Mimba za kuzimu

Mimba za kuzimu

Hapana imani ni jambo la kiroho zaidi kuliko kidunia kwahiyo hata kama mtu yuko subsonscious lakini ufahamu wake uko live
Haya mkuu mshana jr ngoja tu nikubali japo sijaridhika kiviile,hata hivyo shukrani kwa mada zako,ukitulia na kuelewa zina mafundisho makubwa sana,hasa kuhusu ulimwengu usioonekana.shukrani.
 
Haya mkuu mshana jr ngoja tu nikubali japo sijaridhika kiviile,hata hivyo shukrani kwa mada zako,ukitulia na kuelewa zina mafundisho makubwa sana,hasa kuhusu ulimwengu usioonekana.shukrani.
Asante sana nitajitahidi nifafanue zaidi kuhusu hili
 
Ndg mshana jr;
Tahadhari yako nimeifurahia sana, ila unapowaambia watu kuwa wajihadhari na hao wanaojiita manabii sijakuelewa. Ina maana kuwa tusiwakubali tena hao manabii?? Tusipo wakubali manabii tuwaendee wanani?? Sitetei nabii yeyote kwani ninavyo amini mimi ni kwamba, kama kweli huyo ni mtumishi wa Mungu aliye hai, Mungu mwenyewe atamtetea tu. Mungu hatazuiwa na mshana jr au yeyote.
Sisemi kuwa manabii wote ni waongo, ila Neno la Mungu linasema; Kwa matunda yao, mtawatambua. Kwa maneno mengine ni kuwa, tunaweza kuwatofautisha tu kwa matunda yao. Mungu wetu hadhihakiwi, hivyo hawezi kumdhihaki mtu yeyote. Yaani mama amemwomba mtoto, tena kwa uchungu mwingi, miaka 38, halafu Mungu wetu ambaye tunajua jina lake ni UPENDO. amdhihaki, abebe mimba miezi 9 halafu aje kujifungua hizo sura ulizoweka kwenye picha zako. HAPANA. Nasema, haitotokea kamwe.
Kama umemwendea nabii wa kweli, atamwomba Mungu kwa uchungu naye Mungu atakupa mtoto. Ombeni watoto kwa manabii wa kweli. Ishara; Nabii wa kweli hataomba fedha wala zawadi yeyote kwako. Ameambiwa kuwa, ulipewa bure, toa bure. Nimpe pesa kwani yeye ndiye ananipa huyo mtoto??
Mganga, wa kienyeji, hana uwezo wowote wa kukupa mtoto. Akikupa, labda mama ulilala naye na mbegu yake ikarutubisha yai lako. Akikupa mtoto kwa dawa, umempata huyo mshana jr aliyekuambia. Muogope huyo mganga kwani anauwezo na huyo mtoto kwani ni wake sio wako. Akimtaka saa yeyote kama hukutimiza sharti lake anamtwaa. Ni wake maisha yote.
Mh nahisi hamuelewani hapa....zitafika zama ambazo watatokea manabii wa uongo....what did it mean??...hakutotokea nabii wala mtume tena baada ya wale waliopita....sasa hawa waliojaa ndo hao wanaotumia hizo nguvu za hao kwenye picha za mshana jr....kazi kwako....mshana jr big up....dini isome kwa undani wake usifuate kwa ushabiki....itafute elimu ya dini kwa nguvu zote..popote pale...kazi kwako..
 
Wale wanao Mpinga Mshana wengi ni haohao washirikina wanaona jamaa anawaumbua,kiukweli haya mambo yapo kama huamini we kaa kimya ila tunaishi katika ulimwengu complex kabisa I nahitaji hekima na busara ya ya hali ya juu kuyatambua haya,mungu atufungulie tuyafaham kwa kina,thanx mpwa Mshana,jichawi.
 
Jihadhari za mimba na mimba za kutafuta kwa manabii na waganga wa kienyeji.

Jaribu kufuatilia hizo mimba mpaka mwisho wake au kama watoto walizaliwa salama na kama wako hai mpaka leo hii na kama tabia zao ni za kawaida
Nimeshuhudia mara nyingi matangazo kwenye tv magazeti na radii hao wanaojiita manabii mitume na waganga wakijinasibu kuwa wamewasaidia akina mama wengi kupata ujauzito na hatimaye kujifungua watoto.

Lakini kamwe hatujawahi kuletewa mrejesho wa wale watoto maendeleo yao....kiukweli ni kwamba wengi walikufa au kupotea katika mazingira ya ajabu mno..hawa si watoto halisi.

Kujiepusha na maumivu haya nendeni hospital kapimeni wote ijulikane tatizo liko wapi au tatizo ni la nani halafu tiba yake ninini! Kama hakuna shida kila kitu kiko sawa lakini mimba hazishiki mwombeni Mungu atawajaalia mtoto wa haki...!

