BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,118
Nitataja baadhi ya changamoto ambazo zinarudisha nyuma jitihada za nchi yetu kukuza uchumi na kujiletea maendeleo kama ifuatavyo;
(i) Raslimali za Taifa Ardhi, Gesi, mafuta, madini, misitu, Bandari, wanyama, mazao ya uvuvi nk, kulinufaisha Taifa kwa kiwango kidogo sana kutokana na mikataba mibovu inayoingiwa na Serikali, kuingia mikataba ya siri na baadhi ya raslimali za nchi kukabidhiwa wageni kwa mlango wa nyuma kwa kisingizio cha uwekezaji hali hii inaifanya nchi yetu kukosa mapato ya kutosha kugharamia shughuli za maendeleo na kukuza uchumi wa nchi huku raslimali zake zikinufaisha Mataifa na Makampuni ya kigeni" -Mpina
Luhaga Mpina ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM) amezungumza hayo alipokutana na Wanahabari kwenye Uwanja wa New Amani Complex, Zanzibar wakati wa maadhimisho ya miaka Sitini (60) ya Mapinduzi ya Zanzibar