Mikataba ya Madini na Serikali ya Tanzania

Mikataba ya Madini na Serikali ya Tanzania

Yes, kuna tatizo. Ni chain work, nadhani kuna mkakati wa kimkukuta kwa cream ya watawala.
Lakini tatizo zaidi ni la watanzania wenyewe, yote yatokeayo ni njozi tu. Lilililo sahihi ni CCM daima milele, kama chama kimeoza tutatia pamba puani tusisikie harufu, na kuvaa miwani ya rangi tusione kinyaa, lakini kura kwa kishindo tu. Mambo ya Kitetoooooooooo!!!
Ufisadi unalelewa na watanzania wenyewe, utasikia wakisema waacheni tu Mungu anaona. Lakini kibaka akikwapua mtaa wa kongo, wanamvisha tairi na kumchoma moto to arshes.
Si bora huyo anayetafuta kamhogo mumwachie Mungu amhukumu kuliko hao.
 
Atomic Resources to Commence Drilling in Tanzania

Tuesday June 17, 2008, 10:31 am


Original Announcement: Atomic to Commence Drilling in Tanzania

Atomic Resources announced that it has signed a contract with a Zambian based company to commence drilling on the Ngaka coal deposit in Southern Tanzania. The rig has mobilized and is expected to arrive on site early in July. The intention is for the diamond drilling rig to complete a comprehensive programme of work aimed at confirming a JORC compliant resource at the deposit. The company also advised that the deposit has potential target of between 90m and 110Mt of thermal coal based upon the extensive and detailed previous work completed in 1950's.
 
Tunako elekea mimi sikujui ila nina wasi wasi mkubwa na jinsi CCM inavyo fanya mambo na Serikali yake .
 
Tunako elekea mimi sikujui ila nina wasi wasi mkubwa na jinsi CCM inavyo fanya mambo na Serikali yake .

sijui ni organisation ndio mbovu na kushindwa kazi au ndio kumaanisha nchi imeshauzwa hii. Nina wasiwasi kama 2010 itafika salama salmini kwa mwendo huu.
 
Kuna taarifa zozote huko nyumbani zimetolewa kuhusu kuanza kazi ya uchimbaji LINDI kutoka kwa kampuni jamani? Nini hatma ya hao wachimbaji wadogo na ni nani hasa mmiliki mzawa. Any idea

Habari kama hizi za 'wawekezaji' kuchukua migodi yetu kwa bei ya bure kabisa kila kukicha unaziona kwenye vyombo vya habari vya nje. SIRI KALI haiwaambii chochote Watanzania!!! 'Wawekezaji' wanachukua maeneo makubwa yenye itajiri mkubwa wa madini kila kukicha lakini Watanzania hatuoni manufaa yoyote!
 
Public Information - DLKM website

http://www.douglaslakeminerals.com/directors.html

Directors - DLKM
Honorable Joseph Rugumyamheto, Chairman of the Board
The Honorable Joseph Rugumyamheto retired in January 2006 after 30 years of public service in Tanzania. For the past five years, Hon. Rugumyamheto has been the Permanent Secretary in the President's Office of Tanzania, reporting directly to the President of Tanzania. He graduated from Stanford University in the US and was responsible for all civil servants in the Tanzanian government.

Legal Counsel - Tanzania
Maajar, Rwechungura, Nguluma & Makani

DLKM revenue:

2006 - US $400,000
2007 - US $ 1,000,000 (Forecasted)


DLKM claims to be the second (after Barrick Gold) to have largest prospecting licenses in Tanzania.

With such small capital, how many locals (individuals or in groups) have been hindered the opportunity to prosper?

DLKM has acquired the said licenses in the last 3 years i.e.from 2005 to date.

2005 !!! Kuna nini hapa ???

Inauuuuuma saaana........ !!!
 
Habari kama hizi za 'wawekezaji' kuchukua migodi yetu kwa bei ya bure kabisa kila kukicha unaziona kwenye vyombo vya habari vya nje. SIRI KALI haiwaambii chochote Watanzania!!! 'Wawekezaji' wanachukua maeneo makubwa yenye itajiri mkubwa wa madini kila kukicha lakini Watanzania hatuoni manufaa yoyote!

Bubu hivi unajua Raia, kwa mujibu wa Sheria, haruhusiwi kumiliki ardhi yenye madini kwa sababu madini ni ya wote? Na unajua kwamba mtu ambae sio Raia haruhusiwi kumiliki ardhi Tanzania - iwe na madini au haina madini?

