Mikataba ya Madini na Serikali ya Tanzania

Rev. Kishoka

Aliteuliwa kulinda masilahi ya mafisadi, ndo maana yupo tayari kulinda sheria mbovu ambazo kama mwanasheria mkuu alitakiwa kutoa ushauri ambao utaziba mianya ya kuwa na mikataba mibovu au kushauri katiba ibadilishwe, na ni rahisi tu mapendezo yaliyotelewa na tume ya majaji iliyoundwa kupitia na kupendekaza katiba inayoendenana na mabadiliko ya kisisa, kiuchumi na utandawazi, zilkitumika hela nyingi na yalikuwa mapendekezo lakin waliokuwa karibu na mkuu walimwambia achana nayo kwani ingewanyima ulaji, hawa ni viongozi wapo tayari kuona nchi na wananchi wanateketea ili mradi walimbikize mali ambazo hawatakula wamalize. kiujumla na uchoyo uliopita tafsiri
 
Hakuna bunge tanzania, kuna genge la wahuni waganga njaa, na wanyonyaji wa haki za wenye nchi kisheria
 
Bunge halipaswi kufanya kazi ya kupitia mikataba-Nagu

Na Radio One Habari
2007-07-09


Serikali imesema Bunge halipaswi kufanya kazi ya kupitia mikataba kabla ya kutiwa saini ili libaki na uhalali wake wa kuiwajibisha Serikali kwa mujibu wa dhamana ya mgawanyo wa mamlaka, kuchunguzana na kuwajibishana.

Akijibu swali Bungeni Waziri wa Sheria na Katiba Mheshimiwa Mary Nagu amesema kazi ya kujadili na kufunga mikataba ni ya watendaji ambayo kwa mujibu wa Katiba Serikali ndiyo inayowajibika kiutendaji na Bunge ni msimamizi na mfuatiliaji wa utendaji wa Serikali.

Hata hivyo amesema Bunge kama msimamizi Mkuu wa shughuli za Serikali lina uwezo na jukumu la kuweka masharti ya jumla inapobidi na kutunga sheria, kupitisha sera au kuidhinisha bajeti ya Serikali.

Ameongeza kuwa katika kutimiza jukumu hilo tayari Bunge limetunga sheria ya ununuzi wa umma na sheria ya mikataba ambazo huiongoza Serikali katika kufunga mikataba ya ununuzi.

Kuhusu usiri katika mikataba Dakta Nagu amesema iko mikakaba ya aina mbili, ya Serikali na Serikali nyingine na mingine ya biashara ambayo hufanywa siri kwa lengo la kulinda maslahi ya biashara hiyo.

Hata hivyo amesema Serikali iko tayari kupokea maoni na ushauri ili kuongeza uwazi na uwajibikaji bila kulimbikiza madaraka katika chombo kimoja cha dola.
Rev. Kishoka,

Sasa nadhani unaona kuwa aloanza kusema si mwanasheria pekee. Ni tangu 2007 wamekuwa wanasisitiza wabunge wasithubutu kutia mguu kwenye mikataba.

Ni kukukumbusha tu mkuu
 
It is very simple: Wabunge wapitishe sheria kwamba kila 'mwekezaji', hawezi pewa mkataba ambao haujawa 'vetted' na Bunge (assuming bunge lina uwezo wa kuingia mikataba ya maana). Lakini wabunge haohao wameridhia mikataba ya EAC, ambayo ni bomu kuliko hiyo ya madini... so it won't work.

It is the ideology that is flawed or missing altogether: we should sell them the gold that is underground. Cost of taking it out is up to them, lakini tunawauzia gold wholesale price, including taking percentage of gold mined. If they make profit or loss, it is up to them. We don't need their 'charity' work. They can do that if they want. But to be able to create a contract like this, requires understanding of nani aliyeshikilia 'makali' au 'mpini'
 
Wanabodi,

Mimi nina swali moja tuu kuhusu hii ishu ya mikataba , Kwa nini inakuwa siri ? Mimi nilitegemea ya kuwa mikataba ingekuwa inawekwa wazi ili wananchi wajue what to expect !

