BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,769
- 288,283
Ngeleja aambiwa mikataba itamletea shida
Mgaya Kingoba, Dodoma
Daily News;
Sunday,April 20, 2008
MBUNGE wa Longido, Michael Laizer (CCM), amesema utekelezaji wa Muswada wa Umeme wa mwaka 2007, utakuwa kipimo cha Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, vinginevyo utamletea shida.
Akichangia majadiliano ya muswada huo bungeni mjini Dodoma juzi jioni, Laizer alisema wabunge sasa wameanza kuogopa miswada inayowasilishwa bungeni kwa sababu wanaipitisha kwa nia njema, lakini baadaye inazaa mikataba mibovu.
Aidha, Mbunge huyo ameahidi kwamba endapo umeme hautafika jimboni kwake ifikapo mwaka 2010, amekwisha kuwatangazia wananchi wa Longido kuwa hatawania tena kiti hicho. Kila mkataba ni ufisadi mtupu. Hii mikataba ndiyo itakuletea shida Ngeleja.
Wananchi wamepoteza imani na mikataba hii, alisema Mbunge huyo wa Longido na kuongeza: Kwa mfano, sisi tunashiriki kupitisha miswada, kisha inazaliwa mikataba inatuletea matatizo. Dowans inachukua milioni 152 kwa siku, tulipitisha hapa; Meremeta Waziri wa Ulinzi alisema ni mradi wa jeshi, Meremeta leo iko wapi?
Iundwe timu au Kamati ya Bunge, mikataba inapoandaliwa timu hiyo ishiriki kuiona na kuiangalia kama ina manufaa. Sisi sasa tumeanza kuogopa miswada inayoletwa bungeni. Nimepiga kelele hapa bungeni miaka 13, tangu wakati wa William Shija, Yona, Dk. Msabaha na Ngeleja huyu.
Mimi sina matumaini ya umeme. Nimewaeleza wananchi wangu kwamba kama umeme hautafika mwaka 2010, sitagombea tena ubunge, alisema Laizer. Alisema anachangia muswada huo kwa masikitiko kwa sababu amebeba mzigo mkubwa wa kupitisha miswada ambayo ilizaa mikataba mibovu, akitolea mfano pia Kampuni ya NetGroup Solutions aliyosema badala ya kutatua matatizo ya wananchi, ilikuwa mzigo mkubwa kwao.
Aliitaka Wizara kuwa makini na mikataba itakayotokana na muswada huo na kuhakikisha umeme unawafikia wananchi wa vijijini. Kwa upande wake, Mbunge wa Iramba Mashariki, Mgana Msindai (CCM), alipendekeza kuundwa upya kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kwa kuanzia kwa Bodi ya Wakurugenzi.
Wapo wafanyakazi ambao wamekulia humo, wamezeekea humo. Sisemi wote ni wabovu, lakini wapo ambao watakuwa ni kikwazo. Ni heri wakapumzike, wapewe chao wakapumzike, alisema Msindai.
Alipendekeza shirika hilo liongezewe nguvu na fedha ili liweze kumudu ushindani utakaoanzishwa na muswada huo ambao kama ukipita, kwa mara ya kwanza Tanzania itashuhudia wawekezaji binafsi katika umeme.
Aidha, alipendekeza Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), isimamie vyema sheria, akisema, Ikizubaa tu, tumekwisha. Hoja yake kuhusu Tanesco iliungwa mkono na Mbunge wa Tunduru, Mtutura Mtutura, ambaye alisema alikuwa mfanyakazi wa Tanesco kwa miaka 15 na analijua vyema shirika hilo.
Alisema limefika hapo kwa kujitakia baada ya kujenga jengo la kitega uchumi kwa Sh bilioni mbili, bila ya haja hiyo; kuuza shamba la kuzalisha nguzo na sasa inazinunua kwa bei kubwa na wafanyakazi wake kununua umeme kwa bei ya kutupa huku wananchi wakiminywa. A
lisema wafanyakazi wa Tanesco wananunua umeme kwa Senti 20 wakati wananchi wanauziwa kwa Senti 165. Shirika hilo alisema lina wafanyakazi 4,670, hivyo kupoteza mamilioni ya shilingi. Mbunge wa Viti Maalumu, Margaret Mkanga (CCM), alifurahishwa na kuondolewa kwa gharama za uzalishaji (capacity charge), akisema kilikuwa chanzo kikubwa cha ulaji.
Mbunge wa Pangani, Mohamed Risherd (CCM), alitaka kupunguzwa kwa matumizi ya mafuta kwa umeme, na kupendekeza wawekezaji wadogo wasiingizwe kwenye Gridi ya Taifa.
Kwa upande wake, Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa (CCM), alisema zipo kampuni ambazo hazilipi kodi, na kuiitaka Wizara ya Nishati na Madini, kushirikiana na Wizara nyingine kuweka tozo katika kampuni hizo zikiwamo za vinywaji baridi na simu za mkononi ili fedha zitakazopatikana zipeleke umeme vijijini.
Mbunge wa Busega, Dk. Raphael Chegeni (CCM), aliitaka Ewura kutoa leseni kwa uhakika ili kutowapa matapeli, huku Mbunge wa Nyanghwale, James Musalika (CCM), naye akitaka mikataba yote ipelekwe bungeni ili wabunge waithibitishe.
Wabunge wataendelea kujadili muswada huo Jumatatu baada ya mapumziko ya mwisho wa juma na wanatarajia kumaliza Jumanne ijayo. Wabunge 50 wameomba kuchangia muswada huo ulioahirishwa mara kadhaa kusomwa bungeni kwa mara ya pili.
My TAKE:
Na nyinyi Wabunge pia ni wa kulaumiwa. Kuna ushahidi wa kutosha kwamba mikataba mingi ni ya kifisadi, lakini kila kukicha hamuhoji chochote kinachopitishwa mbele ya macho yenu. Kazi yenu kubwa bungeni ni kusifia CCM.
Mlikubali kunyamazishwa na Lowassa mlipokuwa mnahoji ufisadi wa Richmond. Hivyo na nyinyi muwe tayari kujibu maswali ya wananchi je huko bungeni mnafanya nini chenye maslahi na nchi yetu?