Mikael P Aweda kuishambulia TBC kupita ITV. Maoni yangu.

Mwambie Aweda akaitaje alhamisi ijayo, tutamfungia na hiyo ITV yake.
Aah kauli gani hiyo mimi nilidhani tunaongea na mtu mwenye akili, kumbe ndivyo ulivyo ndiyo maana thread imejaa makengeza!
 
mwambie aweda akaitaje alhamisi ijayo, tutamfungia na hiyo itv yake.

mkuu mwambieni yule mtangazaji wenu anaeogopa kuongea wakati wamijadala yake!
Mpelekeni ajifunze kuacha wooga wake!
 
Insensitivity nalo ni gonjwa. Kwani wewe mleta mada una maoni gani kuhusu TBC 1? Hasa kama chombo cha umma na jinsi kinavyotumiwa.
 
mbona kama ni mpembuzi wa mambo utagundua kuna uchama umeingia kwenye huu uzi. BTW AWEDA aligombea udiwani kata ya Kwembe ingawa alikosa lkn alitupa matumain ya kutusaidia ili tuweze kulipwa fidia nzuri kupisha upanuzi wa mji wa DSM lkn hadi leo hatumuoni tunaishia kumwona kwenye ITV. sina imani na siasa zake hata kidogo.

Huna imani na siasa zake kwakuwa hamjalipwa fidia ama unakusudia kusema nini gfsonwin?
Aweda sasahivi ana majukumu makubwa sana anayotekeleza ndani ya chama na kwakuwa mnaye diwani mliyemchagua kama bado hamjalipwa fidia basi mlitakiwa kumbana yeye awaeleze kinachoendelea badala ya kutafuta kumtoa kafara mtu mwingine asiyekuwa na mandate kwa wakati huu.

btw, kama ninyi wa kwembe hamna imani nae kama ambavyo mlionyesha uchaguzi mkuu uliopita, basi mtambue kwamba sisi wa Ukonga tuna imani nae!
 
Last edited by a moderator:
Jimbo hawezi. Utaendesha jimbo kwa kwa kutoa tuhuma za Uwongo. Labda akatafute kata ya kuongoza kama diwani tena Mbulu siyo Dsm na Dr Slaa akampigie Kampeni. Mbulu si inapakana Karatu? Tena nasikia wanaongea lugha Lugha moja. Jimbo hapana.

Utake usitake jimbo atapata. tena yeye ni sawa na magamba kumi mjengoni. Iwe kwao manyara au ukonga tunampa.
hujawaona jana alivyowafunika magamba zaidi ya 10 waliokuwa wanasema waandishi wa habari wako salama? Mbona waliishia kumpigia makofi?
 
mbona kama ni mpembuzi wa mambo utagundua kuna uchama umeingia kwenye huu uzi. BTW AWEDA aligombea udiwani kata ya Kwembe ingawa alikosa lkn alitupa matumain ya kutusaidia ili tuweze kulipwa fidia nzuri kupisha upanuzi wa mji wa DSM lkn hadi leo hatumuoni tunaishia kumwona kwenye ITV. sina imani na siasa zake hata kidogo.

Sasa huyu si aliaga ubungo akaenda ukonga tena kulikuwa na thread nyingi hapa JF? Sasa unataka awatumikie Kwembe kutoka ukonga? ina maana huko kwenu tena jimbo la mnyika hakuna wengine. wewe nawe hueleweki.kwa hiyo unakubali aweda jembe siyo? habari za kuamka usingizini.
 
Mimi namlaumu huyo Awade kwa kutoitaja jina tbccm kipeperushi cha ccm! Huyu mleta mada ndio amepotea njia kwa kuandika vitu vilivyo wazi
 
Sasa huyu si aliaga ubungo akaenda ukonga tena kulikuwa na thread nyingi hapa JF? Sasa unataka awatumikie Kwembe kutoka ukonga? ina maana huko kwenu tena jimbo la mnyika hakuna wengine. wewe nawe hueleweki.kwa hiyo unakubali aweda jembe siyo? habari za kuamka usingizini.

nafikiri kuna usilolijua ama jina lake lipo mara mbili? aliyepita kukusanya michango ya wasimamizi wa kuhesabu kura huku kwembe ni nani? na aliyegombea udiwani kata ya kwenbe ni yupi?
 
Huu utetezi wenu wa kizamani na vile vimakofi walivyokuwa wanampigia wapambe mle ndani ndo mnazidi kumfanya ajione amefanya sawa. Kwani kuna TV gani nyingine imedaiwa kuibeba chama zaidi ya TBC?