Msijaribu kwingineko haitawalipa.
Mkuu Ulishawahi kufuatilia ukathibitsha.. Au ndo assumption at work..
 
Jihadhari za mimba na mimba za kutafuta kwa manabii na waganga wa kienyeji.

Jaribu kufuatilia hizo mimba mpaka mwisho wake au kama watoto walizaliwa salama na kama wako hai mpaka leo hii na kama tabia zao ni za kawaida
Nimeshuhudia mara nyingi matangazo kwenye tv magazeti na radii hao wanaojiita manabii mitume na waganga wakijinasibu kuwa wamewasaidia akina mama wengi kupata ujauzito na hatimaye kujifungua watoto.

Lakini kamwe hatujawahi kuletewa mrejesho wa wale watoto maendeleo yao....kiukweli ni kwamba wengi walikufa au kupotea katika mazingira ya ajabu mno..hawa si watoto halisi.

Kujiepusha na maumivu haya nendeni hospital kapimeni wote ijulikane tatizo liko wapi au tatizo ni la nani halafu tiba yake ninini! Kama hakuna shida kila kitu kiko sawa lakini mimba hazishiki mwombeni Mungu atawajaalia mtoto wa haki...!

Msijaribu kwingineko haitawalipa.
Mshana Jr!

Somo zuri lakini umeliandika kifupi mnoo, wewe unajua kuwa Wapo waliozaliwa kwa miujiza na wapo waliozaliwa kimazingara! Naomba tupe somo refu kidogo.

Submitted for your guidance and record.
 
Dah! Ila mshana jr sipati picha ulivyojichanachana chale, hivi nyumban kwako unasali? Au kwamfano kikatokea kitu chochote ktk mazingira ya kutatanisha hapo si unashinda unatwanga mitishamba?

Unajua nmekumbuka kipind nasoma kuna chumba nilikuwa nakaa sasa alikuja jamaa yangu mmoja kuomba hifadhi kwakuwa nyumban kwao walikuwa na migogoro yule jamaa alikuwa mshirikina hatari, yaan akiona hata mbwa kakatisha tu tayar anaanza kujipaka midawa yake, siku moja nipo kitandan napiga msuli bed nikashangaa nmemwagiwa maji hata mtu aliyenimwagia simuon na hakukuwa na mtu yeyote ndan halafu nikasikia sauti ikijisonya kutoka darini. Ikabidi nimwambie baba alimfukuza yule jamaa.
Daaah mkuu umenivunja mbavu aisee
 
Naam majini wanatofautiana uwezo, ujabali na nguvu.....anaweza kuwa jinn aina fulani eneo fulani na majini wengine hata wawe mia wasiweze kugusa hilo eneo.
Kufuga sipendi kuelezea kwa kuwa si vema sana ila kukufungulia kidogo, mimi binafsi naweza sikia au kuona kuwa eneo fulani lina jini hatari tangu enzi kiasi cha kuvuma kwa vitimbi vya wazi eneo hilo.....naandaa vitu fulani ambavyo ni vyakula kwake na mwili unakuwa safi kisha nafika hilo eneo.
Patakuwa na vishindo maana atakuwa ananiona tangu mbali ila hakuna shida, nikifika nasema kwa sauti na kumuomba tushirikiane awe katika milki yangu pamoja na kuweka vitu vile, pindi nikiondoa hatua kurudi basi ujue narudi nae nyumbani na pia kuwe tayari kimazingira katika nyumba hiyo yeye kukaa haswa kama tayari kuna majini wengine tofauti na yeye.
Vyakula wanakula vitu tofauti ila damu ndio chakula kikuu.....mpaka amekuja ni kwamba mmeshaagana kuwa awe anafanya kazi ipi na vyakula utakuwa unampa kila mda gani.
Yupo rafiki yangu fulani alifanya maagano na jinn mmoja ili amletee wateja katika miradi yake mikubwa mikubwa, alifanikiwa kweli kweli mpaka watu wakawa na shaka nae ila mwisho wa siku hakuwa akipeleka chochote kwa bwana mkubwa.
Alianza kuzika watoto mpaka wajukuu na sasa yule jinn ameshageuka hasikilizi lolote!
Onyo; usijaribu! Mungu anatoa yote.

