Mikataba ya Madini na Serikali ya Tanzania

Finished. Mbona mazingira ya dili la IPTL na Tanesco ni kama copy (Kopi-raiti) ya hii ishu ya Richmond na Tanesco? Hizi sirikali za bongo kweli ni upuuzi mtupu.
 
Serikali yatakiwa kutosaini mikataba mipya ya madini

na Rahel Chizoza, Dodoma
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

KAMATI ya Bunge ya Nishati na Madini imeitaka serikali kusitisha kusaini mikataba mipya ya sekta hiyo hadi sheria mpya za madini zitakapopitishwa na Bunge.

Akiwasilisha bungeni maoni ya kamati hiyo kuhusu mapendekezo ya taarifa ya kamati ya rais ya kuishauri serikali kuhusu usimamizi wa sekta ya madini, Mwenyekiti wa kamati hiyo, William Shellukindo, alisema ushauri huo unapaswa kuzingatiwa kwa manufaa ya taifa.

Alisema suala la mikataba limeonekana kugubikwa na matatizo makubwa ya usiri, utata na kuna vipengele vinavyokiuka taratibu na sheria za nchi, jambo ambalo linasababisha nchi ipate hasara.

Alisema kutokana na hali hiyo kamati yake imeona ni vema sheria ya madini iandikwe upya kabla ya kusainiwa kwa mikataba mipya, ili kuondokana na mikataba isiyokuwa na manufaa kwa taifa.

Alisema kamati yake imependekeza kuzingatia mitaji ya mwekezaji katika sekta ya madini, ili kuepukana na wawekezaji wababaishaji ambapo imetamka kuwa kiwango cha chini cha uwekezaji kiwe ni dola milioni 600 na kuendelea.

Kamati hiyo pia imebainisha kuwepo kwa upotevu mkubwa wa fedha katika sekta ya madini unaotokana na wawekezaji kupewa unafuu wa kodi kwa asilimia 100 wa gharama za uwekezaji katika kukokotoa mapato yanayotozwa kodi kwa mwaka wa uwekezaji.

“Ni aibu kwa nchi kufuta baadhi ya vifungu vya sheria kwa kushinikizwa kwa kigezo cha kuwavutia wawekezaji huku Watanzania wakiendelea kupata hasara, kwa mfano kifungu cha 14(5) cha sheria ya madini kinapaswa kufutwa, kwani kinaitia aibu nchi yetu,” alisema mwenyekiti huyo.

Shellukindo ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli, alisema kamati imetaka serikali kuweka uwazi katika kusainiwa kwa mikataba na mikataba hiyo ipatikane katika ofisi za wilaya, mikoa na halmashauri ilipo migodi hiyo.

Aidha, kamati hiyo imependekeza kufupishwa kwa uhai wa mikataba ya madini kutoka miaka 25 iliyopo hivi sasa na kufikia miaka 10, ambapo wameshauri ukaguzi ufanyike kila baada ya miaka mitano ya mkataba husika.

Alisema tozo za halmashauri zifanane na tozo zilizopo katika sheria ya fedha za serikali za mitaa na kutowaruhusu wawekezaji kuweka fedha zao kwenye benki za nje ambapo asilimia 70 ya mapato ya madini yanapaswa kurudi nchini.
 
Hizi $240,000.00 ni kwa mwaka au ni kwa muda gani? Kama Barrick wanavuna USD $20m a year with 3% rolyalties to Serikali 9$600,000) then it make sense to claim at least $240000-400000 for local development.
Serikali inapaswa iongeze mgawo wake wa royalties to at least 15% ambapo 40% ya hiyo 15% itawekwa kwenye maeneo ambapo huu uwekezaji unafanyika kwa shughuli za maendeleo kama Shule, zahanati, vyuo vya ufundi, maji, umeme na barabara na si kutumia pesa hizi kulipana mishahara na kununua magari mapya!

Didn't Meremeta make $25 million in 2005 and declared bankcruptcy the next year? If Barrick is making almost the same amount of money, what went wrong with Meremeta?
 
Kama alihusika kwenye Mkataba wa Dudu IPTL kama alivyodai Dk. Slaa basi huyo mama anafahamika vema na aliyekuwa Waziri wa Wizara husika Mhe. Rais JK.

Pili, kwa huyu mama kutajwa kwenye Tume Teule ya Bunge ya Dk. Mwakyembe basi TAASISI YA KUENDELEZA NA KUPAMBA RUSHWA (TAKUKURU)ilitakiwa iwe imeanza kazi ya kumfuatilia huyu mama.


Sasa hivi kateuliwa kuwa mjumbe wa bodi ya TANESCO. Mpo hapo?????? Huyu mama si bure yumkini ni mwakilishi wa mtu mzito katika hizi dubious contracts. Wanagawa naye.
 
