Mikopo Elimu ya Juu: Hatimaye Value Retention Fee 6% yaondolewa

Wenyewe wanaita tozo ya kutunza thamani ya fedha
Hata kwenye mabenki sijawai ona hii kitu.Bodi ilijigeuza na kuwa kama tahasisi ya kifedha ya kukopesha.Kilichobaki ilikuwa ni leseni tu.Wakati hata kwenye matasisi ya kifedha mikopo chefuchefu ugeuka kuwa bad debt na mwisho write off,wao waliongeza matozo kuonyesha kuwa mikopo hiyo inalipika.Mama tunashukuru kweli wewe ni Mama.Mtu hana ajira bado unamdai kwani hiyo mikopo mlikoesha wajasiriama au wafanyabiashara. Kilichogeuka kilikuwa mwiba mchungu kwa wafanyakazi.Mama ni Mama tu piga kazi tupo nyuma yako.
 
Retention haikokotolewi kwenye salio la deni bali kwenye kiwango cha kwanza kukopa yaani hapo ungechukua asilimia sita ya milioni kumi ndio uongeze kwenye salio la deni baada ya makato,,ko hiyo riba sio reducing balance
Kwaio kama ulikua unadaiwa 11,900,000 ina maana 11,900,000 x 0.06 = 714,000 = 12,614,000 mfano kwa mwaka unalipa 4,500,000 unapunguza ipi kati ya hizo figure mbili 11,900,000 au 12, 614,000 mkuu?
 
Kwaio kama ulikua unadaiwa 11,900,000 ina maana 11,900,000 x 0.06 = 714,000 = 12,614,000 mfano kwa mwaka unalipa 4,500,000 unapunguza ipi kati ya hizo figure mbili 11,900,000 au 12, 614,000 mkuu?
Haya mahesabu yako sijui umefanyaje.

Kama unadaiwa 11,900,000 na umelipa mwaka mzima 4,500,000 maana yake ndani ya mwaka deni lako litakuwa limebaki 7,400,000.

Sasa kama VRF ingekuwepo, mwishoni mwa mwaka huo kwenye hilo deni lililobaki, wangeongezea tena 6% ya 7,400,000 juu ya deni.

Hiyo 6% ndio inaondolewa maana yake badala yake deni litabaki hiyo hiyo 7,400,000
 
Haya mahesabu yako sijui umefanyaje.

Kama unadaiwa 11,900,000 na umelipa mwaka mzima 4,500,000 maana yake ndani ya mwaka deni lako litakuwa limebaki 7,400,000.

Sasa kama VRF ingekuwepo, mwishoni mwa mwaka huo kwenye hilo deni lililobaki, wangeongezea tena 6% ya 7,400,000 juu ya deni.

Hiyo 6% ndio inaondolewa maana yake badala yake deni litabaki hiyo hiyo 7,400,000
Huyo mdau hapo juu amesema kwamba VRF inakokotolewa kwenye deni halisi i.e original deni sio deni lililobaki baada ya kulipwa mkopo
 
Huyo mdau hapo juu amesema kwamba VRF inakokotolewa kwenye deni halisi i.e original deni sio deni lililobaki baada ya kulipwa mkopo
Yes, ni sawa kwahiyo baada ya malipo hakutakuwa na ongezeko hilo la 6% ya deni halisi juu ya deni lako lililobaki.
 
Kwa mahesabu ya nje ni kweli yanatakiwa yapungue, ila ukienda bodi wao wana vijikanuni vyao vya ajabu wanavyovijua wao tu dunia nzima, watakuvuruga na hesabu uone unadaiwa kihalali kabisa tena wakuaminishe hapo ndio wamekupa na kapunguzo kidogo... jamaa nuksi sana wale..
Ila ngoja tuone baada ya tamko, tujipe muda wa ushuhuda
Kikubwa ulitakiwa ujue deni lako halisi baada ya juhitimu lilikuwa kiasi gani, mimi wakati nahitimu 2011 tulipewa vijitabu vinavyoonesha kila ulichopewa na HESLB, kuanzia hapo ujue umelipa kiasi gani toka ulipo anza kukatwa ili unapenda bodi uwe na evidence za kutosha
 
Wengi ilitukuta hiyo Yukawa na take home ya laki 1.6 hadi laki 2
Hata hamu ya kazi ilipotea
Mkuu hata mimi miaka kadhaa nyuma nilikuwa nawaza kama wewe, nikawa naona naonewa kweli...