Sasa hawa tunaowamilikisha ardhi za madini -tena wageni - hivi tuna tunafikiri nini sisi, mbona tunatukana sheria zetu wenyewe?

Kama alivyosema Ndesamburo, kuna siku Watalii watakuja kuangalia hawa binadamu wa Serikali wakoje wakoje hawa.
 
Habari kama hizi za 'wawekezaji' kuchukua migodi yetu kwa bei ya bure kabisa kila kukicha unaziona kwenye vyombo vya habari vya nje. SIRI KALI haiwaambii chochote Watanzania!!! 'Wawekezaji' wanachukua maeneo makubwa yenye itajiri mkubwa wa madini kila kukicha lakini Watanzania hatuoni manufaa yoyote!


hivi hakuna directory ya haya makampuni ambayo iko wazi (achana na ukiritimba wa BRELA), kwa nini haya makampuni hayaingii ata least kwenye stock market na watanzania wakajinunulia vijihisa humo, au yapo jamani?
 
hivi hakuna directory ya haya makampuni ambayo iko wazi (achana na ukiritimba wa BRELA), kwa nini haya makampuni hayaingii ata least kwenye stock market na watanzania wakajinunulia vijihisa humo, au yapo jamani?

haya makampuni mengi kwa vile wanatuibia sisi na hawatataka sisi tujue zote zina trade new york,london na tokyo
 
Press Release Source: Douglas Lake Minerals


Douglas Lake Minerals acquires massive 430 sq km alluvial gold deposit


VANCOUVER, May 9 /PRNewswire-FirstCall/ - The company is pleased to announce today that it has concluded an agreement with a Tanzanian National who holds the mineral rights to four Prospecting Licenses (PL's). The PL's cover an area of 430 square kilometers, and are situated in Mbwemkuru in the Lindi Region in Southeastern Tanzania.

Source: Douglas Lake Minerals

Huyu Tanzanian National ni nani huyu? lazima tufanye juu chini ili tumjue huyu ni nani maana sasa huu uporaji dhidi ya nchi yetu umekithiri kupita kiasi.
 
Huyu Tanzanian National ni nani huyu? lazima tufanye juu chini ili tumjue huyu ni nani maana sasa huu uporaji dhidi ya nchi yetu umekithiri kupita kiasi.

Directors
Honorable Joseph Rugumyamheto, Chairman of the Board
The Honorable Joseph Rugumyamheto retired in January 2006 after 30 years of public service in Tanzania. For the past five years, Hon. Rugumyamheto has been the Permanent Secretary in the President's Office of Tanzania, reporting directly to the President of Tanzania. He graduated from Stanford University in the US and was responsible for all civil servants in the Tanzanian government.

Harp Sangha, CEO / President and Director......(mhindi)
Harpreet (Harp) Singh Sangha has over 18 years experience in business financing............

Gus Sangha, Director........(mhindi mwingine)
Gurpreet (Gus) Singh Sangha is self-employed and has been providing management consulting services to various companies since 2004. From 2002 to 2004, Mr. Sangha was manager of Terminal Sawmills Ltd........

David Groves, Director.......(nsungu)
David Groves, BSc Honours and PhD, started his career working for the Geological Survey of Tasmania(Australia).David has also been contracted as a consultant to the Geological Survey of Tanzania.

Waswahili twasema huku ndio kula na kipofu......sisi tulie tu
 
Tunako elekea mimi sikujui ila nina wasi wasi mkubwa na jinsi CCM inavyo fanya mambo na Serikali yake .

yaelekea ccm walikufanyia kitu mbaya sana yakhe ! na sidhani kama utasahau ! wee kila kitu ccm ! usipotaja ccm, wewe kama lunyungu basi hoja yako haikamiliki hata kidogo ! nakuonea huruma ice cream kid !
 
yaelekea ccm walikufanyia kitu mbaya sana yakhe ! na sidhani kama utasahau ! wee kila kitu ccm ! usipotaja ccm, wewe kama lunyungu basi hoja yako haikamiliki hata kidogo ! nakuonea huruma ice cream kid !
Kada,
Walimnyang'anya ardhi yake iliyokuwa imejaa dhahabu na kumpa Sinclair.
Mwonee huruma mwenzako hata hakupata compesation.
 
yaelekea ccm walikufanyia kitu mbaya sana yakhe ! na sidhani kama utasahau ! wee kila kitu ccm ! usipotaja ccm, wewe kama lunyungu basi hoja yako haikamiliki hata kidogo ! nakuonea huruma ice cream kid !


