Uchaguzi 2020 Hongera sana ITV, lakini TBC na Vyombo vingine vinadhulumu historia ya Taifa hili

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,486
51,063
Kila siku ipitayo kwa Mungu historia mpya ya nchi hii inaandikwa. Historia hii ina jambo la kijifunza ili kusaidia kujenga taifa kutokana na experience inayopata.

Napenda kuchukua nafasi hii kama Mtanzania kuwasifu na kuwashukuru ITV kwa kutuandalia mahojiano muhimu sana na mazuri sana ya Mh Tundu Lissu. Sisi tuliokuwepo nchini Tangu Marehemu mzee Mengi anaweka ITV nchini tunaweza kusema kuwa tukio hili limenikumbusha ujasiri wa mzee Mengi na kazi njema kabisa aliyoifanya kuhakikisha anahabarisha, anaelimisha na anaburudisha Taifa hili.

ITV ndiyo iliyotuonesha mpira LIVE kombe la dunia mwaka 1994, ndiyo iliyotiburudisha kwa tamthilia nzuri za Tausi, Isidingo n. k, vichekesho vya Max na Zembwela, Vichekesho vya Bishanga Bashaija, Swebe, Muhogo Mchungu. ITV iliibua vipindi vyenye kuibua fikra chanya kwa wananchi vya malumbano ya hoja.

Kwahiyo sisi tunaijua ITV na standard za juu katika kuwatumikia wananchi. Hizi standard zilikuwa zimeanza kushuka kwa kiwango kikubwa hasa kipindi cha utawala wa awamu ya tano, ambapo ITV nayo ilianza kuogopaogopa kutengeneza maudhui hata kama ni mazuri, ya halali yenye manufaa just kwa sababu ya kuogopa rungu la Serikali ya Magufuli.

Hata hivyo nawapongeza sana ITV kwa kutuletea mahojiano murua kabisa na mheshimiwa Lissu. Huyu ni mtu aliyepaswa kupata interview nyingi sana kwa sababu ni hot figure kwa sasa, huwezi kumuignore, kumuignore Lissu ni dalili za uandishi wa habari kanjanja.

Nawataka ITV wasiishie kufanya Interview tu, bali warushe na kampeni za Wagombea kama walivyofanya mwaka 2015.

Kwa upande wa vyombo vingine hususan TBC, hii TV inalidhulumu Taifa. Kitendo cha kufanya hujuma kwenye mkutano wa chama kikuu cha upinzani nchini kinalinyima Taifa uwezo wa kufahamu upande wa pili wa mawazo mbadala katika maono ya kuendesha nchi.

Hebu fikiria, Kama TBC itakataa kuchukua matukio ya uchaguzi mkuu huu ya mgombea mwenye nguvu dhidi ya mtawala wa sasa, kizazi kijacho kitapata wapi rejea nzuri ili kupata kujua chama kikuu cha upinzani kilikuwa na maono gani, mgombea wao alikuwa na sera gani? Watafiti wa kizazi kijacho watahitaji data, lakini hazitopatikana vizuri kwa sababu TBC kwa sababu ya kutaka kuwa TV ya CCM watakuwa hawana kwenye archive zao data za kutosha za chama kikuu cha upinzani nchini na mgombea wao yaani Tundu Antipass Lissu.

Leo hii ukienda kwenye archives za library of congress huko Marekani unakutana na taarifa za kutosha juu ya historia za Marais wote wa Marekani na magazeti yaliyokuwa yanachapisha taarifa zao, hata debate kati ya Abraham Lincoln na mpinzani wake unaweza kuisoma ukajua kila mgombea alikuwa anasimamia nini.

Lakini hapa kwetu TBC wanakataa kuchukua Interview wala kurusha matangazo kwa usahihi bila bias ya mgombea wa Upinzani ambaye ni Mtanzania na anayefanya kazi ya kisiasa kihalali kabisa na kisheria. TBC imegeuka TV ya CCM badala ya Taifa. Nadhani labda TBC wangejifunza kwanza kwa BBC wanavyoendesha mambo yao, jinsi ilivyo fair kwa vyama vyote huko ndani ya Great Britain

Labda niwakumbushe vyombo vya habari, kuwa vina wajibu wa kuhabarisha umma lakini vina wajibu wa kukisaidia kizazi kijacho ili kijue Taifa lilikuwa na mitizamo gani ya kijamii, kisiasa na kiuchumi katika miaka fulanifulani. Sasa hivi vyombo haviwezi kulitendea haki Taifa eti kwa kususa kufanya majukumu yake ya uanahabari kwa sababu wanahabari waiomo humo ndani ni Makada wakereketwa, au wanaogopa watawala.