HII VALUE RETENTION FEE NDIO ILIKUWA KABURI (ni bora kukatwa pesa kubwa kwa muda mfupi zaidi huku unalipa deni lile lile ulilopewa kuliko kukatwa pesa ndogo kwa muda mrefu huku deni likiongezeka zaidi na zaidi) nikopeshe milioni 10 nikulipe 10 yako labda ndani ya miaka 6 kuliko unikopeshe milioni 10 nikulipe milioni 18 ndani ya miaka 15...

By the end of 2015 nililamba mkopo binafsi benki nikawa nalimwa kama jiwe mbili na kitu, halafu bodi asilimia 8 wakawa wanalamba karibia 50k ambayo ningekatwa kwa miaka mingi kidogo.. HAMAD ankoli akaivuta hadi asilimia 15 na makato yakajivuta hadi 140 na kitu hivi kama sikosei.. nilivurugwa mno ngoma ikawa inasoma kama negative laki 4 nikawa najiuliza maswali mengi sana yasiyo majibu kuhusu ankoli...

Ila trust me binadamu ana njia zake za kujiadjust kimatumizi (hapa niligombana sana na watu juu ya michango ya harusi, nikachomoka vikundi kadhaa ambavyo vilikuwa na mlengo wa kutoa michango mara kwa mara au on monthly basis na nikakata kutoa hela za vizinga vya kipuuzi nilivyowazoesha wadau..) nilikuwa natumia kwenye vipaumbele vya kifamilia pekee na hata ununuzi wa mahitaji ulikuwa wa jumla na akili ya kukomaa na michongo ya kando kuongeza senti ikaja.

Ndani ya miaka kama mitatu hivi mzigo ukaisha simultaneously na makato ya benki, nikapata relief, lakini sikwenda kudai clearance certificate bodi ya mikopo as i knew wataniongezea kama mil 4-5 cha juu (kuna kitu moyoni kilikuwa kinaniambia itafutwa)

Nilichojifunza; kama niliweza kuishi kwa amount ambayo kwangu niliiona ndogo back then, imenipa ujasiri wa kuweza kujibana zaidi na adabu ya matumizi. Sasa naweza kujibana na kuassume naweza kuishi kama nina yale makato nikaficha kiasi kizuri cha akiba.

*NAJUA UNAWEZA USINIELEWE KWA SASA, HATA MIMI NILIKUWA NA MAUMIVU NA JAZBA SANA..
**Uzuri ameshaanza kuachia madaraja na kuna dalili za kupandisha mzigo.. mambo yataanza kutembea kwa hesabu za mwaka mwaka.. lets have faith ndugu
 
Kikubwa ulitakiwa ujue deni lako halisi baada ya juhitimu lilikuwa kiasi gani, mimi wakati nahitimu 2011 tulipewa vijitabu vinavyoonesha kila ulichopewa na HESLB, kuanzia hapo ujue umelipa kiasi gani toka ulipo anza kukatwa ili unapenda bodi uwe na evidence za kutosha
Nilimaliza chuo kabla yako. Nilikuwa nalijua deni langu halisi tulipewa ile hati ya deni kamili kutoka bodi baada kuhitimu chuo...

Nilishamaliza deni langu tayari na ile penati ndogo kabla ya hili balaa la retention fee halijaja.. sasa after retention sisi tuliomaliza tuliletewa statement mpya ya deni la ajabu ila tulikuwa hatujaanza kukatwa
BORA MAMA KAIFUTA AISEE
 
Wanaokatwa wengi hii 6% huwa haiwekwi kwenye salary slip sababu inaongezeka kila mwaka. Hivyo wanasubiri umalize kulipa hela uliyokopa hadi isome zero kwenye slip ndipo wakuwekee sasa deni jipya la VRF
Kwahiyo unamaanisha watatoa Statement mpya zenye deni halisi bila hizo nyongeza za 6% walizokua wanaongeza kila mwaka baada ya mnufaika kumaliza masomo?
 
Nilimaliza chuo kabla yako. Nilikuwa nalijua deni langu halisi tulipewa ile hati ya deni kamili kutoka bodi baada kuhitimu chuo...

