Mimi Masudi Kipanya na safari yetu ya miaka 100

Oto...
Sina kawaida ya kumkejeli mtu wala kujaribu kumfanya ajihisi si lolote si chochote.
Hapakuwa na haja ya hiyo ''kwikwikwi.''

Hakuna radio mashuhuri duniani ambayo haijanitafuta kufanya mahojiano na mimi.

View attachment 1755319
Hapa niko BBC Glasgow, Scotland 1991

View attachment 1755320

Hii ni V o A Washington 2011

View attachment 1755324
Radio Iran, Tehran 2007

View attachment 1755325
Hawa ni TBC 7 April 2021

View attachment 1755326
AZAM TV 2015
Heshima kwako Mzee Mohamed
Haya mapichapicha umemaliza, kabisa
Kweli haihitaji kumdhihaki, bali kumtesa na ukweli wa uhalisia ya maisha yako
Yeye kabanana kwenye kichumba cha kupanga... oooppps!!!! ulimi umetereza......
 
Inawezekana simu aliyotumia kupiga picha ilyopgwa ndo inaonyesha tarehe hyo...
Si mtetei ila mzee katumia busara na hekima kuwapa majibu vijana
Luis...
Hiyo picha ni copy ya picha niliyopiga mwaka 1991 kwa camera za kuweka film.

Hii niliyoweka hapa ni copy kutoka digital camera yenye tarehe na saa.
 
Nakukubali sana mzee wangu vijana tuwahitaji sana watu wa Kariba yako ili kuijenga vema nchi yetu.
Karibu na kwetu kaskazini maana huku wazee wetu wamejitahidi sana kuihifadhi historia yetu na kutupa mwongozo wa kuitengeneza kesho iliyonjema
Dp800,
Nilikuwa Kilimanjaro mwaka jana kwa ajili ya utafiti na nimeandika kitabu kutokana na utafiti huo.
 
Mzee,wewe Ni mtu makini..na msomi mwenye kujitambua..japo natofautiana na wewe mambo flani flani..lakini nakuheshimu Sana..
Ikitokea ukatangulia..watu wengi watasema ukweli huu
Ni wale unaweza waita pia kama wazee wa saigon

Ova
 
Kwahiyo hii ni taarifa kabla ya habari au taarifa baada ya habari?

U met Masudi Kipanya in the library, so what? What have u two talked?

Isije kuwa ni ule uzushi wako na uongo uliozoea kuumwaga redio Nur, Iman na zingine za dini yako.

Kwa hapa hutaweza kutusokota nakuambia babu,

Sawa sawa???
Udini ukizidi hugeuka ujinga ndio kinachotokea kwako.
 
Udini ni ujinga ndio kinachotokea kwako.
Teen...
Hapana hakuna udini katika niandikayo.

Mimi nimesahihisha historia ambayo ilikosa ukweli kwa kuwaacha wazalendo wengi waliopigania uhuru wa Tanganyika.

Hili huenda lilisasababishwa na uoga kuwa wengi waliokuwa mstari wa mbele katika TANU walikuwa Waislam ikaonekana bora historia hii ichakachuliwe.

Kuandika historia ya kweli haiwezi kuwa udini.
 
Teen...
Hapana hakuna udini katika niandikayo.

Mimi nimesahihisha historia ambayo ilikosa ukweli kwa kuwaacha wazalendo wengi waliopigania uhuru wa Tanganyika.

Hili huenda lilisasababishwa na uoga kuwa wengi waliokuwa mstari wa mbele katika TANU walikuwa Waislam ikaonekana bora historia hii ichakachuliwe.

Kuandika historia ya kweli haiwezi kuwa udini.
hapana mzee. Bali nilichoandika kimemlenga huyo niliyemquote sababu yeye ndio ameingiza udini kwenye mada.
 
KUTOKA DHUHR HADI ALASIRI NA MASUDI ''MTU SPECIAL'' KIPANYA

Leo ilikuwa siku makhsusi yaani special sana kwangu kwa kuwa katika chumba kimoja na Masudi Kipanya na vijana wake ''sharp'' wa Clouds Plus.

Hiki kwa hakika si chumba kwa maana ya chumba kama tulivyozoea bali ni Maktaba ya Elite Bookstore Mbezi Samaki.

Masudi Kipanya alinikaribisha ndani ya Maktaba hii nadhifu sana si kwa kuangalia na kusoma vitabu bali kwa ajili ya kufanya kipindi cha televisheni.

Mvua kubwa iliyonyesha kipindi cha adhuhuri kwa kiasi cha saa moja hivi ilitosha kunionya kuwa ile ilikuwa tahadhari kwangu kwa mfano wa ''thunder and lightning,'' (radi na kimulimuli) katika mchezo wa Mcbeth kuwa mchana wangu hautakuwa wa kawaida.

Kwa muda wa saa mbili Masudi Kipanya akitembea katika mengi niliyopata kuandika katika historia ya Tanganyika alinirudisha nyuma miaka 100 hapa hapa Dar es Salaam ya 1920s akitaka kujua maisha ya wazee wangu waliosukuma gurudumu la historia ambayo si wengi wanaifahamu.

Masudi Kipanya kama ni mchezo wa masumbwi nitamwita, ''South Paw,'' kwa jinsi alivyonitaabisha na maswali ya kushtukiza na wakati mwingine kunibana nisema nisiyopenda kusema na wakati mwingine kunitoa kwa haraka katika niliyodhani yangefaa kusemwa.

Muda ulikwenda kwa haraka sana jua likazama nikiwa sina habari na hatujamaliza safari yetu ya miaka 100.

View attachment 1755166
Mzee Said Mohamed wewe ni mwamba hasa wa fasihi
 
Mzee Said Mohamed wewe ni mwamba hasa wa fasihi
Last Emperor,
Prof. Ally Mazrui alialikwa kuzungumza Cornell University New York.

Ilikuwa kuhusu sakata la Salman Rushdie.

Aliyemkaribisha na kumtambulisha alimpamba mno.

Basi Prof. aliposimama kuzungumza akamshukuru yule bwana kwa maneno haya: "Thanks for that generous introduction. "
 
Last Emperor,
Prof. Ally Mazrui alialikwa kuzungumza Cornell University New York.

Ilikuwa kuhusu sakata la Salman Rushdie.

Aliyemkaribisha na kumtambulisha alimpamba mno.

Basi Prof. aliposimama kuzungumza akamshukuru yule bwana kwa maneno haya: "Thanks for that generous introduction. "
Asante Mkuu.. umenikumbusha kuhusu Prof Mazrui, kuna kitabu chake matata sana kinaitwa The Trial of ....(nimesahau). Yule bwana ni genius
 
Back
Top Bottom