Mikataba hii inagusa maisha kila either direct or indirect kwa hiyo wazalendo tuna kila sababu ya kujulishwa . Kitu ambacho kinaniuma sana ni baadhi ya viongozi kujiona ya kuwa wao ni smart na sana kuhisi ya kuwa watz wengine ni mambumbu .

Ningefurahi sana kama tungepata kopi ya hiyo mikataba ili tuwezekuisoma between the lines.

Ahsante, kweli katika hili tuko pamoja. Mara nyingi nimekuwa najiuliza kuwa hawa watu wanafanya kazi kwa maslahi ya nani? Ni siri gani hizi hata wabunge hawawezi kuziona? Nani mwenye dhamana ya moja kwa moja?
 
Kama Richmond sasa imekwisha,je mikataba mingine mibovu itachukua miaka mingapi kujadiliwa ndani ya Bunge letu?
 
no-country-for-old-men.jpg
 
Tanzania! its has been 49 yrs and the country rich of resources is still poor! But did you know A Canadian firm acquired additional properties in mining, Katario and Kibara at Mrangi area in Mara region, and they are granted 100% interest of the areas, the project that covers 26,000 acres? wapi tunaenda Tanzania?
 
Ningependa kuanza kwa kumquote Obama wakati wa chakula cha usiku na Hu.

"A reverence for family, the belief that with education and hard work and sacrifice, the future is what we make of it and, most of all, our desire to give our children a better life," Obama said, enumerating what he called common values between the U.S. and China in toasting Hu.

Je sisi watanzania tuna hizo VALUES?.....hatuna, na viongozi wetu hawana, ndio maana tuna haya matatizo ambayo tunayo sasa.

1. hakuna BELIEF IN EDUCATION....ndio maana wanafunzi wanastrike kila kukicha

2. hatuna BELIEF IN HARD WORK....ndio maana barabara na majengo yanajengwa kirahisirahisi ili mradi watu wapate hela za chapchap wasepe.

3. hatuna BELIEF IN SACRIFICE.....viongozi wetu wanajipenda sana, ndio maana wanakaa kwenye majumba yanayokarabatiwa kwa mabilioni kwa mwaka, na kuendesha mashangingi.

na mwishowe

4. hakuna BELIEF IN THE FUTURE AND THE DESIRE TO GIVE OUR CHILDREN A BETTER LIFE....wanajali maisha ya sasa na mambo ya leo bila kuangalia nchi watakayoiacha wakimaliza muda wao.


Jamii yetu ikibadilisha mtazamo wake, nakuanza kuwa na belief in values kama hizi, tutafika mbali sana.

Naomba kuwakilisha hoja.
 
Ni kwasababu tunachagua viongozi wabovu

Hata mahali tukiamua kuchagua viongozi wazuri mfumo uliopo unampitisha kiongozi mbovu aliyeshindwa.
Ndio maana mpaka leo NEC haiwezi kusema kwa uhakika aliyeshinda urais (kama alishinda) alishinda kwa kiwango gani.

Mifano iko mingi Segerea, Kilombero, Shinyanga, Mtwara, Karagwe, Kahama n.k

Mfumo wa ubinafsi umetawala toka kwa kiongozi mpaka anayeongozwa, mkubwa hadi mtoto. Mipango yetu ni ile inayotazama na kutimia in one's life time. Hatuwazi nini cha maana nitaacha hapa duniani ambacho watoto wa watoto wangu watafaidika nacho.

Ndio maana leo hii wapo wanaowatetea watuhumiwa wa uovu nchini simply because matumbo yao yameshibishwa.