Wengine hadi wafe ndiyo watasema STOP. Hawasomi alama za nyakati. Acha wawepo mezani ili siku ya hukumu ikifika, wajulikane na wanaswe mapema kabisa na kwenda kuzila hela zao Keko.

Kweli wanawake na nyie mwachangia katika kukuza UFISADI. Delila na Samson, Anna Mkapa na Benny wake, Merry na EL, Nani na fulani wake..... ila kuna wengine wanao wengi maana kila kamji na nchi ni nyumba ndogo...
 
Huyu mama Maria Kejo[Ndossi] ni mzito sana kiserikali ; kama vile Rostam anavyoogopwa kuguswa kwa siri za viongozi wa ccm anavyozijua, Maria anazijua siri nyingi sana za viongozi wa serikali toka enzi ya Mwinyi na Warioba akiwa waziri mkuu!! Anaogopwa kuthibitiwa kwani atawahusisha wengi wakubwa; mikataba yote iliyopitishwa pale AG chambers enzi za Chenge ina muhuli wa huyu mama! Inaonekana nae watasuasua nae hivyo hivyo bila kumchukulia hatua mpaka atakapostaafu kama walivyofanya kwa wakinn Mgonja.
 
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete jana amefanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Kiislam ya Iran, Bw. Parviz Davoodi ambaye yuko nchini kwa ziara ya siku tatu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, katika mazungumzo hayo Bw. Davoodi alimueleza Rais Kikwete kuwa Iran ina nia ya kuendeleza na kupanua shughuli za kilimo nchini.

Mambo mengine yaliyozungumzwa na viongozi hao ni kuendeleza sekta ya biashara, madini, viwanda, elimu, gesi na masuala ya uvuvi.

Bw. Davoodi alisema nchi yake itatoa misaada kwa Tanzania na italizingatia deni la Tanzania kwa Iran ili kuiwezesha kupambana umasikini kupitia sekta ya kilimo.
Rais Kikwete alimuahidi Bw. Davoodi kuwa ili kufanikisha mazungumzo yao Tanzania itaangalia kufungua ubalozi wake katika mji mkuu wa Tehran ambapo itakuwa ni njia ya kukuza uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Kabla ya kuondoka nchini Bw. Davoodi anatarajia kusaini mikataba saba ama nane ya madini ikiwa ni pamoja na Tanzania kupata huduma ya mikopo kutoka Iran.
========
 
Compare this to any of TZs mining companies board:

attachment.php


Debswana - Board of Directors

wazawa tupu; i don't mind hata kama ni wa serikali...

sasa tazama

attachment.php

attachment.php

attachment.php



TanzaniteOne - The largest and most advanced miner of the rare tanzanite gemstone

Wanamuweka mbongo mmoja ambaye watam'control

Nimejitahidi kupitia hii topic tangu mwanzo na naamini sasa imekaa sawa kimjadala.
 
Duuuhh :shock: :shock: :shock:

Nimesoma mara mbili mbili huo ujumbe wako Mzee Mwanakijiji, yaani hata kile kibanda changu pale bongo nilichopangisha kwa TX mmoja analipa US$ 1200 kwa mwezi, sasa Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa nchi.......US$ 1000 kwa MWAKA!!!!!!! gimme a break guys, wahusika waliosaini huu mkataba ni wahujumu wa uchumi.


Na ndiyo sababu kikawekwa kipengele cha kutomuonyesha "asiyehusika moja kwa moja". Ujinga wa aliyesaini mkataba huo kwa niaba ya serikali hausemeki!
Ujinga wa aliye negotiate mkataba huo kwa niaba ya serikali pia hauna kikomo!
Wakati katiba ya chama "kitukufu" inasema kuwa serikali ni wananchi;)
Tusishangae gurudumu la maendeleo ni zito mno kwenda mbele
 
Na Leon Bahati
Gazeti la Mwananchi

TANZANIA inatarajia kuondokana na adha ya kuingia mikataba mibovu na ya kifisadi kwenye sekta ya madini, nishati na gesi baada ya kujiunga na Taasisi ya Kimataifa ya Kusimamia haki na uwazi wa Mikataba ya Uwekezaji ijulikanayo kwa jina la Extractive Industries Transparency Initiative (EITI).

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi umebaini kwamba kujiunga huko ni faraja kubwa kwa Tanzania ambayo katika miaka ya karibuni imekumbwa na wimbi la mikataba mingi mibovu ya uwekezaji inayoondamana na mipango ya kifisadi na isiyojali maslahi ya wananchi.