Tumeyasoma maoni yako kuhusu Lunyungu.
Una chochote cha kuchangia kuhusu hii mada? 😡


.
 
Mining in Tanzania
Tanzania is rich with natural resources including hydropower, tin, phosphates, iron ore, coal, diamonds, gemstones, gold, natural gas and nickel.

Tanzanian Gold Reserves Deposits
Key: M/OZ = Ounces in Millions
Minimum cash per ounce: $ 270


DEPOSIT M/OZ OWNERSHIP

Golden Ridge 2.2 Barrick
Geita 20 AngloGold Ashanti
Bulyanhulu 19 Barrick
Ridge 8 2.2 AngloGold Ashanti
Kahama 1.8 Barrick/AngloGold Ashanti
Golden Pride 2.7 Resolute
Tulawaka 0.8 Barrick
Buckreef/Rwamagaza 0.7 Gallery Gold
Kitongo 0.6 Gallery Gold
Nyakafuru 0.7 Gallery Gold
North Mara 4.1 Placer Dome
Buhemba 0.8 Tanganyika
TOTAL: 46.6




Mining Majors in Tanzania

Barrick – Lake Victoria District in Tanzania
At the Buzwagi project in Tanzania, Barrick successfully extended the known mineralization along strike and down dip and more than met the objective of doubling the geological resource, adding 2.0 million contained measured and indicated resource ounces. A scoping study is planned for 2005. As well, a $5 million exploration program is designed to extend the mineralization along strike and will test other areas on the property. Over the past few years, Barrick has reduced its extensive land position to 9,000 square kilometres in the Lake Victoria Goldfields, in order to focus on the prospective areas identified during the regional work. Drill programs are also planned in the Golden Ridge and Nzega West areas.

Barrick – Tulawaka JV

The Tulawaka Mine in Tanzania was obtained by Barrick through the acquisition of Pangea Goldfields Inc. in June 2000. Tulawaka is a 70/30 joint venture between Pangea Goldfields Inc., a wholly-owned subsidiary of Barrick, and Northern Mining Explorations Ltd. The site is located approximately 1,000 kilometres from Dar es Salaam and 120 kilometres west of Barrick’s Bulyanhulu Mine. The Tulawaka Mine began production in the first quarter of 2005. The mine is an open-pit operation, recovering half the gold with gravity separation technology and the balance from conventional carbon-in-leach technology. The mine is expected to produce between 75,000 and 80,000 ounces in 2005 to Barrick’s account at an average cash cost of $270-$275 per ounce.The mine life is expected to be 4 years.
Barrick – Bulyanhulu

The Bulyanhulu Mine is located in northwest Tanzania, East Africa, approximately 55 kilometres south of Lake Victoria and approximately 150 kilometres from the city of Mwanza. The mine is an underground trackless operation using long hole and drift-and-fill as its principal stopping methods. Ore reserves are accessed via a surface shaft and an internal ramp system. In 2004, the mine produced 349,864 ounces of gold at a total cash cost of $283 per ounce. In 2005, production is expected to be between 320,000 and 325,000 ounces of gold at an average total cash cost of between $340 and $350 per ounce. Based on existing reserves of 19 million ounces and current production capacity, the expected minimum remaining mine life is approximately 24 years. At the time of acquisition in 1999, proven and probable mineral resources were approximately 3.6 million ounces of gold. At the end of 2004, Bulyanhulu had 19 million ounces of proven and probable gold reserves.
 
Waarabu wameamka, sisi bado twakoroma vitandani!

mbwambo.jpg

Johnson Mbwambo

Raia Mwema
Juni 18, 2008


WIKI iliyopita nilipata fursa ya kubadilishana mawazo na mtu mmoja ambaye alirejea Dar es Salaam karibuni kutoka katika vijiji kadhaa vya Tanzania alikokwenda kukusanya taarifa kwa ajili ya utafiti anaoufanya.

Bwana huyu alihuzunishwa sana na maisha ya kimasikini aliyoyakuta huko vijijini; maisha ambayo yamezidi kuwa magumu kutokana na kupaa kwa bei ya mafuta duniani ambako kumesababisha baadhi ya wanavijiji nchini washindwe kununua hata mafuta ya taa.

Kwa mujibu wa simulizi yake, bei ya lita moja ya mafuta ya taa katika vijiji alivyovitembelea ni kati ya Sh. 1,500 na 1700, na kwamba ni wanavijiji wachache mno wanaomudu kununua nishati hiyo kwa kiwango hicho cha bei.

