Mimi naamini wapo manabii wa kweli wanaotumika na roho mtakatifu ambao mungu amewapa uwezo wa kutambua mambo yaliofanyika zamani katika maisha yako na hata yale yajayo. hapa kwetu tuna padri anaitwa Fr. Shija wa kanisa katoliki kwa sasa ameamia malangali watu kibao huku mafinga wanaenda anawabashiria mambo yao pia wanapata uponyaji.. yaani mtu ukienda kwake kabla hata ujamwambia anakwambia kila kitu kinachofanyika na hata kile kitakachokutokea. kuna rafiki yangu alienda alikuwa anahitaji mtoto wa pili ila mimba ikawa inagoma kuingia fr. alimwambia kila kitu kilichosababisha asishike ujauzito mwingine kwa alipata mimba ya pili wakati mtoto yule wa kwanza akiwa na miezi sita tu akaona mhhh aitoe kumbe ile damu ya yule mtoto ilikuwa ikidai kisasi.
So fr.akamwambia inabidi wamfanyie misa yamazishi ya ile mimba aliyokuwa ameitoa pia aombe toba na rehema kwa mungu. baada ya wiki akamwambia unaenda kushika mimba ya mtoto wa kike. na kweli akapata mimba mimba na kuzaa mtoto wa kike .mtoto yule ana akili na nimchangamfu kuliko hata yule wa kwanza hivi naongea yupo darasa la saba.
Hapa Mafinga tumebahatika pia, kwani tuna nabii anaitwa Prophet Sareh wa madhabahu ya moto watu tumebashiriwa mambo yetu yanakuwa vilevile kama alivyo bashiri .watu kibao wanapata wenza, wanapona kisukari, presha ,HIV,watoto , just to mention a few
Mungu wetu yupo na anafanya kazi na watu wake, japokuwa katika msafara wa mamba na kenge wapo.No way , kabla hujaenda kutafuta kuombewa kwa jambo fulani mshirikishe roho mtakatifu akuongoze katika njia sahihi.
SAMAHANI KWA KUANDIKA KWA KIREFU. .......SHALOM......