Kaeleza hisia zake ambazo zinaweza kuwa za kweli au laa,nadhani ingekua vizuri kama umebaini alikua ameilenga TBC ukafanya udukuzi kidogo wa mda mfupi ukaja na data zinazomprove wrong na alichokisema tofauti na hivo mtakuwa na lenu jambo kati yako na Aweda ambalo sisi hatulijui na wala hatutahitaji kulijua
 
TBC ni ****!
Jimbo hawezi. Utaendesha jimbo kwa kwa kutoa tuhuma za Uwongo. Labda akatafute kata ya kuongoza kama diwani tena Mbulu siyo Dsm na Dr Slaa akampigie Kampeni. Mbulu si inapakana Karatu? Tena nasikia wanaongea lugha Lugha moja. Jimbo hapana.
 
Jana nilimsikiliza vizuri sana Aweda kwenye Malumbano ya hoja. Alizungumza vizuri sana kuliko wazungumzaji walio wengi. Lakini point yake ya pili kwa maoni yangu alipotea ramani kabisa na kujiharibia mwenyewe kabisa. Si sahihi yeye kuisifia ITV ambayo inamwalika karibu kila wiki mara malumbano ya hoja, mara kipima joto mara vipindi vipindi vingine halafu akapata ujasiri wa kitoto wa kuishambulia TBC kuwa ni kipeperushi cha baadhi ya vyama. Nina uhakika alikuwa analenga TBC japokuwa hajaitaja kwa jina. Ina maanisha kwamba Aweda hahitaji kutumia TBC hata siku moja? Je, kwa kuwa Mbowe na kamati kuu wamesema yeye ilikuwa inamhusu nini kuingia kwenye hoja ambazo hazimsaidii.
Kwa kweli, nilikuwa namheshimu sana Aweda kwenye mitandao na ktk vipindi vya ITV ambavyo mimi nimtazamaji mzuri lakini jana nilimwonea kama mwanampotevu.
Mwisho, Aweda nakushauri, najua JF unakuja kwa mara na thread yangu utaisoma, achana utoto. Vinginevyo siasa zitakushinda mapema kabisa mdogo wangu.
Mods msifute mada yangu, kwa sababu mimi sijui kama Mikael P Aweda huyo ni wa JF au La.

Kiuhalisia wewe ndiye umeitaja TBC na kama ni kufunguliwa Mashtaka wewe ndiye ungeburuzwa kortini na si Aweda. Wewe umejuaje Aweda alikuwa anailenga TBC? What if likuwa anailenga Channel Ten, Star TV au Clouds TV? Kitendo cha wewe kupata jibu la moja kwa moja kwamba, Aweda aliilenga TBC basi inathibitisha kweli TBC ni kipeperushi cha moja ya vyama vya Siasa na wewe unalijua hilo fika.

Aweda alikuwa na uhuru wa kuisifia ITV maana ukiacha ukweli kwamba imekuwa ikimualika kwenye vipindi vyake kwa vyovyote vile objectivity yake haiwezi kulinganishwa na TBC.
 
Mleta uzi jifunze kuelewa kisemwacho na acha kuweka maneno yako mdomoni mwa mtu mwingine, sasa kama wewe hukusikia akitaja TBC, wewe unapata kiherehere cha nini kwa kuusemea moyo wa mwenzio!? huo ni uzandiki unaotokana na utapiamlo wa fikra! unajua alikuwa anamaanisha nini au ana lengo gani kwa kutotaja! na kwa nini ulazimishe iwe TBC tu! kwani hakuna TV stations nyingine zaidi ya TBC na ITV? na kama kwa mtazamo wako unaona TBC ndio inafanana na sifa alizotaja Aweda, ni nini basi ambacho hujaelewa au unachopinga? if you are not a low thinker what worse than that are you?
 
nafikiri kuna usilolijua ama jina lake lipo mara mbili? aliyepita kukusanya michango ya wasimamizi wa kuhesabu kura huku kwembe ni nani? na aliyegombea udiwani kata ya kwenbe ni yupi?
Wewe nawe gamba. unataka kutubadishia mada na kuleta vitu visivyoeleweka. Mimi niko kwembe hata sikuelewi unachoongea na nilikuwa wakala central pia. Aweda ndo alikuwa awe Diwani wetu. Huyo mama yenu si aliuza nyumba na kiwanja akahonga kwembe, msakuzi, mji mpya na kwembe shuleni. Kote huko alihonga. Aweda alikuwa na gari lake na sera tu. Au unataka tupasue jipu kuwa hata mtendaji wa kata naye alihongwa akachakachua kama walivyofanya mbezi, kibamba, goba nk? Kama siyo uchakachuaji meya ndo angekuwa wetu. Au hujui kuwa ccm walichakachua matokeo ya ubunge majimbo zaidi ya 50.
Hoja ni Aweda kuitaja TBCCM kuwa kipeperushi cha ccm. Wewe unakubali au unakataa? Usilete umagamba hapa.
 
