Mikataba ya Madini na Serikali ya Tanzania

Mikataba ya Madini na Serikali ya Tanzania

siku zote alikuwa wapi huyu!? 😕

Mbunge wa CCM naye akerwa na wawekezaji katika migodi
* Awakoromea mbele ya Waziri Mkuu Lowassa

Na Mkinga Mkinga, Mara
Kutoka Gazeti la Mwananchi

Mbunge huyo aliwahi kususia makabidhiano ya Sh240 milioni kutoka kwa wawekezaji, akidai kuwa hataki kuona uchafu ukifanyika mbele yake kwa sababu hajui umiliki wa migodi hiyo pamoja na uliokuwa jimboni lake la Buhemba.

Sitaki kuona uchafu huo unafanyika mbele yangu. Maana hiyo mikataba mimi siijui, hata ule wa mgodi wa Buhemba, ambao uko jimboni kwangu sijui unamilikiwa na nani,? alinukuliwa Mkono wakati akisusia kushuhudia makabidhiano hayo kati ya Kampuni ya Barrick Gold Tanzania na halmashauri za wilaya ambako kuna migodi yake.

Nilipata kichefuchefu saba ninaposoma
Huyu Mkono ni mtu wa ajabu sana; msimamo wake kuhusu wawekezaji haueleweki na sijui kama hapa anafanya unafiki au ndiyo msimamo wake kweli kweli. Kumekuwa na tetesi zisizothibitishwa kuwa yeye alikuwa msitali wa mbele katika kutayarisha mikataba ile na hivyo kujipatia mapesa mengi sana. Makampuni mengi ya nje yaliyoingia Tanzania yameptia kwake, na kuna siku aliwahi kusema kuwa yeye ndiye aliuza MNB. Sasa imekuwaje? hata mimi sielewi, nadshani huu utakuwa unafiki tu.


Katika maneno yake hapo juu na hizi tetesi za Kichuguu; ni mtazamo wangu kuwa huenda kweli hata yeye ameachwa gizani.
 
Sasa kama unasikia unafiki basi ndiyo huu, na hii inadhihirisha ni kweli katika hoja ya Mb.Zitto Bunge lilikaa kama kamati ya chama cha mapinduzi(ccm). Sasa basi wabunge wa CCM si wazalendo na hanacho fanya mkono ni kujikomba kwa wananchi wake ili wamuone naye anapinga hii mikataba ya Madini yaani yuko upande wa zitto. kazi kweli kweli.
 
hivi huyu mkono naye vipi?siku zote alikuwa haoni haya?ama kweli viongozi wetu wasanii
 
Watalia sana mwaka huu wangoje 2025 ndio watakuwa wamejizatiti kiasi.

FD
 
Huyu mzee kibandiko hana jipya!
Kwani alikuwa wapi wakati hoja ya Zitto inatupwa? mbona hakusimama kutoa maoni yake make huo ndo ulikuwa muda muafaka! Mbona aliunga asilimia miamoja zitoafukuzwe?

Anataka umaarufu tu..
 
Pamoja na huo "unafiki" mnaouzungumzia bado nampongeza Mkono; angalau yeye amelisemea hilo na ameonyesha kutoridhishwa na Uwekezaji wa Madini na kwa jinsi hiyo ameonyesha kuwa ingawa Chama chake na serikali yake inawakingia kifua lakini "mimi simo" kwa hiyo ni juu yake EL kumeza au kutema! Message sent and delivered.

Kumbukeni ndani ya Bunge kuna kitu kinaitwa "nidhamu ya chama" na kuna Wabunge wa upinzani but akiwa nje ya Bunge Mkono is free from the so called nidhamu ya chama.
 
Ama anakasirikia hao walio wekeza jimboni kwakwe kwa vile hawakumpa tenda wakati wanaingia hiyo mikatba uchwara??

Mbona hao alio wasaidia yeye bado wanatunyonya lakini anaona sawa tu?

