Siri nzito mikataba gesi asilia Tanzania

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Na Mwandishi Wetu

NI ukweli usiopingika kwamba majadiliano ya mikataba, hasa ya mafuta, gesi, madini na maliasilia nyingine za nchi huchukua muda mrefu kukamilika.

Hili ni jambo la kawaida hasa kwa Serikali ambayo ni makini na inayobeba jukumu la kulinda utajiri na maliasilia za nchi zisihujumiwe.

Waafrika na watu wengine katika nchi mbalimbali wamekuwa wakifuatilia kwa umakini mazungumzo yanayoendelea kati ya Timu za Majadiliano ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na kampuni za kimataifa za nishati zinazoongozwa na Shell na Equanor.

Hii ni kutokana na mazungumzo ya aina hii kuingiliwa mara kwa mara na Serikali za nchi za kampuni hizo kubwa zinapotoka. Kampuni hizo zinapokwama katika jambo lolote hutumia viongozi wa nchi zao, au viongozi wakubwa wa kampuni hizo kushinikiza kupata mikataba kwa haraka, hata kama mikataba hiyo itakuwa yenye masharti hasi.
Kuna mifano huko nyuma jinsi kampuni kama Equinor ambayo zamani ilikuwa inaitwa Statoil ya Norway zilivyotaka kulazimisha mikataba yenye masharti hasi nchini Tanzania hadi pale “shame campaign” nchini kwao ilivyowalazimisha kubadilika.

Nchini Msumbiji walilazimika kuingia katika mikataba ya uchimbaji wa gesi ambayo bado wengi wanaiona kuwa na athari kwa nchi hiyo hasa katika mgawanyo na matumizi ya rasilimali hiyo nyeti. Kampuni kama Shell zinajulikana ulimwenguni kote kwa kulazimisha kupewa mikataba ambayo haizinufaishi nchi zenye rasilimali kama mafuta na gesi.

Wananchi katika nchi mbalimbali, hasa barani Afrika wamekuwa na shauku ya kujua mikataba inayojadiliwa italeta manufaa gani kwa nchi zao. Lengo ni kutaka nchi ambazo zina utajiri wa maliasilia nyeti hazipotezi mapato kupitia mikataba onevu na inayonyang’anya na kutorosha utajiri na maliasilia hizo.
Majadiliano yanayoendelea nchini yanaangaliwa kwa upekee kwa sababu katika miaka ya karibuni Tanzania imekuwa nchi kinara katika kuhakikisha mikataba yenye athari haipewi nafasi. Wengi wameshuhudia jinsi mikataba ya bomba la mafuta maarufu kama EACOPS ilivyochukua muda kujadiliwa na muafaka kupatikana.

Ni kawaida kwa majadiliano kufanyika kwa kuaminiana baina ya timu za majadiliano. Lakini pia ni kawaida kuwa kabla wahusika wa pande zote kutoa ridhaa zao, rasimu za mikataba pendekezwa ni lazima zikaguliwe na zijadiliwe kwa kina na wataalamu na vyombo mbalimbali baada ya majadiliano ya awali ya timu za majadiliano kukamilika.

Hii ni kwa sababu vyombo vya ridhaa vinapaswa kupata ushauri huru ili kuwepo na nafasi ya kurekebisha vitu ambavyo katika rasimu zinazowasilishwa vinawezekana kutokuwa na ubora au ufasaha unaotakiwa ili mikataba itakayofungwa isiwe na utatanishi wenye athari kwa nchi wakati wa utekelezaji.

Ndiyo maana katika nchi mbalimbali kama Tanzania kuna utaratibu wa Serikali kukagua rasimu pendekezwa na kushirikisha wataalamu mbalimbali na kupata ushauri wa vyombo mbalimbali vya kisera na kiutendaji ikiwa ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kabla ya kupeleka mapendekezo ya ridhaa kwenye Baraza la Mawaziri.

Endapo kuna upungufu uliyobainika katika rasimu pendekezwa ni kawaida kwa timu za majadiliano kuelekezwa kuendelea na majadiliano ili kurekebisha upungufu uliyobainika kabla ya rasimu pendekezwa kuwasilishwa kwa ridhaa ya Serikali.

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa tatanishi ambazo zimetolewa na Serikali ya Marekani ambazo ni muhimu zipate ufafanuzi kutoka kwa aliyetoa taarifa hizo au kampuni zinazohusika na majadiliano hayo. Taarifa ya kwanza tatanishi ilitolewa Bloomberg tarehe 28, Februari, 2024 ambayo iliandikwa na Paul Burkhardt na Kari Lundgren na taarifa ya pili ilitolewa katika gazeti la East African la tarehe 2, Machi 2024 iliyoandikwa na Bob Karashani.

Taarifa ya kwanza inailamu Serikali ya Tanzania kutosaini mikataba kwa kipindi cha miezi tisa baada ya mazungumzo kukamilika. Taarifa ya pili inaripoti onyo lililotolewa na Serikali ya Marekani kwa Serikali ya Tanzania kuwa haitaaminika iwapo inachelewesha mikataba bila sababu.