Hapa ndipo tunapokoseaga binadam hauwezi kupewa tu bila kutoa chochote
 
Mada namna hii ni nzuri maana naishi ndani ya yanazungumzwa na nayajua......binafsi kuna dada mmoja wa miaka kama 37 hivi ambae hakuwahi kushika mimba tangu kuvunja ungo kwake.
Alinifuata kuhitaji msaada wangu maana ameshapoteza matumaini na tiba za kizungu hazionyeshi manufaa kwake, nikafanya nnachokijua akashika mimba na kujifungua (japo alijifungua kwa tabu mpaka nikatuma nguvu za ziada)
Jana amenitembelea akiwa na furaha kuu na yeye kuwa na mtoto na alikuwa mtoto ameshafikisha siku arobaini.
Narudi kwenye mada.....nayajua maagano yake na roho zinazomuandama yule mtoto na mama......najua anahitaji ukaribu na mimi ili mambo yaendelee kuwa sawa......najua pindi mambo akiyaacha njiani kwa kunidharau kisa katimiza lengo lake nini kitampata......nk nk
Ikitokea mola akakuchukua itakuwaje? (Sikuombei kifo ila hutokea mara nyingi waganga kufa na kuwaacha njiani wateja wao)
 
Huku kwetu kuna mabosi wanaomiliki mabasi ya safari za mikoani na ni marafiki zangu......si mara moja wala mara mbili pale wanapopokea simu kuwa mabasi yao yamepinduka na kuua watu wengi.....hawaonyeshi mshtuko ila wanakuwa na furaha! Na baada ya mda mtu anaongeza mabasi mapya hii inakuwaje? Ni kafara?

Na pia nina mtoto wa dada yangu anaishi Dar na alikuwa ni tax drive, ghafla amekuwa na pesa ana nyumba si chini ya nne hapo Dar achilia mbali za chalinze, pia anamiliki gari tofauti za kutembelea na ameoa mwarabu kwa pesa ndefu (sishangai kupata maana pengine ni jitihada zake)

Kinachoshangaza ni kuwa pale kwake analala chini hatumii kitanda tofauti na awali, mke wake analalamika kwa ndg kuwa mume hampi mapenzi japo akiaga safari anaruhusiwa na kupewa gari na pesa za kutosha.
Kuna wakati jamaa alisafiri kwenda Tanga na mke huku nyuma alinunua kitanda na kufunga, jamaa aliporudi alilia sana kwa uchungu na kusema unataka kuniua! Ugomvi haukuamulika na jamaa kampa mke talaka moja.
Je, jamaa ni free mason?
Ukiona masharti ya hivyo jua ni uchawi
 
Ni kwa vile tuko busy na dunia na tunaendeshwa na mihemko na matukio ya papo kwa papo huku tukiaminishwa kuwa huo ndio uhalisia
Hatuna muda wa kutafakari kwakuwa kila wakati Tunahitaji kupata tukio jipya ...tungekuwa tunafuatilia mpaka mwisho haya matukio hakika tungefunuliwa mengi mno...watu hushangilia mtu kupata mimba au mtoto lakini yanayofuta baada ya hapo ni siri yake na hata kuna wakati hutishwa asiseme chochote
Kuna watu wamebeba mimba hizi za kuombewa na kufanyiwa dawa zaidi ya mwaka mmoja na wanapokuja kujifungua huzaa kitu cha ajabu au mtoto mfu huku vipimo vyote vya hospital vikionyesha hakuna shida yoyote
Mkuu.. naomba muwe mnawaambia madhara ya hizo kabla ya kuzitoa
 
Bado Mungu ndie mweza wa yote...wapo waganga wachache mno watakaoweza kukufungua bila side effects
Sidhani kama mganga wanaweza kumfungua aliyefungwa na nguvu za Giza zaidi ya maombi rasmi kwa Mungu.

Kwani kwenda kwa mganga wa kienyeji ili kufunguliwa vifungo ni ngumu kwa kuwa mganga na mchawi wote ni wa ufalme mmoja.

Akijitahidi sana atakuwekea jini kubwa kuliko ulilopewa na mchawi.hivyo anaongeza matatizo.

Kwa Yesu tu ndio jibu.
 
Sidhani kama mganga wanaweza kumfungua aliyefungwa na nguvu za Giza zaidi ya maombi rasmi kwa Mungu.

Kwani kwenda kwa mganga wa kienyeji ili kufunguliwa vifungo ni ngumu kwa kuwa mganga na mchawi wote ni wa ufalme mmoja.

Akijitahidi sana atakuwekea jini kubwa kuliko ulilopewa na mchawi.hivyo anaongeza matatizo.

Kwa Yesu tu ndio jibu.
Mganga anaweza kama akiamua kutumia tiba za asili za mitishamba bila kuhusisha tunguli viapo na damu
 
wanaotaka mimba




kuliko kwenda kwa mganga, chukua asali vijiko viwili changanya na mdalasini wa kutosha, hadi mchanganyiko uo uwe kama big g, usiku wakati wa kulala paka katika fizi za juu na chini lala na mchanganyiko huo, au fanya mapenzi ukiwa na mchanganyiko huo na kama uko ktk siku zako za kushika mimba, au tumia mchanganyiko huo, baada ya siku tatu shiriki tendo ndani ya siku za mimba, InshaAllah naamini utapata mimba, Tiba hii nimewasaidia watu saba na wote sasa wanawatoto, ni ushauri tu niliwapa,
 
Back
Top Bottom