Baadhi yao, kwa mujibu wa maelezo yake, sasa hulazimika kuwasha moto nje ya nyumba zao ili kupata mwanga wa kulia chakula cha usiku; kwa sababu ndani ya nyumba ni giza kwa kuwa kandili na vibatari havina mafuta.

Vibatari havina mafuta kwa sababu wanalazimishwa kuchagua kati ya kununua lita moja ya mafuta ya taa (sh. 1,700) au kilo moja ya unga na maharagwe. Wengi huchagua kununua chakula: Ni uchaguzi kati ya kulala kwenye mwanga ukiwa na njaa au kulala na giza ukiwa na shibe!

Wanavijiji hao hulazimika kuchoma magogo nje ili waendelee kupata mwanga; huku wakivuta muda kwa kupiga soga kabla ya kuingia ndani ya nyumba (nyumba au mbavu za mbwa?!) zao zenye giza kulala. Yaani; bei ghali ya mafuta ya taa imewalazimisha warejee kuishi maisha ya zama za ujima!

Siku mbili baada ya simulizi ya jamaa yangu huyo, nikasoma makala katika gazeti moja la njeinayoonyesha jinsi Saudi Arabia, nchi inayoongoza duniani kwa uzalishaji wa mafuta, inavyoogelea, hivi sasa, kwenye ukwasi mkubwa kutokana na kunufaika na kupaa kwa bei ya mafuta katika soko la dunia. Mpaka wakati naandika safu hii pipa moja la mafuta yasiyosafishwa katika soko la dunia lilikuwa linauzwa kwa dola 135.

Kwa siku moja tu Saudi Arabia inatoa na kuuza mapipa milioni 11 ambayo kwa bei ya sasa katika soko la dunia huiingizia mapato yasiyopungua dola bilioni moja kwa siku. Ndiyo, dola bilioni moja kwa siku.

Ukwasi huo mkubwa uliochangiwa kwa kiasi kikubwa na kupaa, kwa hivi karibuni, kwa bei ya mafuta katika soko la dunia, kumeifanya Saudi Arabia kuanza kufikiria kufanya mambo makubwa zaidi.

Hebu zifikirie kichwani mwako duniani hizo mbili tofauti: Saudi Arabia wanachekelea kwa furaha bei ya mafuta inavyozidi kupaa katika soko la dunia; lakini maelfu ya Kilomita katika kijiji masikini cha Tanzania, wanavijiji wanateseka kutokana na bei hiyo ya mafuta. Furaha yao (Waarabu) ndiyo kilio chetu.

Hata hivyo, ninachotaka kujadili leo si duniani hizo mbili tofauti; bali ni taarifa iliyomo katika makala hiyo kwamba Saudi Arabia inajiandaa kwa miaka ya mbeleni ambako mafuta yake yatakwisha au bei itashuka sana kutokana na nchi nyingi kuhaha, hivi sasa, kutafuta nishati mbadala ya bei nafuu; hususan Biofuel.

Katika maandalizi yake ya kukabiliana na hali hiyo wakati itakapowadia, Saudi Arabia imeamua kuutumia ukwasi wake wa sasa kujenga uchumi mbadala wa mafuta ili visima vyake vitakapokauka, isiathirike kiuchumi.

Ni katika maandalizi hayo ambapo imeibuka na mradi mkubwa wa ujenzi jangwani wa miji sita mipya mikubwa ya kibiashara ukiwemo ule mkubwa kabisa unaoitwa King Abdullah Economic City (KAEC).

Inaelezwa kwamba KAEC utakuwa sawa na Washington DC, utakuwa na bandari kubwa kabisa duniani na utakuwa na ukanda wa biashara na burudani na ukanda wa elimu vkiwemo vyuo vikuu kadhaa. Mradi wa ujenzi wa miji hiyo mipya sita utakamilika katika kipindi cha miaka 15 ijayo.

Nilipomaliza kuisoma makala hiyo ndipo fikra zangu ziliporejea nyumbani Tanzania na kuanza kujiuliza maswali kibao. Kama Saudi Arabia imeshaanza kuingiwa na hofu kwamba siku moja maliasili yake hiyo (mafuta) itakwisha na imeanza kujiandaa kwa hilo, je sisi Tanzania hatuna hofu kwamba madini yetu nayo siku moja yataisha kabisa ardhini? Kama fikra hizo tunazo; je na sisi tunajiandaa kwa hilo kama wajiandaavyo Wasaudia?