Msemaji wa Serikali ya Marekani anayetajwa kuwa ni Bi. Basu anasema kuna “delays which are not in good faith and based on the right reasons”. Ameeleza pia kuwa “I’m afraid of the signal it will give to other big investors who want to invest in Tanzanian foundational infrastructure if they can’t rely on the government keeping its side of the bargain”.

Sisi tunaofuatilia maendeleo ya majadiliano tunaelewa kuwa rasimu za mwanzo zilikamilika mwezi wa tano mwaka jana kwa madhumuni ya kuziwasilisha kwa mapitio na uhakiki wa ubora wa pande zote husika kabla ya ridhaa kutolewa kuingia katika mikataba husika.

Kila upande ukiwa huru kupata fafanuzi mbalimbali na kutoa mapendekezo ya marekebisho. Timu za majadiliano zinategemewa kukutana tena ili zikamilishe majadiliano kutokana na maelekezo yaliyotolewa na Serikali. Hivyo, siyo kweli kuwa majadiliano yamekamilika wala rasimu za mikataba bado hazijafika hatua ya mwisho ya kuridhiwa.

Swali tunalojiuliza ni kwanini ghafla lawama zimeanza kutolewa dhidi ya Serikali? Pili ni kwanini lawama hizi zitoke kwa Serikali na waandishi kutoka nje ya nchi?

Je kuna kampeni inatengenezwa kuleta mashinikizo ili rasimu za mikataba ambazo hazijaiva zisainiwe bila majadiliano kukamilika?

Tunajua kuwa kwa unyeti wa majadiliano haya pande zote za majadiliano zinapaswa kuheshimu usiri mpaka yakamilike kabla ya kutoa tamko rasmi baada ya kupokea rasimu zilizokamilika baada ya timu za majadiliano kwa pamoja kutoa taarifa ya kukamilika kwa majadiliano hayo na kuzingatia maelekezo ya vyombo vya uchambuzi na uamuzi vya Serikali.
Hisia zinazojitokeza ni kuwa kuna hila zinafanyika kutaka kuyumbisha majadiliano kwa kutoa taarifa potofu ili Serikali ya Tanzania ilaumiwe.

Kampuni husika zinafahamu fika kuwa majadiliano hayajakamilika na kuwa na rasimu zilizosainiwa Mei, 2023 zilikuwa ni kwa ajili ya kuwasilisha kwenye mamlaka husika kwa ajili ya kuchambua iwapo rasimu hizo zinakidhi viwango vya ubora na uamuzi. Huu ni utaratibu wa kawaida kwenye majadiliano yanayohusisha timu za majadiliano. Ni vizuri kampuni husika zitoe taarifa hizo kwa sababu lawama zinazotolewa zinaonesha kampuni hizo ndizo zinasambaza lawama dhidi ya Serikali ya Tanzania.

Raia Mwema Toleo No.1220 la Jumatano Machi 6-12, 2024
IMG-20240306-WA0007.jpg
 
Ujasusi was kiuchumi unafeli sana!pale tunamwachia mwanasiasa aamue uchumi na hatma ya taifa lake!

Matokeo yake anafanya maamuzi ya kulisha tumbo lake na la wanae TU badala ya taifa!!

Vyote vimeenda kizembe sana na itahitajika madhara makubwa sana kurejesha rasilimali zetu mikononi mwetu!!

"UJASUSI WA KIDOLA NA KIUCHUMI"
 
mhusika mwenyewe always on the road atasoma na kusaini saa ngapi? muda wa kukaa ofisini hakuna …
 
View attachment 2925930
Kwa Wamarekani hakuna cha Siri. Kila kitu kitajulikana tu
 
Mama Samiah hatakubaki kuja kupata lawama huko mbeleni .Mheshimiwa kaza kamba hato hao makuwadi wanapita kwenye ofisi za umma na kutushia oh hiyo gesi baada ya miaka kadhaa haitakuwa na thamani.Ni vyema mradi usiwepo kuliko mama yetu aje abebeshwe msalaaba na mkataba wa ovyo
 
Taifa lilojaa rushwa huwa halini mpango mkakati wowote wa maendeleo,zaidi ya watendaji kutumia nafasi Sao kujinufaisha.Ukiona unasaini mikataba ya hovyo isiyo na tija kwa taifa ni wazi kwamba umezidiwa "akili" na tatizo hilo halipo kwa mwekezaji bali wenye mamlaka ndani ya nchi.

Kitendo Cha gazeti hili kuuliza kwamba,kwanini waandishi wa nje ndo wenye kuandika hayo na sio wa ndani ?kinaonesha ni namna gani media industry ya Tanzania haina weredi pia hakuna monopolization ya stories hivyo hakuna mipaka juu ya uandishi wa habari.

Usipo andika history yako tambau wazi utaandikiwa.
 
Back
Top Bottom