Kwa mfano naishangaa TBC inapotoa sababu zisizo na mashiko eti haaitorusha habari za mikutano ya Chadema mpaka ihakikishiwe ulinzi, sasa nani wa uihakikishia ulinzi, Chadema au Jeshi la Polisi? Sisi wananchi tunataka kufahamu kitu gani kinachojiri kwenye mikutano ya CHADEMA na vyama vingine vyote vinavyoshiriki Uchaguzi huu, hii ni haki yetu ya kikatiba, na TBC ina wajibu huo wa kutuhabarisha kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi, sisi wananchi hatuna interest na beef binafsi kati ya viongozi wa CHADEMA na TBC, sisi tuna interest ya kuonyeshwa mikutano ya kampeni. Sasa TBC ifanye kila inaloweza ipewe huo ulinzi au ifanye inachojua kutupatia sisi wananchi haki yetu ya kikatiba na kisheria!

TBC na vyombo vingine, igeni mfano wa ITV wa kuturushia habari za Lissu, tunataka kumuona Lissu na wagombea wengine wakipewa airtime kwenye vyombo vyenu ili wananchi tuwe na informed decision ya mtu sahihi wa kumpigia kura!

MSILIDHULUMU TAIFA
 
Ayoub Ryoba ni mshikaji wetu zamani zile, tukipata moja Moto moja baridi pale bar ya Maryland Mwenge, alikuwa critic sana kwa serikali namshangaa alipoteuliwa amepiga dramatic u turn, siyo mwenzetu tena.
Kaka, Kiafrika Afrika wanasema unapokula hutakiwi kuongea, kwa sababu kinywa chako kinakua kimejaa msosi. Utaongeaje kwa mfano? This theory applies to Ryoba, Kitila Mkumbo, Katambi, Kafulila nk. Walipopata nafasi ya kula keki ya taifa wakasahau kwamba walikuwa critics wa serikali.
 
Hii ndio maana ya great thinker unadadavua mambo unakosoa unatoa mifano mwisho wa siku hauegemei upande wowote kisiasa

Paschal mayala alikuwa mgombea ubunge kawe kupitia ccm unategemea atakapo toa ushauri utakandamiza chama chake?

Lolote atakalo shauri paschal la kisiasa haliwezi kubalance kamwe labda uje utawala mwingine sio huu wa Magufili
 
Aisee baada ya kuwasifia sana ITV kesho utasikia wanapigwa kadi ya njano wakirudi watasahau hadi wanakopeleka mpira
 
nani alikuambia Tbc1 na 2 ni za Taifa?

Hizi ni mali ya ccm na hufanya kazi ya ccm tu.

hawajui wajibu wao kabisa!

CHADEMA kuwafukuza siku ile ni haki kabisa kwani hata wangekuwepo hawawezi kurusha kwa haki mambo ya CHADEMA.
 
ITV na tv zingine ni sawa na mbingu na ardhi havifanani kabisa iyo ni SUPER BRAND EAST AFRICA hawakujipa bali kazi yao ndo imefanya wakawa hapo walipo
 
Kinachoponza media house nyingi siku hizi ni teuzi, uchwara amejua kuwaharibu vijana kwa kuwateua... wengi wamekuwa wakipambana kujilamba kwa tumaini la kumfurahisha uchwara!
 
Ayoub Ryoba ni mshikaji wetu zamani zile, tukipata moja Moto moja baridi pale bar ya Maryland Mwenge, alikuwa critic sana kwa serikali namshangaa alipoteuliwa amepiga dramatic u turn, siyo mwenzetu tena.
Shetani hana rafiki, iko siku atatutaka tumsaidie bila mafanikio.
 
Back
Top Bottom