Taarifa zilizopatikana kwenye tovuti ya EITI na kuthibitishwa na serikali, Tanzania imejiunga na taasisi hiyo Februari 16, mwaka jana na tayari imeanza kutekeleza hatua muhimu za kuukamilisha uanachama wake.

Lengo kuu la kuanzishwa kwa taasisi hiyo linaelezwa ni kuhakikisha uwepo wa haki na uwazi kwenye mikataba inayoingiwa kwenye sekta hiyo.

"EITI itaweka mikataba hiyo wazi ikiwa ni pamoja na mapato ya serikali yanayotokana na wawekezaji ili kuwapa fursa wananchi kuweza kuyasimamia na kuhakikisha yanatumika vizuri katika kuwaletea maendeleo," inaeleza sehemu ya maelezo ya EITI kwenye tovuti hiyo.

Hata hivyo, maelezo ya taasisi hiyo yanaonyesha Watanzania wataanza kufaidika na taasisi hiyo Februari 15, mwaka ujao wakati ambapo uanachama wa Tanzania utakapothibitishwa na sekretarieti ya EITI inayoongozwa na Jonas Moberg na Katibu wake Mtendaji, Leah Krogsund.

Baadhi ya hatua ambazo tayari Tanzania imeanza kuzichukua ili kuhalalisha uanachama wake ni pamoja na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kuteua timu ya wataalamu watano, miongoni mwao wakiwepo maafisa wa serikali na wadau binafsi wa sekta ya nishati na madini, kufanya kazi na EITI.

Hata hivyo, taarifa za mtandao huo zinaonyesha kwamba Tanzania bado haijamteua mwenyekiti wa timu hiyo, lakini Mwananchi lilibaini kwamba hatua hiyo tayari imetekelezwa na aliyeteuliwa ni Jaji Mstaafu, Mark Boman.

Miongoni mwa mambo yaliyochangia kuundwa kwa EITI ambayo ilianza kufanya kazi kuanzia mwaka 2003 ni "migogoro mingi na wawekezaji iliyoandamana na rushwa na usimamizi mbovu wa serikali za nchi mbalimbali katika sekta ya madini, gesi na mafuta."

"Hizi ni juhudi mahususi na zenye kuleta matumaini kwa kuhamasisha uwepo wa uwazi ili kulinda maslahi ya pande zote (wananchi na wawekezaji)," inaeleza sehemu ya maelezo ya EITI kwenye tovuti yao.

Miongoni mwa faida ambazo nchi wanachama atazipata zinatajwa kuwa ni kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa kuzingatia kanuni zilizoridhiwa kimataifa za kuzingatia uwazi na haki.

Licha ya hayo, EITI inajinadi: "Tunasimamia uwajibikaji na utawala bora pamoja na kuhimiza ustawi wa kiuchumi na kisiasa. Hii itasaidia kuondoa migogoro kwenye maeneo ya uchimbaji wa madini, mafuta na gesi."

Baadhi ya miakataba ya uwekezaji nchini ambayo imelalamikiwa ni pamoja na ya sekta ya madini ambayo inadaiwa kutoinufaisha serikali.

Mikataba mingine ni ya sekta ya umeme ambayo imekubwa na kasoro nyingi zikiwepo za vipengele vinavyowapendelea zaidi wawekezaji na yenye nafasi kubwa ya kusababisha hasara kwa taifa pale inapobidi kuivunja.

Miongoni mwa mikataba ya sekta ya nishati ambayo imeliingiza taifa kwenye misukosuko mikubwa ni ya kuzalisha umeme iliyoingiwa kati ya serikali na kampuni mbili, Independent Power Tanzania (IPTL) kuzalisha megawati 100 na Richmond Development LLC ambao baadaye ulihamishiwa Dowarns kuzalisha umeme wa dharura.

Mkataba na Dowans tayari serikali imefanikiwa kuuvunja, lakini wa IPTL imeshindikana na kwa sasa mustakabali wake inategemea namna itakavyoamuliwa kwenye kesi iliyopo mahakamani.
 
Uhhh!...Hii mambo inakuja wakati ripoti zinasema Tanzanite iliyobaki aridhini ni ya kuchimba kwa miaka 10, then kwisha, sijui kwa madini mengine.!

Lakini najua pia kuwa Mkataba huu unakuja wakati kuna mashimo huko Shinyanga, Mara, Mwanza na Mpanda yaliyoachwa wazi baada ya dhahabu kumalizika.

Mungu saidia watu hawa!
 
Hivi kuweka mikataba wazi ni mpaka tujiunge na shirika fulani la kimataifa? Hivi nchi ni ya Watanzania kweli?
 