Nakubaliana nawewe kichuguu pengine ni unafiki, ama hasira ya kutopata tenda wakati wa kuingia mikataba hiyo!
 
Huu unafiki huu,unajua Nkono namfananisha na Tariq Aziz aliyekuwa wazxiri wa habari wa Sadam Hussein.Hakya nani Tanzania tuna hazina ya Wasanii.Mhh,Ingekua ile vita ni kati ya Tz vs Usa,basi tungeshinda maanake kwa hii hazina ya viongozi wanafiki,waongo,wapotoshaji na wapiga propaganda lazima askari wetu wangejawa na nguvu za ajabu kama za Samson lazima Usa angechapwa tu.Ila sasa wanavyo misuse vipaji vyao sisi tunaugulia tu maumivu huku.
SWALI SASA! Mhe.NKONO ulikua wapi siku ile Mzalendo Zitto akihujumiwa Bungeni?Kama umefunuliwa ukaona haya unayoyatamka sa hivi basi tangazia umma na utoe ushuhuda.Himma Himma!
 
Wanasheria wataka kuanzishwa daftari la kusajili mikataba

Na Mwandishi Wetu
Gazeti la Mwananchi

CHAMA cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) Tawi la Arusha kimeitaka serikali kuanzisha daftari maalum la kusajili mikataba yote inayohusu ubinafsishaji na uvunaji wa rasilimali za umma.

Hatua hiyo inafuatia makubaliano yaliyofikiwa na wanasheria 30 wanachama wa chama hicho mkoani Arusha, ikiwa ni hatua ya kujitolea kuisaidia serikali kuipitia mikataba yote yenye utat na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuiboresha ili ilinde maslahi ya Taifa kwa mujibu wa Katiba.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Mwenyekiti wa Chama hicho, Akoonay Sang'ka ni imani yao kwamba wanaohusika kwa namna yoyote kutia sahihi kwenye mikataba yenye utata hawana uwezo wa kuifanyia mapitio.

"Tunaamini kinyozi hajinyoi, pia mganga hajigangi, tunahitaji serikali ianzishe daftari hili kana ilivyo kwenye daftari la usajili wa hati za kumiliki ardhi ili mwananchi yeyote aweze kufanya upekuzi kwa lengo la kujiridhisha kuwa mikataba hiyo inalinda maslahi ya taifa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," alisema Sang'ka.

Aliongeza kuwa, kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano, vifungu vya 8, 9 na 27 vinaiwajibisha serikali kuweka wazi mikataba yote inayohusu ubinafsishaji wa mali za mashirika na taasisi zote za umma na kuweka wazi mikataba yote inayohusu uchimbaji wa madini na vito vya thamani na uvunaji wa aina yoyote wa maliasili ya nchi.

Sang'ka alisema lengo ni kuhakikisha kuwa, wananchi wanapata nafasi ya kujiridhisha iwapo mikataba hiyo inafuata masharti ya katiba ili kulinda maslahi ya taifa na si vinginevyo kwa kuwa madai ya mikataba hiyo kuwa ya siri ni ukiukaji wa wazi wa katiba ya nchi.
 
Tutaisaidia Serikali kupitia mikataba – Wanasheria

na Amana Nyembo
Tanzania Daima


WANASHERIA wa Tanganyika tawi la Arusha, wamedai kuwa, wapo tayari kuisaidia serikali kupitia mikataba yote yenye utata na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuiboresha ili kulinda maslahi ya taifa kwa mujibu wa katiba.
Hayo yalibainishwa jana katika taarifa iliyotolewa na Katibu wa chama cha wanasheria hao, Eliakunda Makange, kuhusu mikataba ya ubinafsishaji na uvunaji wa rasilimali za taifa, hususani madini.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa, katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, serikali inawajibika kuchukua hatua za kuweka wazi mikataba inayohusu ubinafsishaji wa mali za mashirika na taasisi za umma na mikataba inayohusu uchimbaji wa madini na vito vya thamani na uvunaji wa aina yoyote ya maliasili ya nchi.