Saudia Arabia imeamuya kuutumia ukwasi wake unaotokana na mafuta kujenga miji mipya sita mikubwa ya kibiashara – ili mafuta yao yatakapokwisha; angalua wawe na miji hiyo sita mipya ya kuonyesha. Je, sisi madini yatakapomalizika katika ardhi yetu, tutakuwa na lipi la kuwaonyesha wajukuu wetu kwamba hiki na hiki na kile vilitokana na madini tuliyokuwanayo zamani?

Historia inaonyesha kwamba maliasili kama mafuta au madini vinapopatikana mahali huwa ndiyo chimbuko la baadhi ya miji mikubwa ya kisasa kujengwa katika maeneo hayo.

Chukua mfano wa Johannesburg – moja ya miji inayovutia sana barani Afrika. Johannesburg ni mji uliojengwa vizuri. Una barabara pana nzuri, majengo marefu na mandhari ya kuvutia inayomfanya mgeni ajihisi kuwa pengine yuko Marekani au Ulaya.

Lakini kabla ya mwaka 1886 ilipogundulika dhahabu hapo, eneo hilo halikuwa na chochote cha kuvutia. Kukua kwake ni matokeo ya uwekezaji uliofanywa na unaoendelea kufanywa na makampuni ya uchimbaji madini nchini humo.

Je, sisi katika Tanzania ni mji gani mkubwa na wa kileo ambao tunaweza kujivunia kwamba huu tunao kwa sababu ya dhahabu au almasi iliyokuwa inachimbwa maeneo hayo? Je si kweli kwamba tanzanite zinaisha Mererani, na kwamba kitakachobakia pale na maeneo yale kuonyesha wajukuu zetu ni mashimo tu?

Kwa hakika, nashindwa kuielewa Serikali hii ya CCM inashindwa vipi kuhakikisha wawekezaji hawa wa kigeni wanaochimba madini yetu wanawekeza angalau kidogo hapa nchini mwetu kabla hawajatuachia mashimo.

Tanzania inayo kiwango kikubwa cha madini yakiwemo dhahabu na tanzanite ambayo haipatikani popote duniani. Tanzania ni nchi ya tatu barani Afrika kwa utoaji wa dhahabu ikitanguliwa na Afrika Kusini.

Lakini tofauti na Afrika Kusini ambayo imeweza kutumia utajiri wake wa madini kujenga uchumi imara unaoongoza bara zila la Afrika, Tanzania imeshindwa kabisa kuwafanya wawekezaji katika sekta ya madini wasaidie kujenga uchumi wake; hata kujenga angalau nyumba zao za kuishi hapa nchini!

Wawekezaji hawa wanaishi mahotelini mjini Dar es Salaam na Mwanza. Kila siku asubuhi hupanda ndege kuoka katika miji hiyo kwenda katika migodi yao kusimamia kazi na jiobni hurejea pia kwa ndege katika miji hiyo! Kwa nini, kwa mfano, wasijenge ka-hoteli hata ka ghorofa tatu pale Kahama?

Ni kweli kwamba baadhi ya wawekezaji wamejenga madarasa kadhaa, barabara chache wanakopita na vituo vichache vya afya, lakini je, hivi hayo ndiyo manufaa pekee ambayo Watanzania tunastahili kupata kwa utajiri wao wa madini?

Wenzetu Waarabu (Saudi Arabia) wamezinduka usingizini na kutambua kwamba kuna siku mafuta yao yatakwisha, na sasa wanautumia ukwasi wao unaotokana na kupaa kwa bei ya mafuta katika soko la dunia kujenga haraka miji mipya ya kibiashara kabla mambo hayajaharibika.

Lakini sisi bado tumelala na kukoroma vitandani – hatuna habari kabisa kwamba, siku moja, madini yetu yatakwisha, na hakuna kitu tutakachoweza kuwaonyesha wajukuu wetu kilichotokana na maliasili hiyo.

Mererani tanzanite inaisha, dhahabu katika mgodi wa Bulyanhulu, ambayo hutoa ounces 360,000 kwa mwaka, itamalizika mwaka 2,028, North Mara (ounces 300,000) itamalizika mwaka 2016, Tulawaka (ounces 105,000) itamalizika 2009 na Buzwagi (ounces 250,000) itamalizika mwaka 2,018. Kwa ufupi, itakapofika mwaka 2,028 dhahabu itakuwa imemalizika kabisa katika ardhi ya Tanzania.


