Mimba za kuzimu

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,676
729,839
Jihadhari za mimba na mimba za kutafuta kwa manabii na waganga wa kienyeji.

Jaribu kufuatilia hizo mimba mpaka mwisho wake au kama watoto walizaliwa salama na kama wako hai mpaka leo hii na kama tabia zao ni za kawaida
Nimeshuhudia mara nyingi matangazo kwenye tv magazeti na radii hao wanaojiita manabii mitume na waganga wakijinasibu kuwa wamewasaidia akina mama wengi kupata ujauzito na hatimaye kujifungua watoto.

Lakini kamwe hatujawahi kuletewa mrejesho wa wale watoto maendeleo yao....kiukweli ni kwamba wengi walikufa au kupotea katika mazingira ya ajabu mno..hawa si watoto halisi.

Kujiepusha na maumivu haya nendeni hospital kapimeni wote ijulikane tatizo liko wapi au tatizo ni la nani halafu tiba yake ninini! Kama hakuna shida kila kitu kiko sawa lakini mimba hazishiki mwombeni Mungu atawajaalia mtoto wa haki...!

Msijaribu kwingineko haitawalipa.
 
Hakika mshana barabarani tuna Mashetani wengi sana waliozaliwa na binadamu.

Pia ni bora kuwapeleka watoto hao kwa viongozi wa kidini walio na nguvu za Mungu JEHOVA
1455327537785.jpg
1455327546459.jpg
1455327567019.jpg
 
Dah! Ila mshana jr sipati picha ulivyojichanachana chale, hivi nyumban kwako unasali? Au kwamfano kikatokea kitu chochote ktk mazingira ya kutatanisha hapo si unashinda unatwanga mitishamba?

Unajua nmekumbuka kipind nasoma kuna chumba nilikuwa nakaa sasa alikuja jamaa yangu mmoja kuomba hifadhi kwakuwa nyumban kwao walikuwa na migogoro yule jamaa alikuwa mshirikina hatari, yaan akiona hata mbwa kakatisha tu tayar anaanza kujipaka midawa yake, siku moja nipo kitandan napiga msuli bed nikashangaa nmemwagiwa maji hata mtu aliyenimwagia simuon na hakukuwa na mtu yeyote ndan halafu nikasikia sauti ikijisonya kutoka darini. Ikabidi nimwambie baba alimfukuza yule jamaa.
 
Mada namna hii ni nzuri maana naishi ndani ya yanazungumzwa na nayajua......binafsi kuna dada mmoja wa miaka kama 37 hivi ambae hakuwahi kushika mimba tangu kuvunja ungo kwake.
Alinifuata kuhitaji msaada wangu maana ameshapoteza matumaini na tiba za kizungu hazionyeshi manufaa kwake, nikafanya nnachokijua akashika mimba na kujifungua (japo alijifungua kwa tabu mpaka nikatuma nguvu za ziada)
Jana amenitembelea akiwa na furaha kuu na yeye kuwa na mtoto na alikuwa mtoto ameshafikisha siku arobaini.
Narudi kwenye mada.....nayajua maagano yake na roho zinazomuandama yule mtoto na mama......najua anahitaji ukaribu na mimi ili mambo yaendelee kuwa sawa......najua pindi mambo akiyaacha njiani kwa kunidharau kisa katimiza lengo lake nini kitampata......nk nk
Nimekumbuka tu haya maandiko "Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake na moyoni mwake amemwacha Mungu"

Ulivyoongea hapo juu tu nimewaza eti mtu na mtoto wako maisha yenu yote yupo binadamu anayeyacontrol. Siku mkimuudhi au amefariki bahati mbaya au yeye tu akiamua ndivyo sivyo basi ndo kila kitu kushney

Mmh Mungu tunaomba ubariki matumbo yetu. Kukosa mtoto sio kitu kirahisi jamani, hata ukiambiwa ufanye kitu gani sijui, for the sake of a child mbona utajikuta unafanya tu. What matters ni wewe kuitwa mama. Mungu atusaidie jamani
 
Heri ya yule anaekufungua masikio kuliko anaenyamaza......
Lengo ni kukumbushana kesho yetu...akhsante kwa maandiko
Ni kweli mkuu maana anaesema anataka watu waache......vipi kuhusu pesa mtu anaweza pata kiasi cha kutajirika kwa njia hizo?
 
Jihadhari za mimba na mimba za kutafuta kwa manabii na waganga wa kienyeji.

Jaribu kufuatilia hizo mimba mpaka mwisho wake au kama watoto walizaliwa salama na kama wako hai mpaka leo hii na kama tabia zao ni za kawaida
Nimeshuhudia mara nyingi matangazo kwenye tv magazeti na radii hao wanaojiita manabii mitume na waganga wakijinasibu kuwa wamewasaidia akina mama wengi kupata ujauzito na hatimaye kujifungua watoto.

Lakini kamwe hatujawahi kuletewa mrejesho wa wale watoto maendeleo yao....kiukweli ni kwamba wengi walikufa au kupotea katika mazingira ya ajabu mno..hawa si watoto halisi.

Kujiepusha na maumivu haya nendeni hospital kapimeni wote ijulikane tatizo liko wapi au tatizo ni la nani halafu tiba yake ninini! Kama hakuna shida kila kitu kiko sawa lakini mimba hazishiki mwombeni Mungu atawajaalia mtoto wa haki...!

Msijaribu kwingineko haitawalipa.
Kama unasema kwa manabii sasa huyo Mungu tunamuombea wapi??
 
Naam ila kafara lazima ziwepo pamoja na masharti....
Huku kwetu kuna mabosi wanaomiliki mabasi ya safari za mikoani na ni marafiki zangu......si mara moja wala mara mbili pale wanapopokea simu kuwa mabasi yao yamepinduka na kuua watu wengi.....hawaonyeshi mshtuko ila wanakuwa na furaha! Na baada ya mda mtu anaongeza mabasi mapya hii inakuwaje? Ni kafara?

Na pia nina mtoto wa dada yangu anaishi Dar na alikuwa ni tax drive, ghafla amekuwa na pesa ana nyumba si chini ya nne hapo Dar achilia mbali za chalinze, pia anamiliki gari tofauti za kutembelea na ameoa mwarabu kwa pesa ndefu (sishangai kupata maana pengine ni jitihada zake)

Kinachoshangaza ni kuwa pale kwake analala chini hatumii kitanda tofauti na awali, mke wake analalamika kwa ndg kuwa mume hampi mapenzi japo akiaga safari anaruhusiwa na kupewa gari na pesa za kutosha.
Kuna wakati jamaa alisafiri kwenda Tanga na mke huku nyuma alinunua kitanda na kufunga, jamaa aliporudi alilia sana kwa uchungu na kusema unataka kuniua! Ugomvi haukuamulika na jamaa kampa mke talaka moja.
Je, jamaa ni free mason?
 
Kuhusu hao mabosi wa mabasi unaowasema siwezi kuwahukumu moja kwa moja, ila wapo wanaotumia uchawi/majini kufanikiwa na watu wanapokufa wao hufurahi kwani milango itazidi kufunguka kwani wakuu wameshapata damu.
Kuhusu huyo ndugu yako sio Freemason bali ni maagano ya kiganga na mizimu.
Ni vema ukajikita kwenye mada
Akhsante mkuu
 
Back
Top Bottom