Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,298
Mikataba ya madini inazidi kuchachafya wananchi, naona ndiyo kabisaa kumekuchwa tu...
Mkataba wa EPAs hauna maslahi kwa wananchi
Na Kizitto Noya
Gazeti la Mwananchi
HOFU ya ufisadi na ubovu wa mikataba katika sekta ya madini, vimewatisha viongozi wa dini za Kikristo na Kiislamu ambao sasa wameazimia kuishinikiza serikali kutosaini mkataba wa Mpango wa Makubaliano ya Kibiashara na Uchumi kati yake na nchi za Jumuiya ya Ulaya (EPAs).
Viongozi hao walifikia uamuzi huo jana katika hitimisho la warsha yao ya siku mbili ya mashauriano ya EPAs iliyoandaliwa na Kikundi cha Majadiliano cha Makanisa ya TEC na CCT (TEDG) na kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Baraza la Maaskofu Tanzania, jijini Dar es Salaam kwa siku mbili.
Wakizungumza katika warsha hiyo iliyoandaliwa kwa ajili ya kutathmini faida na hasara ya mkataba huo, viongozi hao walisema kama ilivyo kwa mikataba mingine, mkataba wa EPAs hautaisaidia Tanzania zaidi ya kuliongozea taifa umaskini.
Mpango wa EPAs unalenga kupunguza masharti ya kibiashara baina ya nchi zinazoendelea na za Jumuiya ya Ulaya kwa bidhaa zinazozalishwa katika nchi hizo.
Mratibu wa Shirika la Madeni na Maendeleo nchini (TCDD), Chamba Kejege, alisema kuwa mikataba mingi nchini imekuwa chanzo cha umaskini kwa kuwanufaisha wageni na kuwasahau wazawa.
Alisema pamoja na sababu nyingine, umaskini nchini umechangiwa na mikataba mibovu iliyosainiwa kuwanufaisha wageni na kikundi fulani cha watu badala ya wananchi wa kawaida.
Alisema Tanzania ni ya tatu barani Afrika kwa umaskini ambao kwa kiasi kikubwa unatokana na madeni haramu yaliyopatikana kwa hulka za baadhi ya watu kujiongezea utajiri.
"Wakati mwingine huwa tunaomba mikopo wakati hatuna ulazima na matokeo yake fedha hiyo zinaingia katika matumizi ambazo hayakuainishwa," alisema Kajege.
Alisema historia inaonyesha kuwa nchi za Ulaya hazijawahi kufanya biashara yenye lengo la kuzinufaisha nchi maskini na mpango wa EPA hauna maana yoyote zaidi ya kuendelea kuziibia nchi hizo.
Alisema Tanzania haina budi kuanza kujifunza kukuza uchumi kwa kudhibiti matumizi ya rasilimali zake, badala ya kutegemea mikopo na mikataba ambayo kwa kiasi kikubwa inaliongezea taifa umaskini.
Kwa mujibu wa Kajege ni hatari kwa Tanzania kuingia katika mpango wa EPA kwa kuwa masharti yake yameonekana dhahiri kutaka kuua soko la bidhaa za ndani na kupalilia soko la bidhaa za nje.
Mwakilishi wa Shirika la Misaada la Makanisa la Norway nchini, Fredrik Glad-Gjernes aliwataka viongozi wa dini kuwa mstari wa mbele kupinga mpango huo kwa kuwa nchi inaweza kujiendesha kwa rasilimali zake.
"Utasemaje kuna uwiano wa uhuru wa kibiashara wakati kuna masharti ya ubora wa bidhaa na mengine mengi?" alihoji.
Alidai kuwa mpango wa EPA ni maalum kwa ajili ya kuzinyonya nchi maskini kwani masharti yanayoambatana nao hayatoi fursa kwa nchi maskini kufanya biashara yenye uwiano kati yake na Ulaya.
Kwa mujibu wa mwakilishi huyo, Tanzania inapaswa kuacha tabia ya kukimblia mikataba bila kufanya tafiti za faida na hasara zake, kwani kufanya hivyo ni kulipeleka taifa pabaya.
Aliwataka viongozi wa dini kusimamia hatima ya nchi yao kwa kuishinikiza serikali isitishe mpango wake wa kusaini mkataba huo ufikapo Desemba 31 mwaka huu kwa maslahi ya wazawa.
Mkurugenzi wa Life Ministry Tanzania, Dismas Shekalaghe aliitaka serikali kupitisha sheria ya wabunge kushirikishwa katika kuidhinisha madeni ya nje ili kuziba mianya ya rushwa na ufisadi
Alisema moja ya sababu za umaskini nchini ni rushwa na ufisadi unaofumbiwa macho na wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi.
"Mimi nina mashaka na Bunge kwamba linachangia ufisadi kwa kuwakilisha maoni yao na matakwa ya vyama badala ya wananchi. Kwa nini lisishirikishwe katika kuidhinisha madeni ya nje ili kuziba mianya ya rushwa?" alihoji Shekalaghe.
Awali, Kajege alitaja sababu za bunge kushindwa kudhibiti mianya ya rushwa kuwa ni pamoja na tabia ya kulindana.
"Bunge lilitakiwa kuidhinisha madeni ya nje likiwawakilisha wananchi, lakini hapa nchini hili haliwezekani kwa sababu nyingi ikiwamo kulindana na takrima.
Alitaja tatizo lingine kuwa ni udhaifu wa katiba ya nchi ambayo mpaka sasa hairuhusu wananchi kuwafukuza kazi wabunge waliowachagua.
Askofu Dk Peter Mwamasika wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma alisema Tanzania haihitaji kuendelea kuwanufaisha watu wachache kwa kusaini mikataba isiyokuwa na tija kwa taifa.
Alibainisha kuwa umaskini wa Tanzania ni matokeo ya ufisadi na kubebana kwa baadhi ya viongozi katika kuendesha nchi.
Juzi mtaalam wa masuala ya mikataba ya biashara za Kimataifa, Profesa Francis Matambalya alisema katika mada zake kuwa mpango wa EPA ni hatari kwa kuwa hauruhusu ushindani wa kibiashara baina ya pande hizo mbili.
Alisema kimsingi Tanzania inatakiwa kuingia katika mpango huo baada ya kuwashirikisha wananchi wake na watalaam ili kubaini faida na hasara zake, kuondoa matatizo yasiyo ya lazima.
"Serikali peke yake haitoshi kuingia katika mkataba huo bila kuwashirikisha watalaam kuuchambua na kujua athari zake," alisema Matambalya.
SteveD.