Nilishamaliza deni langu tayari na ile penati ndogo kabla ya hili balaa la retention fee halijaja.. sasa after retention sisi tuliomaliza tuliletewa statement mpya ya deni la ajabu ila tulikuwa hatujaanza kukatwa
BORA MAMA KAIFUTA AISEE
sema bora bwana yule kafa
 
sema bora bwana yule kafa
Hamna bwana mkuu, sote tutakufa, muhimu ni kutakiana radhi njema na kuomba Mungu penye ugumu na kadhia pakae sawa..
Jaribu kuimagine kuna binadamu walipitia enzi za kufanywa watumwa bila shaka waliumia sana nyoyo na kulia vizazi kwa vizazi ila ikafika wakati Mungu akafanya afueni zile zama zikaisha na maisha yakaendelea...

Tunashauriwa subira, uvumilivu na kutokata tamaa kumuomba Mungu..
 
Wengi ilitukuta hiyo Yukawa na take home ya laki 1.6 hadi laki 2
Hata hamu ya kazi ilipotea
Hahahahaa ilikuwa hatari ndugu, halafu hakukuwa na dalili za ongezeko la 'salare' wala madaraja aisee.
Plus reduced or no seminars wala workshops,
 
Mama Samia miaka 9 tena. Sasa hivi tutalipa tulichokopa tu bodi ya mkopo. Hongera mama.

=====

SERIKALI imefuta tozo ya asilimia 6 ya thamani ya deni la wanufaika wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu (HESLB) iliyokuwa ikitozwa zaidi.

Agizo la kufutwa kwa tozo hiyo imetolewa leo na Rais Samia Saluhu katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Mwanza.

Akitoa agizo hilo Rais Samia alisema “Serikali imeamua kufuta asilimia 6 iliyokuwa ikitozwa zaidi, lakini hata hivyo tumeamua riba ya asilimia 15 itabaki kama ilivyo.

Awali Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) liliwasilisha kilio cha wanufaika wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu (HESLB) kwa Rais Samia Suluhu, na kutaka ongezeko la makato ya mkopo huo ipunguzwe na tuzo nyingine ziondolewe.

Akisoma risala Kaimu Katibu Mkuu wa Tucta, Said Wamba alisema mikopo ya elimu ya juu imegeuka kiama kikubwa kwa wafanyakazi na inapoteza dhana halisi ya serikali kuwa wanaopewa mikopo hiyo ni watoto wa maskini.

Alisema tozo ya kutunza thamani ya mkopo ya asilimia 6 (Value retention fee -VRF), tozo ya asilimia moja ya shughuli za kiutalawa (Loan Administration Fee) na adhabu ya asilimia 15 ya deni linalodaiwa kwa anayechelewa kulipa deni baada ya miaka miwili tangu kuhitimu chuo ni kaa la moto kwa wanufaika.

“Tozo ya asilimia 6 ya thamani ya deni inakuwa kubwa, kila mwaka inaongezeka tofauti na kiasi alichokopeshwa mnufaika, tunataka ipungue, mkopo unageuka kiama kikubwa kwa wafanyakazi na inapoteza uhalisia kuwa ni watoto wa maskini.” alisema Wamba na kuongeza

“Viwango au makato haya yanafanya vijana kutopiga hatua yeyote. Pia ni kinyume na katiba yetu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 23(1) inayohitaji mtu kupata ujira kulingana na kazi yake,” alisema Wamba

Kwa mujibu wa Sheria Bodi ya Mikopo ya 2016, Kifungu 7.2.1.1 cha Mwongozo wa HESLB wa Utoaji Mikopo na Ruzuku kwa Wanafunzi kinabainisha kuwa mnufaika wa mkopo wa bodi hiyo atalipa tozo ya kulinda thamani ya fedha ambayo itakatwa asilimia sita kwa mwaka tangu tarehe mnufaika aliyoanza kupokea mkopo.

Pia, katika kifungu 7.2.1.2 cha mwongozo wake huo, HESLB inaeleza kuwa itakata asilimia moja ya ada ya uendeshaji kwa mwanafunzi mnufaika.
View attachment 1770644
Mbona watu wanakatwa tena
 
Back
Top Bottom