwa na uwakilishi zaidi ya 60% lazima mijadala ya kitaifa iwe wazi kuepusha influence ya viongozi wa chama na bahati mbaya wakiwa corrupted.

Viongozi wa chama wakitisha wabunge kuwe na utaratibu wa mbunge kutumia mahakama kuwashtaki.

Kama uwakilishi bungeni unakaribiana haina tatizo maana hawatakuwa na mlengo mmoja.

Ni muhimu sana kwa zama hizi tuangalie influence ya chama hasa kwenye mazingira ambayo si maslahi ya Taifa au kukiuka katiba yetu.

Hatuwezi kuwa na dubwana tuliloliachia dhamana ambalo linaelekea kushindwa kujidhibiti na watu kuota sharubu kama hii nchi ni yao peke yao.

Hili la bandari litufunue macho tuweke mifumo ya check and balance kabla siku moja hatujaamka tunaambiwa Mlima Kilimanjaro ni mali ya Kenya na Taifa litaongeza mapato mara 100.
 
Back
Top Bottom