ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 13,386
- 30,687
Kuna wanaume Mungu kawajalia familia nzuri sana mke mwema, anayejitunza, anayeheshimu ndoa yake, anayekutii na kusimama kwenye nafasi yake kama mke.
Pengine amekuzalia watoto na amekuwa nawe kipindi kigumu na chepesi.
Lakini kutokana na tamaa, unaanza kuchezea amani ya familia yako mwenyewe.
Unaingia kwenye umalaya wa wazi wazi bila hata kujificha, ukiwa na ego kubwa kwamba hakuna atakayekufanya chochote
Sasa hapo mwanamke kakufanyia nini mpaka umtendee hivyo?
Tatizo kubwa si tu kucheat
Tatizo ni dharau, maudhi na mabadiliko ya tabia baada ya kupata (nyama mpya)huko nje
Na unataka mke aendee kukuheshimu kama zamani wakati wewe mwenyewe umebadilika
Heshima haiji yenyewe, heshima inatengenezwa
Kama zamani ulikuwa unaheshimiwa, basi jiulize: nini kimebadilika?
Kwa nini leo unaonekana wa kawaida tu machoni mwa mke wako?
Huenda ni tabia zako mpya dharau, ukali, kiburi na kutothamini familia
Lakini pia nisieleweke vibaya sizungumzii wanawake wenye tabia mbaya, wenye matusi, visirani na gubu kupitiliza Hapana
. Nazungumzia mwanamke mwema ambaye anajitahidi kuijenga familia lakini bado anatendewa vibaya.
Wanasema mshahara wa dhambi ni mauti.
Na kuna kisa nilikishuhudia karibu kabisa kwenye familia
Kuna dada mmoja alikuwa na maisha ya kudanga sana Akapata mimba ya kwanza, mwanaume akamkimbia na kumuachia mtoto
Hakutulia, akapata mimba ya pili, akaolewa haraka haraka kuficha aibu ya ujauzito, lakini ndoa nayo haikudumu akaachika akiwa na mtoto mwingine
.
Bado hakutulia.
Akabeba mimba ya tatu. Siku moja akaja kwangu baada ya swala ya Magharibi. Akanambia:
Mdogo wangu, nimejifunga
Lakini hakuwa na furaha hata kidogo. Nilipomuuliza kulikoni, akasema hajui mimba ni ya nani kwa sababu alikuwa ametembea na wanaume wawili kwa nyakati zinazokaribiana
Tulivyohesabu tarehe, ikaonekana wazi mimba ni ya kijana mmoja wa kawaida anayejitafuta. Lakini yeye alitaka mimba ihesabike kwa mwanaume mwingine mume wa mtu mwenye pesa
Bahati mbaya kwake, yule mwanaume mwenye pesa alikataa na hata akatoa pesa mimba itolewe
Mimba haikutolewa
Mwisho wa siku yule kijana wa kawaida akaambiwa ndiyo mwenye ujauzito na akakubali
Lakini baadaye wakaja kuachana.
Cha kushangaza zaidi, mimba ile ile ikapewa mwanaume mwingine 🙌
ambaye hata hakuhusika kabisa kwenye huo mchezo
Na kwa sababu ya upendo au ujinga, akaikubali mpaka akaanza kuhangaika na majukumu ya mtoto ambaye si wake
Leo hii huyo mwanaume amemuoa kabisa last kama mke wa pili
Nilipomuangalia siku ya harusi nilihuzunika sana
Nikajiuliza
Kama huyu mwanaume angeweza kutuliza tamaa zake na kuwa makini, angejikuta kwenye hali hii kweli?
Kwa sababu wakati mwingine tamaa na uzembe vinaweza kukufanya ubebe majukumu ambayo si yako, huku ukiwaumiza watoto au familia yako halisi
Swali langu kwa wanaume ni hili:
Una uhakika huyo mtoto unayemhudumia ni wako?
Pima hata DNA 🤪
Na kabla hamjaharibu familia zenu kwa tamaa za nje, kumbukeni kuwa amani ya nyumba hujengwa kwa uaminifu, heshima na kujitambua si kwa starehe za muda mfupi
ShesRise_1 👋