Mama Samia miaka 9 tena. Sasa hivi tutalipa tulichokopa tu bodi ya mkopo. Hongera mama.
=====
SERIKALI imefuta tozo ya asilimia 6 ya thamani ya deni la wanufaika wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu (HESLB) iliyokuwa ikitozwa zaidi.
Agizo la kufutwa kwa tozo hiyo imetolewa leo na Rais Samia Saluhu katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Mwanza.
Akitoa agizo hilo Rais Samia alisema “Serikali imeamua kufuta asilimia 6 iliyokuwa ikitozwa zaidi, lakini hata hivyo tumeamua riba ya asilimia 15 itabaki kama ilivyo.
Awali Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) liliwasilisha kilio cha wanufaika wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu (HESLB) kwa Rais Samia Suluhu, na kutaka ongezeko la makato ya mkopo huo ipunguzwe na tuzo nyingine ziondolewe.
Akisoma risala Kaimu Katibu Mkuu wa Tucta, Said Wamba alisema mikopo ya elimu ya juu imegeuka kiama kikubwa kwa wafanyakazi na inapoteza dhana halisi ya serikali kuwa wanaopewa mikopo hiyo ni watoto wa maskini.
Alisema tozo ya kutunza thamani ya mkopo ya asilimia 6 (Value retention fee -VRF), tozo ya asilimia moja ya shughuli za kiutalawa (Loan Administration Fee) na adhabu ya asilimia 15 ya deni linalodaiwa kwa anayechelewa kulipa deni baada ya miaka miwili tangu kuhitimu chuo ni kaa la moto kwa wanufaika.
“Tozo ya asilimia 6 ya thamani ya deni inakuwa kubwa, kila mwaka inaongezeka tofauti na kiasi alichokopeshwa mnufaika, tunataka ipungue, mkopo unageuka kiama kikubwa kwa wafanyakazi na inapoteza uhalisia kuwa ni watoto wa maskini.” alisema Wamba na kuongeza
“Viwango au makato haya yanafanya vijana kutopiga hatua yeyote. Pia ni kinyume na katiba yetu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 23(1) inayohitaji mtu kupata ujira kulingana na kazi yake,” alisema Wamba
Kwa mujibu wa Sheria Bodi ya Mikopo ya 2016, Kifungu 7.2.1.1 cha Mwongozo wa HESLB wa Utoaji Mikopo na Ruzuku kwa Wanafunzi kinabainisha kuwa mnufaika wa mkopo wa bodi hiyo atalipa tozo ya kulinda thamani ya fedha ambayo itakatwa asilimia sita kwa mwaka tangu tarehe mnufaika aliyoanza kupokea mkopo.
Pia, katika kifungu 7.2.1.2 cha mwongozo wake huo, HESLB inaeleza kuwa itakata asilimia moja ya ada ya uendeshaji kwa mwanafunzi mnufaika.