Tunahitaji kukaa kama jamii ya watu kukaa na kutafakari kama bado tunataka kubaki jamii moja ya watu (one people)
 
Mikataba mibovu sio chanzo, ni tunda.

Matatizo ya Tz ni mengi, yana sura tofauti na majibu yake pia hivyo hivyo. Kwa uchache:-
1) Nchi kutokuwa defined na kuwa national codes of ethics
2) Mifumo mbovu wa elimu maarifa
3) Mifumo hasi ya kumwendeleza mwanadamu kielimu, kiafya, kijamii na kimaadili
5) Sheria na Mifumo mibovu ya mihimili mikuu ya nchi
6) Sera za ujima katika karne ya sayansi na teknlojia
7) Ubinafsi na choyo kwa mtu mmoja mmoja, familia na Taifa kwa ujumla
...........endelea
 
Watanzania tunalalamika kwamba Madini yetu hayatunufaishi kwa sababu ya mikataba mibovu
ambayo serikali yetu imeingia na wawekezaji.

Wakati sisi tunalalamika, ofcourse, wakati watanzania wanapigika kimaisha huku wageni
wakifaidika na dhahabu zetu kwa Mfano, Rais Jakaya Kikwete bila kujijua kwamba anatoa
ushahidi wa kwamba ni yeye ndiye aliyeiingiza nchi yetu katika mikataba ya kijinga,
anajisifu huko nje namna hii

"Ladies and Gentlemen;
Since, the early 1990’s we have witnessed increased Canadian investments in Tanzania, particularly in gold, nickel and natural gas development. Today Canada is the largest investment source in mining and gas. It is heart-warming indeed, for me to have had the opportunity to play a part in these important developments. I was the Minister for Energy and Minerals (1990 – 94) who did the spade work of talking to Canadian companies and encourage them to come and invest in Tanzania. I still have fond memories of my visits and meetings with prospective investors in Ottawa, Toronto, Vancouver and Calgary. It was these meetings that brought companies like, Placer Dome, Ocelot, Trans-Canada, Sutton Resources, Pangea Minerals, etc take interest in Tanzania. Later Barrick and Xtrata Minerals followed."

Maneno haya aliyatoa jakaya mwenyewe katika hotuba yake
kwenye mkutano wa kumbukumbu ya baba wa taifa, uko
Canada Mwezi Machi mwaka huu.

Tunalo
 
Mbona inajulikana Mbona Tundu aliwahi kuonyesha kwenye ufunguzi wa Kampeni za uchaguzi,mkataba mmoja aliousaini mbovu kabisa na kama alienda Calgary ,Canada hilo ni jimbo tajiri ambapo wananchi wake huwa wanaingiziwa bonus kwenye accounts kila mwka kutokana na mgao wa fedha za mafuta,kwa nini hakuiga hayo basi
 
Nchi yetu ni shamba la bibi.
Tunahitaji mabadiliko makubwa kwenye sekta ya madini. Najiuliza kwa nini hatukujifunza kwa kuangalia mikataba ya madini kwenye nchi nyingine kama Ghana, South Africa nk. Au sisi ndo wa kwanza kuingia mikataba ya uchimbaji madini hapa duniani?
 
Tatizo sio mikataba... ishu tunauza rasirimali zetu pasi kujua thamani halisi ya hizo rasilimari. Upo hapo? Ndo maana tunajikuta tayari tumekwisha saini hiyo mikataba. Kumbukeni hayo ni Madini na madini yapo aridhini. Sisi hatuna technology ya kujua ni kiasi gani cha madini kipo chini. Eti unamtegemea mnunuzi ndo akuambie thamani ya mali uliyonayo mkononi?? Nafikiri kwa tulipo fikia inabidi tuwachukue machinga pale BBA wakasaini hii mikataba kwani angalau wao uwa wanajua kuiflate price hata mara nne na ukiingia kichwa kichwa umekwisha au utatua kwenye thamani halisi.
 
Back
Top Bottom