Natuamke basi usingizini na kuhakikisha tuna vitu vya maendeleo tutakavyowaonyesha wanetu au wajukuu wakati madini yatakapomalizika na kuwaambia vilitokana na madini tuliyozawadiwa na Mwenyenzi Mungu.

Lakini pia natuamke usingizi na kujiandaa mapema kwa uchumi usiotegemea dhahabu, wala alamasi, wala tanzanite; maana muda si mrefu vyote hivyo vitakwisha.

Nimalizie kwa kusema kwamba nilikuwa na matumaini kwamba pengine mapendekezo ya Kamati ya Rais ya Madini ingekuwa chanzo cha ujio wa mabadiliko makubwa chanya katika sekta ya madini nchini, lakini matumaini hayo yamepungua baada ya kusoma waraka wa
Bw. James Sinclair - Swahiba wa Rais Kikwete.

Akiwaandikia wawekezaji wenzake wa kigeni katika sekta ya madini nchini,
Bw. Sinclair anatamba kwamba ameshaisoma ripoti ya Kamati hiyo iliyowasilishwa kwa Rais Kikwete na ambayo bado ni siri, na anawatoa hofu kwa kuwaambia kwamba ina mambo mazuri kwao.

“Nimepata nafasi ya kupitia mapendekezo ya Kamati hiyo – pamoja na maoni ya Baraza la Madini – na sina matatizo makubwa nayo. Hata hivyo, jambo muhimu kujua ni kuwa uamuzi wa mwisho wa mapendekezo hayo uko kwa rais – na si Kamati,” ndivyo alivyoandika
Bw. Sinclair.

Kwa kauli hiyo ya mwisho ya
Bw. Sinclair; maana yake ni kwamba swahiba wake (Rais Kikwete) hawezi kuwaangusha! Na ndiyo maana matumaini yangu kuona mabadiliko makubwa katika sekta ya madini yakifanyika yamefifishwa na kauli hiyo ya Bw. Sinclair.

Wenzetu Saudi Arabia wameamka usingizini. Sisi tukiendelea kukoroma vitandani; kina Sinclair wa dunia hii wataendelea kutughilibu tushindwe kujenge uchumi imara, tushindwe kusambaza umeme vijiji vyote.

Na kwa sababu ya kushindwa huko kutumia vizuri utajiri huu wa madini tulionao; tumeshindwa kusambaza umeme vijiji vyote, na ndiyo sababu wanavijiji wetu wanaendelea kulala gizani kwa sababu vibatari havina mafuta ya taa!

Tafakari.
 
Ni kweli mkuu madini yetu yana mwisho na hayo yanajulikana kitambo sana tu! Ujambazi wao wanaujua kuwa si mzuri lakini wamechagua hivyo na sisi tuswachague tena!

Nina ndugu yangu anafanya huko Barick na ni geologist aliyekuwa akifanya kazi serikalini na alishawahi kuniambia maneno haya haya wakati huo mwaka 1999 kama sikosei huko Mwanza!

NB:Tanzanite yenyewe haina muda kwasababu huyu ndugu yangu naye alishafanya utafiti kwa niaba ya serikali na kutoa ripoti kama hiyo..Hivyo hilo linajulikana na hapo unaweza kuona ni kwanini kamati ya madini ilikuwa CHANGA LA MACHO!
 
Wakati Sisi Tunaendelea Kulala, Mafisadi Mambo Yao Yako Fresh Kabisaa, By The Time Madini Yanaisha Maisha Yao Na Wajukuu Wa Wajukuu Wao Yatakuwa Yana Uhakika Kabisaa, Kwa Hiyo Sidhani Kama Wanajali Na Hicho Kilio Chenu Cha Madini Yanaisha. Kwa Sababu Nasikia Kuna Fisadi Mmoja Mjukuu Wake Wa Miaka 4 Ana Mabilioni Kadhaa Benki, Huyo Atawaza Kujenga Miji Badala Ya Kujijengea Nyumba Zao? Na Inaweza Ikawa Sio Bongo Tuu Hata Nje Ya Nchi. Tusipoangalia Tutakuja Kuishia Kubaya Sana Huko Tunakoenda.
 
Tunasema weeeeeee hata kitendo kimoja tunashindwa .Watu tumesema tuanze na RA kwente Vodacom bas watu wanaanza maswali kibao na kuombaushahidi .Wache tuendelee kuandika hapa badala ya ku transform mawazo katika vitendo nakulinjusuru Taifa .
 
Back
Top Bottom