Mikopo Elimu ya Juu: Hatimaye Value Retention Fee 6% yaondolewa

Mikopo Elimu ya Juu: Hatimaye Value Retention Fee 6% yaondolewa

Sasa washushe ulipaji hadi 8%
 
Mwenye uelelwa na hii anifafanulie tafadhari. Atabarikiwa sana kwa msaada wake huo
Tumia mfano huu utaelewa
a. Una deni la 10,000,000
b. Ukalipa 250,000 kwa miezi 12 yaan 3,000,000 kwa mwaka chukulia ndio makato toka mshahara wako
c.mwisho wa mwaka mkopo uliobaki Ni 10-3=7m.
Tunaingia kwenye retantion charges
6% Mara 7000,000=420,000
Deni jipya 7m +420,000 ambayo ni 7420,000
Kwa picha hiyo kama mshahara Ni chini ya 2.5m Hilo deni humalizi kwani linakua kila kipindi
 
Serikali haija shauriwa vizuri kwenye hili.

1. Retention fee inaongeza muda wa kulipa.
2. 15% inakaza ukali wa maisha.

Hii maana yale kwenye makato hakuna unafuu, bali muda wa kulipa deni ndio utapungua.

Ni heri wangeacha 6% lakini wapunguze loan fee kutoka 15 to 9% au even lower.

Kwangu mimi sioni unafuu hapo..
Hapa umepuyanga, bora kukamuliwa kwa muda mfupi. Hiyo 6% ilikuwa wizi tu. Au umetumwa na bodi?!
 
Sasa mimi nauliza, hiyo asilimia 6 iliyokatwa itajumuishwa katika deni au ndo ishaliwa tunaanza hapa kuhesabu?
Mkuki kwa nguruwe, kama walipandisha makato kutoka 8%-15%, wakawahusisha wale wenye mikataba kabla ya hapo basi tutahitaji uzalendo wao kuondoa mahesabu ya value retention kwenye madeni halisi ya watu ya sasa.
 
Ndio maana wafanyakazi wa nchi hii wana lundo la madeni.

Yaani mtu anaona ni bora akatwe pesa kidogo kwenye mshahara wake ( ili abakiwe na pesa kubwa ) lakini adumu na deni kwa kulilipa hata miaka 40.

Akimaliza, anapiga mahesabu anaona amelipa jumla ya oesa kubwaaa anaanza kulialia kama zezeta na kuwaumu mkopeshaji, kumbe yeye mwenyewe ndio ZWAZWA.

Lipa deni kwa kukatwa pesa kubwa kwa muda mfupi ili liishe mapema uwe huru ingawa utaishi kwa shida ila ni muda mfupi.

Wafanyakazi wengi nchi hii hamna Akili.
Mkuu ni huyo zwazwa peke ake!
 
Wajitahidi na ajira zipatikane, kupunguza kodi wakati hakuna ajira na huku unaendelea kukopesha wengine ni maigizo tu.
Serikali haina uwezo wa kumuajiri kila mtanzania, toka nje ya box, jiajiri.
 
Tumia mfano huu utaelewa
a. Una deni la 10,000,000
b. Ukalipa 250,000 kwa miezi 12 yaan 3,000,000 kwa mwaka chukulia ndio makato toka mshahara wako
c.mwisho wa mwaka mkopo uliobaki Ni 10-3=7m.
Tunaingia kwenye retantion charges
6% Mara 7000,000=420,000
Deni jipya 7m +420,000 ambayo ni 7420,000
Kwa picha hiyo kama mshahara Ni chini ya 2.5m Hilo deni humalizi kwani linakua kila kipindi
Shukran mkuu, umenifungua akili
 
Mwenye uelelwa na hii anifafanulie tafadhari. Atabarikiwa sana kwa msaada wake huo
Yaani Kama ulikopeshwa let say 10million. Ukisha ajiriwa unalipa 15% ya mshahara wako kila mwezi ili kulipia deni walilokukopesha.
Kwa mishahara yetu hii hauwezi ukalipa deni ndani ya mwaka mmoja. Sasa tuchukulie kwa mwaka ukawa umelipa jumla ya sh. 2million.
Ukichukua hela waliokukopesha ukatoa na hela uliyowapa unapata 10mil-2mil=8mil
Kwa hiyo hapo Deni lako limebakia sh million 8.
Sasa hawa jamaa ni kwamba hilo deni lililobakia linazaa riba ya 6% ambayo itakuwa Kama ifuatavyo.
6%*8000000=480000
Kwa hiyo mwaka unaofuata jumla ya deni lako linakuwa 8000000+480000=8480000.
Jumla inakuwa sh. 8480000.
Sasa ni kuwa mama Samia amesema kuwa hiyo 6% inayojizaa kila mwaka ameifuta. Kwa maana kuwa mtu alipe deni alilokopa tu. Sorry kwa uandishi wangu mbovu.
 
Tunataka kuona haya mabadiliko kwenye Salary Slip kuanzia mwezi huu.

Kumbafu sana HESLB
 
Ndio maana wafanyakazi wa nchi hii wana lundo la madeni.

Yaani mtu anaona ni bora akatwe pesa kidogo kwenye mshahara wake ( ili abakiwe na pesa kubwa ) lakini adumu na deni kwa kulilipa hata miaka 40.

Akimaliza, anapiga mahesabu anaona amelipa jumla ya oesa kubwaaa anaanza kulialia kama zezeta na kuwaumu mkopeshaji, kumbe yeye mwenyewe ndio ZWAZWA.

Lipa deni kwa kukatwa pesa kubwa kwa muda mfupi ili liishe mapema uwe huru ingawa utaishi kwa shida ila ni muda mfupi.

Wafanyakazi wengi nchi hii hamna Akili.
Ni kweli wangetukata hata 20% ambapo deni unamaliza mapema.Mimi iyo asilimia 15 ibaki maana nimebakiza 3.8 mil,deni likikaa muda mrefu linaathiri Mikopo ya Benki maana Makato yanaongezeka kadri ya nyongeza ya mshahara.
 
Tumia mfano huu utaelewa
a. Una deni la 10,000,000
b. Ukalipa 250,000 kwa miezi 12 yaan 3,000,000 kwa mwaka chukulia ndio makato toka mshahara wako
c.mwisho wa mwaka mkopo uliobaki Ni 10-3=7m.
Tunaingia kwenye retantion charges
6% Mara 7000,000=420,000
Deni jipya 7m +420,000 ambayo ni 7420,000
Kwa picha hiyo kama mshahara Ni chini ya 2.5m Hilo deni humalizi kwani linakua kila kipindi
Lengo lakuiweka 6% lilikuwa lipi kwa uelewa wako tu.
 
Back
Top Bottom