Ilifafanua kuwa, kuwekwa wazi kwa mikataba hiyo, lengo ni kuwawezesha wananchi kujiridhisha iwapo inakidhi masharti ya katiba na kulinda maslahi ya taifa, badala ya usiri uliopo sasa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ni jukumu la chama cha wanasheria hao kutetea na kuisaidia jamii juu ya masuala yanayogusa sheria na kutekeleza wajibu chini ya kifungu 3(e).

Aidha, waliielekeza serikali na wananchi kuwa, vifungu vya nane, tisa na 27 vya Katiba ya Muungano, vinatamka kuwa Tanzania ni nchi inayofuata misingi na demokrasia na haki ya kijamii, kwa hiyo serikali itawajibika kwa wananchi.

Taarifa hiyo, ilieleza lengo la katiba hiyo ni kuwezesha ujenzi wa Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, au chochote kati ya vyombo vyake, na kufuata siasa ya ujamaa na kujitegemea, inayosisitiza utekelezaji wa misingi ya kijamaa kwa kuzingatia mazingira.

Iliendelea kudai kuwa, shughuli za serikali zinatekelezwa kwa kuhakikisha kuwa utajiri wa taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi, na kuzuia mtu mmoja kumnyonya mwingine.

“Matumizi ya utajiri wa taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi hasa yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondoa umaskini, ujinga na maradhi…

“Kila mtu ana wajibu wa kulinda maliasili ya Jamhuri ya Muungano, mali ya mamlaka ya nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, pia kuheshimu mali ya mtu mwingine,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Ilieleza kuwa waliohusika kwa namna moja au nyingine katika kutia sahihi mikataba yenye utata hawana uwezo wala uhalali wa kuifanyia mapitio mikataba hiyo.

Hata hivyo, waliitaka serikali kuanzisha daftari maalum la kusajili mikataba yote inayohusu ubinafsishaji na uvunaji wa rasilimali za umma, ili mwananchi afanye upekuzi kwa lengo la kujiridhisha kuwa mikataba hiyo inalinda maslahi ya taifa kwa mujibu wa katiba.
 
...tatizo la mikataba yetu siyo la Kisheria ni la KIUCHUMI. Wachumi wetu wamekuwa wakipiga mahesabu famba ktk hiyo mikataba. Wachumi wetu wameshindwa ku-burgain for the benefit of mother Tanzania.
 
Tutaisaidia Serikali kupitia mikataba – Wanasheria

Ni jambo la heri,
ningependa kufahamishwa zaidi haya walitamka katika mazingira gani? kwenye warsha au walienda kuhojiwa na mwandishi? au ni wao walitoa tamko?
 
Hatuwataki nyie, tutaomba wataalamu wa mikataba kutoka Norway.
 
Kama wanasheria wenyewe ndio hawa malimbukeni tuliona nao mjini kama kina.....na makuwadi wa unyang'au kama kina Mkono ni bora tukaendelea na hawahawa majini watujuawo......

Kwanza tuna ushahid wa kutosha kuwa ni hawahawa ndio walotumika kuwafix watanzania katika hiyo mikataba yao kwa vijisenti na vibenzi uchwala vya kupigia mtama vigori wetu...

Tanzanianjema
 
Kama wanasheria wenyewe ndio hawa malimbukeni tuliona nao mjini kama kina.....na makuwadi wa unyang'au kama kina Mkono ni bora tukaendelea na hawahawa majini watujuawo......

Kwanza tuna ushahid wa kutosha kuwa ni hawahawa ndio walotumika kuwafix watanzania katika hiyo mikataba yao kwa vijisenti na vibenzi uchwala vya kupigia mtama vigori wetu...

Tanzanianjema
Uko right,

Mkono ni mwanasheria anayesifika sana. lakini ndiye aliyetumika kwa kiwango kikubwa sana katika kuiingiza serikali mkenge. Sidhani kama kweli wanasheria wa nchi zilizoendelea wanaweza kuwasaidia wateja wao kuhujumu serikali zao, ingawa wana uhuru mwingi.
 
Mimi naona tatizo ni kukosa wanasheria na wachumi wenye uzoefu na uelewa mkubwa kukadiria vizuri mategemeo ya matokeo, faida ama madhara ya mikataba ya kiuchumi wanayoiingiza nchi hasa kwa kuwiana na sheria za kibiashara za kimataifa na pia kutowaelewa vema hao tufanyao nao biashara. Dawa ni kujifunza na kurekebisha wakati tunasonga mbele maana kwa karne nne tumekua kwenye giza katika ubepari. Pia CCM wamekwama kwa muda mrefu bila kuleta maendeleo kwa watu na sasa wanaona hakuna muda wa kusubiri tena, kama jadi yao wanakurupuka bila kupanga vizuri na kutuingiza kwenye hiyo mikataba duni, naamini mikataba mingine si rushwa bali ni ujinga mwingi wa viongozi wetu.
 
Mimi naona tatizo ni kukosa wanasheria na wachumi wenye uzoefu na uelewa mkubwa kukadiria vizuri mategemeo ya matokeo, faida ama madhara ya mikataba ya kiuchumi wanayoiingiza nchi hasa kwa kuwiana na sheria za kibiashara za kimataifa na pia kutowaelewa vema hao tufanyao nao biashara. Dawa ni kujifunza na kurekebisha wakati tunasonga mbele maana kwa karne nne tumekua kwenye giza katika ubepari. Pia CCM wamekwama kwa muda mrefu bila kuleta maendeleo kwa watu na sasa wanaona hakuna muda wa kusubiri tena, kama jadi yao wanakurupuka bila kupanga vizuri na kutuingiza kwenye hiyo mikataba duni, naamini mikataba mingine si rushwa bali ni ujinga mwingi wa viongozi wetu.

Mimi siwezi kuwalaumu wataalam wetu, tuna wataalam wazuri sana, tatizo ni kwamba serikali yetu haiko tayari kuwatumia hao wataalam wetu ipasavyo na badala yake wanawaagiza wafanye kile ambacho viongozi wetu wanataka. Wataalam hao kutokana na njaa zao wameishia kukubali kutekeleza wanayoagizwa na viongozi wao na hawana ujasiri wa kujiuzulu na hivyo inabidi wakae kuganga njaa, matokeo yake rais anakuja kuwatukana kwamba anahitaji wataalam kutoka Norway kwa kuwa wataalam wetu hawana ujuzi wa ku-bargain.

Kwanini tunaona watalaam kutoka nje wanafaa sana? Ni kwamba wakija kufanya kazi viongozi wa serikali hawawaingilii na pia wana power zaidi ya kusema NO pale wanapoona wameingiliwa. Lakini wataalam wetu wa ndani ndiyo kama akina Hosea, DG wa PCCB ambaye pamoja na kudai kwamba PCCB iko independent, lakini bado anasema JK ni Boss wake na hivyo kile anachosema JK ndiyo final na akifanya kinyume na maagizo ya JK ni kama vile anakiuka maagizo ya Boss. Hali hiyo ndiyo inayowakumba wengi wa hao watalaam wetu ambao tunawalaumu kila siku kwamba wameshindwa kufanya kazi zao na wanaposhiriki kuandaa mikataba wanaiandaa ikiwa mibovu kwa maelekezo kutoka juu na hawana ujasiri wa kusema NO!
 
Hatuwataki nyie, tutaomba wataalamu wa mikataba kutoka Norway.

haya yalikuwa ni matusi ya nguoni, sikutarajia kauli kama hiyo kutoka kwa Rais wa nchi, aliwadhalilisha wataalam wote wa Tanzania. maana shule walizosoma hao wa Norway na masomo ni yale yale, kwanini wao wawe na uwezo wa ku-bargain na wa kwetu washindwe? wapeni uhuru wachape kazi muone kama watawapa mikataba mibovu. mikataba mibovu ni matokeo ya njaa na kuwaingilia sana watalam wetu!
 
Back
Top Bottom