Hawa mimi siwaamini hata kidogo. Kama kweli wana nia hiyo basi waanze kuanika hadharani mikataba ya uchimbaji dhahabu iliyosainiwa katika awamu ya tatu.

Majina ya wale mafisadi wa EPA "waliorudisha" shilingi bilioni 70 na kiasi kilichorudishwa na kila mmoja wao hadi hii leo ni siri kali, labda majina hayo nayo kuanikwa hadharani inabidi "tujiunge" na taasisi ya kimataifa. Usanii kila kukicha! Kazi kweli kweli!
 
Hivi kuweka mikataba wazi ni mpaka tujiunge na shirika fulani la kimataifa? Hivi nchi ni ya Watanzania kweli?

Hii sio nchi ya Tanzania ni nchi ya wazungu. Wazungu wanajenga nchi zao kwa rasilimali za Tanzania kilichobaki ni sisi kuwa watumwa ndani ya nchi yetu yenye rasilimali za kutosha lakini tunaitwa nchi masikini.
 
Hii sio nchi ya Tanzania ni nchi ya wazungu. Wazungu wanajenga nchi zao kwa rasilimali za Tanzania kilichobaki ni sisi kuwa watumwa ndani ya nchi yetu yenye rasilimali za kutosha lakini tunaitwa nchi masikini.

Wanasema kwenye miti hakuna wajenzi!
 
Kauli ya Mwanasheria Mkuu Werema kudai kuwa Bunge halina haki au mamlaka kupitia na kuidhinisha mikataba ya Tanzania ni kauli ya kebehi na dharau kwa Bunge la Tanzania na umma wa Watanzania.

Leo hii Tanzania imegubikwa na utovu wa nidhamu unaofanywa na Watendaji na Viongozi kwa mujibu wa Katiba hii hii ambayo imetoa mamlaka yasiyo na mipaka wala udhibiti kitu ambacho kimeangukia kwa Taifa letu kuingia katika mikataba mibovu, lakini Werema anaendeleza wimbo ulio maarufu wa Mafisadi kwa kudai Katiba hairuhusu Wabunge kupitia Mikataba!

Ningekuwa mimi Werema, ningemwambia Mbunge mwenye hoja kuwa Bunge lifikishe mapendekezo ya kubadilisha Katiba na Sheria za nchi ili Mikataba yote ipitiwe na kuidhinishwa na Bunge!

Tamko langu kwa Werema ni hili; pamoja na majibu yako ya kitaalamu, umepuuzia kufuata BUSARA na kung'amua kuwa tatizo la Tanzania si Katiba kuzuia bali ni katiba kunufaisha wachache kwa migongo ya Watanzania na hivyo hitimisho na hukumu ya Mchungaji kwako kwa kauli hii ni kuwa ;- Wewe Werema MWanasheria Mkuu wa Tanzania ni mlinzi wa mianya ya Uhujumu wa Hazina za Taifa letu na Unawalinda Mafisadi!

No need for Bunge to ratify contracts, says AG‏

Leonard Mwakalebela, Dodoma, 3rd February 2010 Daily News

THE government has neither plans, nor strategy of tabling a bill to enable Parliament to ratify all contracts entered by the government.

The Attorney General Mr Frederick Werema told the National Assembly today that such move would be contrary to the Constitution of the United Republic of Tanzania.

According to him, such contracts, which are commercial by nature, are being made by government servants as per section 35 (1) of the Constitution.

The AG also told the House that the President, according section 33 (2) of the Constitution, was the head of the government apart from being Head of the State and Commander in Chief.

The AG was answering questions by Ussi Amme Pandu (Mtoni-CCM) on behalf of the minister for Justice and Constitutional Affairs.

The MP wanted to know as to when the government would table such a bill because such confidentiality of the contracts was fuelling corruption.

Mr Werema noted, however, that the Bunge still had the chance of advising and monitoring the government on contracts as per section 63 (2) and (3) of the Constitution.

“It’s not true that the current arrangement fuels graft. Your Parliament enacted Public Procurement Act which has put in place conditions to be observed while entering into contract.

The conditions are supervised by the government through Public Procurement Regulatory Authority (PPRA) which has mandate of nullifying unsatisfactory contracts,” the AG explained.

He stressed that there were neither suggestions, nor evidences that there were ghost contracts entered by some of the public organisations and government institutions.

“What I know is that there’re arguments and feelings among experts that there’re valid contracts whose conditions are painful to the nation or did not take into consideration national interest,” observed Mr Werema.

He said that according to Act no.4 of 2005, the office of AG was obliged to advise the government on commercial contracts and international conventions and protocols.

The AG urged the public to have confidence in their government and that the government would not bless contracts which were not in public interest and welfare.

 
Back
Top Bottom