Mikael P Aweda kuishambulia TBC kupita ITV. Maoni yangu.

Mpaka sasa bado sijaelewa nia kamili ya mleta hoja..maana imekaa kiushabiki na uzandiki zaidi
 
Naona argument yako imebebwa na maneno kwamba "hahitaji kuitumia tbc siku nyingine?!" na "hapaswi kuingilia hoja zisizomhusu!"

Bora yeye kasema mtazamo anaouamini kuliko unafiki wako wa kutaka kufichaficha mambo kwa kuwa eti atahitaji kuitumia TBC wakat ujao labda?!

Huu uzi umeonesha madhaifu yako kuliko ya huyo unayemlaumu!
 
Acha wivu wa kike we magamba. Astaghafrulah laana tu lah. Ngoja niondoke maana naona mods wanataka kubonyeza kitufe cha ban
 
Jana nilimsikiliza vizuri sana Aweda kwenye Malumbano ya hoja. Alizungumza vizuri sana kuliko wazungumzaji walio wengi. Lakini point yake ya pili kwa maoni yangu alipotea ramani kabisa na kujiharibia mwenyewe kabisa. Si sahihi yeye kuisifia ITV ambayo inamwalika karibu kila wiki mara malumbano ya hoja, mara kipima joto mara vipindi vipindi vingine halafu akapata ujasiri wa kitoto wa kuishambulia TBC kuwa ni kipeperushi cha baadhi ya vyama. Nina uhakika alikuwa analenga TBC japokuwa hajaitaja kwa jina. Ina maanisha kwamba Aweda hahitaji kutumia TBC hata siku moja? Je, kwa kuwa Mbowe na kamati kuu wamesema yeye ilikuwa inamhusu nini kuingia kwenye hoja ambazo hazimsaidii.
Kwa kweli, nilikuwa namheshimu sana Aweda kwenye mitandao na ktk vipindi vya ITV ambavyo mimi nimtazamaji mzuri lakini jana nilimwonea kama mwanampotevu.
Mwisho, Aweda nakushauri, najua JF unakuja kwa mara na thread yangu utaisoma, achana utoto. Vinginevyo siasa zitakushinda mapema kabisa mdogo wangu.
Mods msifute mada yangu, kwa sababu mimi sijui kama Mikael P Aweda huyo ni wa JF au La.


Hayo ni maoni yako na yeye alikuwa anatumia uhuru wake wa kutoa maoni, au kuunga mkono maoni ya wengine kuhusu hiyo TV station. Mathalani hizo ambazo mara nyingi zimekuwa hazielezi ukweli, au kutumiwa kipropaganda. sasa ulitaka asifie hata kama wanaboronga, au ulitaka akesemee wapi ambako wewe unafikiri ni muafaka?
 
nafikiri nikuache ukikua utajua namaanisha nini. uliza wakongwe wa hili jamvi huyu gfsonwin ni chama gani? utajua usikurupuke tu kudandia treni kwa mbele. sina imani na Aweda full stop. wala msikaririshe watu kwamba chadema ndo chama chenye watu safi kuliko vyama vingine allah! tatizo wanachadema wengi mnatawaliwa na jazba kuliko kuangalia facts. na kamwe hamtashika madaraka kwa stail hii. mnafanya jamvi kuwa mali ya cdm tu akisema mtu mwingine kosa mkikosolewa kosa nyie nani hadi mtutishe ama tuwaogope? mmefanya nini cha ajabu sana ambacho kitatushawishi hata kuwafikiria? ama huko kupiga kelele na kusababisha vifo vya wenzenu? tena natamani kweli nikufahamu vizuri ama ulete ID yako nyingine hapa.

Dadangu gfsonwin naona unataka kuvuka mipaka na kujivika uwezo wa kinabii kama si unajimu.
Mwenyezi Mungu akiamua kwamba Chadema isishike madaraka ya nchi hii itawezekana kwakuwa yeye ndiye muweza wa yote. Lakini hizi personal vendata zinavyokufanya ukishambulie chama chote badala ya kudeal na huyo mtu anayekukera na kukutia jazba inakuwa ni kujishushia heshima yako ambayo naamini heshima yako ni kubwa zaidi ya hapo unapotaka kujielekeza.

Kama unampinga Aweda mpinge kwa facts na si maneno makavu.
Kama unakiri kwamba wewe ni mkongwe hapa JF ulitakiwa kufahamu kwamba Aweda alishahama siku nyingi huko kwenu kwembe na sasahivi yupo Ukonga na ndiye mwenyekiti wa Chadema jimbo la Ukonga. Na suala la yeye kuhamia Ukonga lilikuwa wazi sana kiasi kwamba hata hapa JF zilianzishiwa thread kadhaa za kuzungumzia kuhama kwake toka wilaya ya kinondoni kwenda Ukonga.

Ushauri wangu wa bure kwako kama una tatizo kubwa sana na Mikael P Aweda na umeshindwa kumpata ili kumweleza dukuduku lako, naomba tuwasiliane nikupe mawasiliano yake, ama nikukutanishe naye ili useme lililo moyoni mwako. Ama la ukiona hiyo si njiia muafaka unaweza kuanzisha thread ya malalamiko yako na mimi nitamtafuta huko aliko aje hapa kujibu hoja zako.
 
Last edited by a moderator:
Wewe imekuuma nini yeye kueleza yaliyo moyoni mwake? Una hisa TBCCM? Hakuna channel ya hovyo kwa habari kama hiyo TBCCM unayotaka tuamini kwamba haikutendewa haki. TBC ilianzishwa kama television ya taifa lakini kwa sasa ni ukweli usio na kificho kuwa imehodhiwa na ccm ijapokuwa inaendeshwa kwa kodi za watanzania wote. Huu ni ufisadi, kwa hiyo yeyote anayetetea ufisadi ni fisadi kama ulivyo wewe.
 
