[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Wednesday, 22 June 2011 21:35
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]'Misamaha kodi za madini inalitafuna taifa'
[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"]
Send to a friend
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Wednesday, 22 June 2011 21:35
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
Fidelis Butahe
MBUNGE wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, amesema Tanzania ni nchi isiyojifunza kutokana na matatizo yaliyopita, na ndiyo maana imekuwa ikiendelea kutumia sheria zinaifanya isifaidike na rasilimali ya madini.
Akichangia hoja kuhusu mswada wa mabadiliko ya sheria ya fedha ya mwaka 2011, jana bungeni mjini Dodoma, Lissu alisema kwa miaka 12 amekuwa akichambua matatizo ya sekta ya madini, ili kuelewa kiini cha uporaji wa rasilimali za madini.
"Nimejifunza mengi, kikubwa nilichokiona ambacho nataka kukipendekeza leo ni misamaha mikubwa ya kodi ambayo ilitungiwa sheria na Bunge hili mwaka 1997,"alisema Lissu. Alisema sheria hizo zimetengeneza kitu alichokiita katika tafiti wake kuwa ni utatu usiokuwa mtakatifu, unaoyafanya mataifa tajiri duniani, kunufaika na madini ya Tanzania.
Lissu alisema juzi Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, aliliambia Bunge kuwa alisema Taifa linategemea kupata Sh32 bilioni kutokana na rasilimali za madini."Tumepewa taarifa ya hali ya uchumi wa taifa ambayo imetueleza kuwa mwaka 2010 sekta ya madini imeingiza Dola 1.5 bilioni za Marekani kwa bei ya Sh1,600 kwa dola moja, hicho kiwango cha mapato yanayotokana na madini yetu kitakuwa zaidi ya Sh4 trilioni," alisema Lissu.
"Hoja ya msingi ni kwamba nchi hii inaangamizwa na misamaha ya kodi na wema mkubwa ambao tumezipatia kampuni tajiri kutoka kwenye nchi tajiri za magharibi ambazo zinatajirika na utajiri wa nchi hii wa madini, tatizo ni ni sheria tu," alisisitiza.
Alisema kilio kuhusu misamaha ya kodi si cha kwake yeye tu lakini kinatolewa pia na timu za wataalamu ndani serikali ambao wameweka wazi kuwa misamaha ya kodi inaliangamiza taifa.
Alisema mwaka 2004, Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye, iliunda tume kuchunguza matatizo ya sekta ya madini na mchango wake katika pato la taifa na kwamba katika mapendekezo yake, tume ilisema taifa linaangamizwa na misamaha mikubwa ya kodi inayotolewa kwa kampuni za madini kwa kutumia sheria za mwaka 1997.
"Mwaka 2005, Rais Jakaya Kikwete aliliambia Bunge kuwa hali ya madini haikubaliki tena, Januari, mwaka 2006 aliunda tume chini ya Waziri wa Nishati na Madini wa wakati huo, Lawrence Masha, ikijumuisha wataalamu 11 na ilitoa majibu kuwa hakuna mafanikio katika sekta ya madini Tanzania," alisema.
Lissu alisema mwaka 2010 Kampuni ya Sofire International Development yenye makao makuu yake mjini London, Uingereza imetoa taarifa kwamba katika kipindi cha miaka 10 kufikia 2008, dhahabu pekee ya Tanzania imeingiza zaidi ya Dola 5 bilioni lakini, mapato ya serikali ya Tanzania ni pungufu ya dola 300 milioni.
"Hii ni kwa sababu ya misamaha ya kodi ambayo Serikali na Bunge hili imekuwa inawapa matajiri wa nchi za nje," alisema Lissu."Leo (jana) tunaletewa muswada wa sheria unaopendekeza sio tu kutoa misamaha kwa maeneo maalum ya uwekezaji, unapendekeza pia kuongeza misamaha ya kodi katika sekta ya madini," alisema Lissu.
Alisema suala la misamaha ya kodi pia lilipendekezwa na Kamati ya Jaji Mark Bomani iliyoteuliwa na Rais Kikwete mwaka 2007 ambayo ilisema kuwa misamaha ya kodi kwa kampuni za madini ifutwe.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]