Hebu nisaidie hii, kama unajua Kiswahili.......... Ikiwa hii 11,000 =ni shs elfu kumi na moja. Jee, hii 10,001 = na ngapi? Nisaidie ndugu yangu.
Kiswahili kama wanavyokifahamu wengi ni lugha inayobadilika kila siku.
Kwa vijana wa kileo watakuambia BEI gani?
Hata hivyo kujibu swali lako
Shs 11,000 ni elfu kumi na moja
Shs 10,001 ni elfu kumi na shilingi moja
Upo hapo .
 
Jimbo hawezi. Utaendesha jimbo kwa kwa kutoa tuhuma za Uwongo. Labda akatafute kata ya kuongoza kama diwani tena Mbulu siyo Dsm na Dr Slaa akampigie Kampeni. Mbulu si inapakana Karatu? Tena nasikia wanaongea lugha Lugha moja. Jimbo hapana.

Anaweza kabisa bana. Mbona hata lusinde ni Mbunge? Na mwigulu Je?
 
Wewe nawe gamba. unataka kutubadishia mada na kuleta vitu visivyoeleweka. Mimi niko kwembe hata sikuelewi unachoongea na nilikuwa wakala central pia. Aweda ndo alikuwa awe Diwani wetu. Huyo mama yenu si aliuza nyumba na kiwanja akahonga kwembe, msakuzi, mji mpya na kwembe shuleni. Kote huko alihonga. Aweda alikuwa na gari lake na sera tu. Au unataka tupasue jipu kuwa hata mtendaji wa kata naye alihongwa akachakachua kama walivyofanya mbezi, kibamba, goba nk? Kama siyo uchakachuaji meya ndo angekuwa wetu. Au hujui kuwa ccm walichakachua matokeo ya ubunge majimbo zaidi ya 50.
Hoja ni Aweda kuitaja TBCCM kuwa kipeperushi cha ccm. Wewe unakubali au unakataa? Usilete umagamba hapa.
nafikiri nikuache ukikua utajua namaanisha nini. uliza wakongwe wa hili jamvi huyu gfsonwin ni chama gani? utajua usikurupuke tu kudandia treni kwa mbele. sina imani na Aweda full stop. wala msikaririshe watu kwamba chadema ndo chama chenye watu safi kuliko vyama vingine allah! tatizo wanachadema wengi mnatawaliwa na jazba kuliko kuangalia facts. na kamwe hamtashika madaraka kwa stail hii. mnafanya jamvi kuwa mali ya cdm tu akisema mtu mwingine kosa mkikosolewa kosa nyie nani hadi mtutishe ama tuwaogope? mmefanya nini cha ajabu sana ambacho kitatushawishi hata kuwafikiria? ama huko kupiga kelele na kusababisha vifo vya wenzenu? tena natamani kweli nikufahamu vizuri ama ulete ID yako nyingine hapa.
 
Utake usitake jimbo atapata. tena yeye ni sawa na magamba kumi mjengoni. Iwe kwao manyara au ukonga tunampa.
hujawaona jana alivyowafunika magamba zaidi ya 10 waliokuwa wanasema waandishi wa habari wako salama? Mbona waliishia kumpigia makofi?

Huyo anayesema jimbo hapati ni gamba, mwambie 2015 ameze wembe maana Dr Slaa akiingia ikulu hawa wenye ujasiri kama akina Aweda ndo tunawataka mjengoni. Na kura haitaibiwa tena
 
Jana nilimsikiliza vizuri sana Aweda kwenye Malumbano ya hoja. Alizungumza vizuri sana kuliko wazungumzaji walio wengi. Lakini point yake ya pili kwa maoni yangu alipotea ramani kabisa na kujiharibia mwenyewe kabisa. Si sahihi yeye kuisifia ITV ambayo inamwalika karibu kila wiki mara malumbano ya hoja, mara kipima joto mara vipindi vipindi vingine halafu akapata ujasiri wa kitoto wa kuishambulia TBC kuwa ni kipeperushi cha baadhi ya vyama. Nina uhakika alikuwa analenga TBC japokuwa hajaitaja kwa jina. Ina maanisha kwamba Aweda hahitaji kutumia TBC hata siku moja? Je, kwa kuwa Mbowe na kamati kuu wamesema yeye ilikuwa inamhusu nini kuingia kwenye hoja ambazo hazimsaidii.
Kwa kweli, nilikuwa namheshimu sana Aweda kwenye mitandao na ktk vipindi vya ITV ambavyo mimi nimtazamaji mzuri lakini jana nilimwonea kama mwanampotevu.
Mwisho, Aweda nakushauri, najua JF unakuja kwa mara na thread yangu utaisoma, achana utoto. Vinginevyo siasa zitakushinda mapema kabisa mdogo wangu.
Mods msifute mada yangu, kwa sababu mimi sijui kama Mikael P Aweda huyo ni wa JF au La.

huvuti bangi kweli wewe?
 
Back
Top Bottom