Tanzania tumelelewa katika mfumo wa uwoga waoga
kuna watu hadi leo ukisema ukikosoa kitu watakuona msaliti au mtovu wa nidhani
kuna watu wao wanadhani kila mtu lazima asifie kila kitu kinachofanywa na viongozi wetu au media zetu
kuna watu kwa vile wananufaika na utawala uliopo kwao ni dhambi kuwakosoa
nampongeza Michael kwa kutokuwa mnafiki
na ili kukososa mfumo fulani lazima utumie media ili kuwafikia wengi
TBC imeshakufa na kuoza siku nyingi sana machoni pa wengi
inatumia kodi zetu vibaya kwa manufaa ya chama tawala ukweli uko wazi
haina balance katika habari zake.sio muda wa kunyamaza tena ni muda wa kuisema
ingekuwa nchi za wenzetu wangeshaichoma moto siku nyingi sana mitambo yake
tusiwe wanafiki kwa hili.TBC is no more in peoples mind.
RIP TBC
 
Huna imani na siasa zake kwakuwa hamjalipwa fidia ama unakusudia kusema nini gfsonwin?
Aweda sasahivi ana majukumu makubwa sana anayotekeleza ndani ya chama na kwakuwa mnaye diwani mliyemchagua kama bado hamjalipwa fidia basi mlitakiwa kumbana yeye awaeleze kinachoendelea badala ya kutafuta kumtoa kafara mtu mwingine asiyekuwa na mandate kwa wakati huu.

btw, kama ninyi wa kwembe hamna imani nae kama ambavyo mlionyesha uchaguzi mkuu uliopita, basi mtambue kwamba sisi wa Ukonga tuna imani nae!
Kuhusu uchambuzi wa masuala mbali mbali yanayokabili Taifa letu Aweda ni level nyingine,as a matter of fact this guy need a clap for yesterday topic,
 
Huna imani na siasa zake kwakuwa hamjalipwa fidia ama unakusudia kusema nini gfsonwin?
Aweda sasahivi ana majukumu makubwa sana anayotekeleza ndani ya chama na kwakuwa mnaye diwani mliyemchagua kama bado hamjalipwa fidia basi mlitakiwa kumbana yeye awaeleze kinachoendelea badala ya kutafuta kumtoa kafara mtu mwingine asiyekuwa na mandate kwa wakati huu.

btw, kama ninyi wa kwembe hamna imani nae kama ambavyo mlionyesha uchaguzi mkuu uliopita, basi mtambue kwamba sisi wa Ukonga tuna imani nae!
Kuhusu uchambuzi wa masuala mbali mbali yanayokabili Taifa letu Aweda ni level nyingine,as a matter of fact this guy need a clap of hand for yesterday topic,
 
Hebu nisaidie hii, kama unajua Kiswahili.......... Ikiwa hii 11,000 =ni shs elfu kumi na moja. Jee, hii 10,001 = na ngapi? Nisaidie ndugu yangu.


Mkuu mi nadhani itakuwa hivi
11,000/= sawa sawa na elfu kumi na moja.
10,001/= ni kumi elfu na moja,,,

kwa kheri!
 
politics politics politics u kill tanzanian, lakini wenyewe hawajui masikini wengine wamesoma phd, masters, degree lakini mmmhhhhh, lets change now guys!!! its a bomb.
A%20S%20465.gif
A%20S%20465.gif
A%20S%20465.gif
A%20S%20465.gif
A%20S%20465.gif
A%20S%20465.gif
A%20S%20465.gif
A%20S%20465.gif
A%20S%20465.gif
A%20S%20465.gif
 
Mwisho, Aweda nakushauri, najua JF unakuja kwa mara na thread yangu utaisoma, achana utoto. Vinginevyo siasa zitakushinda mapema kabisa mdogo wangu.
Mods msifute mada yangu, kwa sababu mimi sijui kama Mikael P Aweda huyo ni wa JF au La.

Kwahiyo angeisifia TBC angekuwa anafanya mambo ya kiutu uzima?
 
Kama Great Thinker, hukutakiwa kuwa na jaziba juu yake iwapo umethibitisha pasi kuacha shaka kuwa hauitaja kwa jina kuwa ni TBC. Hivyo hisia zako ndo zilikupelekea kufikiri hivyo. Kwa ushauri wangu jipange upya, ondoa jaziba na umwombe msamaha then toa allegations zako juu yake ili aweze kukujibu. Vinginevyo hapo jibu lake ni dogo na ni moja tu "Sikutaja TBC"
na hata kama aliitaja tatizo liko wapi?? mleta mada ana maprobulemu aisee,
 
Sawa, nani kamtuma yeye kuishambulia TBCCM?
Na wewe nani kakutuma kumshambulia Aweda? Aweda ni mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema na mara nyingi anaalikwa ITV kama kiongozi wa Chadema na jana aliongea kama Kiongozi wa Chadema. Unaposema anafuata tamko la Mbowe unaonyesha upungufu mkubwa na ushabiki uliopitiliza. Hakuna tamko la Mbowe bali tamko la Chadema kutoka Kamati kuu lililosomwa na Mwenyekiti. Unapjaribu kuisaficha TBC ndio unazidi kuichafua zaidi. Kama wewe unafanya kazi TBC au una maslahi nayo ujue kuwa unalipwa kwa kupitia kodi ya Aweda, Mbowe, Mengi na wengineo lakini mtangazi wa ITV hatumii kodi yako wewe NAMI.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom