Miezi mitano bila Dkt. Magufuli: Chanjo ya Marekani na Uingereza inavyoathiri soko la Tanzania

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
MIEZI MITANO BILA JPM:CHANJO YA MAREKANI NA UINGEREZA INAVYOATHIRI SOKO LA TANZANIA.

Leo 14:30hrs 28/08/2021

Tanzania inategemewa na nchi zote majirani kwa bidhaa mpya ambazo kwa asilimia 75% zinatoka China,hivi sasa nchi hizo majirani zinaelekea Afrika ya Kusini kufuata bidhaa mpya ili kuendana na soko la Wananchi wao,Soko la Kariakoo,nchini Tanzania ndilo linalohudumia nchi zote majirani hasa bidhaa za nguo na viatu,bidhaa za nguo ni tofauti na bidhaa nyingine ambazo zipo ubaoni,bidhaa za nguo zinahitaji watu kwenda China kuchagua sample tofauti tofauti ili kuweza kukidhi soko letu,China ina chanjo yake ambayo ndio kigezo cha mtu yeyote kuingia China,Vivyo hivyo Marekani ina Chanjo yake kama kigezo cha mtu kuingia Marekani.

Asilimia 75% ya bidhaa za Tanzania zinatoka nchini China,kila baada ya wiki mbili Mfanyabiashara anashusha kontena katika bandari ya Dar es Salaam, Tanzania inaitegemea China kwa bidhaa mpya kuweza kukidhi mahitaji ya bidhaa zinazohitajika katika nchi majirani za Congo,Zambia,Malawi,Rwanda na Burundi.Mfanyabiashara wa Kariakoo itamlazimu kutumia maduka machache ya kwenye simu anayoyaamini yaliyopo nchini China,yale maduka aliyozoea kwenda kusagula sagula na kupata aina tofauti tofauti za nguo,hawezi tena kupata bidhaa na wasaa huo kwa kuwa hawezi tena kwenda China kwa sababu hajachoma chanjo ya China,na kwa kuwa chanjo iliyopo ni ya Marekani basi itampasa kwenda Zanzibar kuchoma chanjo nyingine ya China ili aweze kwenda kununua bidhaa nchini China,zaidi ya hapo hawezi kwenda China,na biashara itakuwa si ya bidhaa mpya zinazoendana na uhitaji wa soko.

-Ujasiri wa Rais Magufuli.

Vita ya kiuchumi inakupasa kuwa jasiri,la sivyo unafeli,vitisho vitatoka kila upande, pengine raia tunaweza tusione lakini wakubwa wa dunia wana uwezo wa kutisha na ukatishika ili uweze kufuata matakwa yao,Hayati Rais Magufuli aliweka msimamo wa kutokwenda Ulaya,maana vita ya kiuchumi ilikuwa kubwa,wazo lilikuwa Mimi siji na nyie msije,na kwa kuwa wanatutegemea sisi kwa asilimia 90% wasingeweza kuvumilia,kwa vyovyote vile wangekuja mezani kuzungumza,hivi leo Wachina wanaingia kwetu free wakiwa wamepiga michanjo yao lakini Watanzania hawawezi kwenda China kwa kuwa hawajapiga chanjo ya China,kwa Rais Magufuli hili lilikuwa jepesi sana kama sisi hatuji kwenu basi na ninyi msije kwetu,haiwezekani wewe uje kwangu halafu Mimi unanikataza kuja kwako,Mimi naiamini vipi chanjo yako,basi ili twende sawa Mimi nitapiga chanjo ya China na Wachina wakija nao wanunue Covidol,hii ndio win win situation,mfano haiwezekani Mimi nilipie Visa dola 200 kuja kwako halafu wewe ulipie dola 100 kuja kwangu,hii si sawa,mia kwa mia ndio sawa.

Mzozo wa kiuchumi uliowahi kuingiwa kati ya Tanzania na Kenya uliosababisha Wakenya kuzuia magari kuingia Kenya kuchukua watalii kuwaleta katika mbuga ya Serengeti,nchini Tanzania,Mzozo huo uliibuka baada ya Kenya kuona inapoteza watalii kwenda Tanzania,na sisi tulivyokataza gari zao kuingia Tanzania,walishindwa kuvumilia wakaja mezani na tukatafuta win win situation,Mbuga nzuri ya Serengeti yenye wanyama wote wanaopatikana duniani,hotel nzuri za kisasa tofautisha na hotel za Kenya zilizojengwa miaka ya 1940,Changamoto ya mizozo ya Kenya na Somalia ilifanya watalii kupendelea kuja Tanzania,Mwaka 2018 idadi ya Watalii iliongezeka nchini Tanzania baada ya ununuzi wa Ndege ambazo zimeweza kuwaleta Watalii moja kwa moja nchini Tanzania bila kushukia Kenya,Vivyo hivyo tuliona mzozo mpakani mwa Tanzania na Rwanda ambao madereva wa malori walikuwa wanaishia mpakani halafu wanawapa magari yao madereva wa Rwanda ili waweze kuyaingiza nchini Rwanda hali iliyosababisha hasara kwa Wafanyabiashara wa Tanzania,nasi tukawafanyia hivyo hivyo,wakashindwa kuvumilia wakaja mezani,Jiwe kwa jiwe,vinginevyo wanakunawa maji wanakufanya mtaji,Tanzania ni tajiri kwa kila kitu,hatuwezi kuwa mitaji ya watu.

-Nini tufanye kuokoa Soko la Kariakoo.

China imekuwa msaada kwa nchi za dunia ya tatu ambazo kwa muda mrefu zimekuwa wahanga wa hofu,Magonjwa,unyonyaji,kupuuzwa na ukandamizaji,lakini kujitokeza kwa China na kuwa na sauti kwenye jukwaa la kimataifa, iwe ni kwenye eneo la uchumi au eneo la kidiplomasia, kumefanya hali ya unyonyaji na kupuuzwa kupungua au hata kutoweka,Tukiangalia tangu mwaka 2001 China ilipojiunga na Shirika la Biashara duniani WTO, hali mpya ilianza kujitokeza katika nchi za Afrika, na kwenye nchi za dunia ya tatu. Bidhaa ambazo zamani zilikuwa ni haki ya matajiri, zilianza kuwa za kawaida kwa watu maskini katika nchi hizo,mambo ambayo yalikuwa ndoto tu au yaliyoonekana kuwa haki ya matajiri wa Ulaya na Marekani, yakaanza kuonekana kuwa ni mambo yanayowezekana kwa watu wa nchi hizo. Maendeleo ya viwanda nchini China yakawa ni msaada mkubwa sana kwa watu wa nchi hizo kubadilisha maisha yao,mbali na biashara zilizogusa moja kwa moja maisha ya watu wa kawaida, serikali za nchi hizo zilipata chanzo kipya cha fedha, iwe ni mikopo au mitaji,Kwa muda mrefu, baadhi ya nchi za magharibi zilikuwa zinatumia nyenzo hizo kama njia ya uingiliaji na ukandamizaji wa nchi za dunia ya tatu yaani nchi masikini.

Tumeona ushirikiano kati ya China na Afrika ulipata habari nyingi nzuri,China ilipotengeneza chanjo yake,ilitoa msaada kwa nchi za Ethiopia, Rwanda, Lesotho na Togo zilipata msaada wa chanjo kutoka kwa China; Kenya imeidhinisha matumizi ya chanjo ya Sinopharm ya China, na dozi milioni 2 zinatarajiwa kuwasili Nairobi,hii itakuwa pigo kwa Tanzania,Kenya wataanza kwenda China kuchukua bidhaa bora tofauti tofauti wakichagua wenyewe madukani na kuzileta Tanzania,watatuuzia kwa bei juu,Wizara ya Afya ya Misri itasambaza chanjo ya Sinovac ya China iliyotengenezwa nchini humo kwa kituo cha usambazaji wa chanjo cha taifa ili itolewe kwa umma, na uwezo wa uzalishaji wa chanjo hiyo nchini humo unaweza kufikia dozi milioni 15 hadi 18 kwa mwezi. Hivi sasa, China inaongoza duniani kwa kutoa chanjo kwa wingi zaidi kwa nchi za nje, idadi ambayo imezidi jumla ya chanjo zilizotolewa na nchi nyingine zote kwa nje. Kati ya nchi zilizopokea chanjo za China kama msaada, theluthi moja ni nchi za Afrika,Ukosefu wa chanjo ya China nchini Tanzania,inaathiri soko la biashara nchini Tanzania,kwa kuwa tumeyavulia maji nguo basi hatuna budi kuyaoga,tuagize chanjo ya China ili watu waende China wakauze na kununua, vinginevyo tutingishe kiberiti tuwazuie wasije Tanzania kwa kuwa wao wametukataza tusiende China,jiwe kwa jiwe.

-Tuzingatie vigezo na masharti tunapoagiza chanjo.

Hivi karibuni, makala moja iliyochapishwa kwenye Gazeti la The New York Times imefichua ukweli unaoumiza na kukasirisha watu, pengine chanjo itakayotolewa na nchi za magharibi kwa watu waliomaliza kuchanjwa inazalishwa barani Afrika ambako watu wengi hawajapata chanjo,kwa mujibu wa utafiti wa gazeti la The Times la Uingereza, mwaka huu serikali ya Afrika Kusini ilisaini mkataba usio wa kawaida na kampuni ya Johnson ya Marekani ambao unaitaka Afrika Kusini iache haki ya kuzuia uuzaji chanjo inazotengenezwa ndani ya nchi hiyo kwa nchi za nje. Msemaji wa Wizara ya Afya ya Afrika Kusini Popo Maja, alisema serikali hairidhiki na mkataba huo, lakini haina karata ya kukataa madai hayo. “Serikali haina chaguo lolote, kusaini mkataba ama kutokuwa na chanjo.” alisema katika taarifa moja. Hii imefichua umwamba wa nchi hizo za magharibi, na pia kuonesha hisia za kutokuwa na la kufanya na kukata tamaa kwa nchi hizo za Afrika.

Nimalizie kwa kumuenzi Hayati Rais Daktari John Pombe Magufuli na mfano wa nchi zote zilizojaribu kupambana na Corona kwa kufuata mfumo wa kimagharibi mwishoni wa mwaka 2020 ziliishia kupata ukuaji hasi wa uchumi kwenye nchi zao,Tanzania tu ndiyo iliyopata ukuaji wa uchumi chanya kwenye nchi zote za Afrika mashariki. Sasa kwa nini sisi watanzania tunaona aibu kujivunia hizo mbinu za asili?Mwaka jana tulipambana na Corona kwa kutumia njia tatu.
1. Kumtanguliza Mungu mbele
2. Kufuata mbinu mbalimbali tunazoshauriwa na watalaamu wetu
3.Kuchapa kazi kwa bidii

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.

-Master of Leadership and Management.
 
Hivi wachina kwanini mnajidanganya ni ndugu zenu??

Unasema watu wamechanja chanjo ya US na sio ya China na huku unamtaja Magufuli aliyekataa chanjo kabisa huku akidhani nchi imejifungia bila kupokea wageni wala watanzania kusafiri kwenda nje
 
Kwakua una uovu ndani mwako....Hiyo chuki yako kwa Hayati ipo siku utaijutia sana and you wont have a chance to repent
Kuna watu vipofu na wasio na maono na hao ndio wapinzani wa Magufuli. Nani kasema kutojitenga na Dunia kunamaanisha kuwa Photocopier wa kila kitu cha Wengine? Misemo ya Mama SSH eti hatuwezi kujitenga na Dunia. Kwa hiyo, Magufuli alijitenga na Dunia? Ni kauli za watu wasio nq Maono kabisa. Sasa Kufuata mkumbo wa Lockdown kama njia ya kutojitenga na Dunia kuliwasaidia vipi waliofuata huo mkumbo?
 
Kwakua una uovu ndani mwako....Hiyo chuki yako kwa Hayati ipo siku utaijutia sana and you wont have a chance to repent
Kwa economic analysis ndogo ya nchi yetu ni kwamba JPM amekufa ili kuinusuru nchi yetu hata hayo makato yametokana na uharibifu wa banking system kwa mtindo wake wa kitoto wake wa ku freeze account za wafanya biashara.TATIZO WATANZANIA TUPO KAMA MALAYA HATUELEWI TUNATAKA NINI.Tukipata bwana mwenye pesa tunaanza kulalamika hana nguvu za kiume,tukipata mwenye nguvu za kiume tunaanza kulalamika anatuchubua uk...
 
MIEZI MITANO BILA JPM:CHANJO YA MAREKANI NA UINGEREZA INAVYOATHIRI SOKO LA TANZANIA.

Leo 14:30hrs 28/08/2021

Tanzania inategemewa na nchi zote majirani kwa bidhaa mpya ambazo kwa asilimia 75% zinatoka China,hivi sasa nchi hizo majirani zinaelekea Afrika ya Kusini kufuata bidhaa mpya ili kuendana na soko la Wananchi wao,Soko la Kariakoo,nchini Tanzania ndilo linalohudumia nchi zote majirani hasa bidhaa za nguo na viatu,bidhaa za nguo ni tofauti na bidhaa nyingine ambazo zipo ubaoni,bidhaa za nguo zinahitaji watu kwenda China kuchagua sample tofauti tofauti ili kuweza kukidhi soko letu,China ina chanjo yake ambayo ndio kigezo cha mtu yeyote kuingia China,Vivyo hivyo Marekani ina Chanjo yake kama kigezo cha mtu kuingia Marekani.

Asilimia 75% ya bidhaa za Tanzania zinatoka nchini China,kila baada ya wiki mbili Mfanyabiashara anashusha kontena katika bandari ya Dar es Salaam, Tanzania inaitegemea China kwa bidhaa mpya kuweza kukidhi mahitaji ya bidhaa zinazohitajika katika nchi majirani za Congo,Zambia,Malawi,Rwanda na Burundi.Mfanyabiashara wa Kariakoo itamlazimu kutumia maduka machache ya kwenye simu anayoyaamini yaliyopo nchini China,yale maduka aliyozoea kwenda kusagula sagula na kupata aina tofauti tofauti za nguo,hawezi tena kupata bidhaa na wasaa huo kwa kuwa hawezi tena kwenda China kwa sababu hajachoma chanjo ya China,na kwa kuwa chanjo iliyopo ni ya Marekani basi itampasa kwenda Zanzibar kuchoma chanjo nyingine ya China ili aweze kwenda kununua bidhaa nchini China,zaidi ya hapo hawezi kwenda China,na biashara itakuwa si ya bidhaa mpya zinazoendana na uhitaji wa soko.

-Ujasiri wa Rais Magufuli.

Vita ya kiuchumi inakupasa kuwa jasiri,la sivyo unafeli,vitisho vitatoka kila upande, pengine raia tunaweza tusione lakini wakubwa wa dunia wana uwezo wa kutisha na ukatishika ili uweze kufuata matakwa yao,Hayati Rais Magufuli aliweka msimamo wa kutokwenda Ulaya,maana vita ya kiuchumi ilikuwa kubwa,wazo lilikuwa Mimi siji na nyie msije,na kwa kuwa wanatutegemea sisi kwa asilimia 90% wasingeweza kuvumilia,kwa vyovyote vile wangekuja mezani kuzungumza,hivi leo Wachina wanaingia kwetu free wakiwa wamepiga michanjo yao lakini Watanzania hawawezi kwenda China kwa kuwa hawajapiga chanjo ya China,kwa Rais Magufuli hili lilikuwa jepesi sana kama sisi hatuji kwenu basi na ninyi msije kwetu,haiwezekani wewe uje kwangu halafu Mimi unanikataza kuja kwako,Mimi naiamini vipi chanjo yako,basi ili twende sawa Mimi nitapiga chanjo ya China na Wachina wakija nao wanunue Covidol,hii ndio win win situation,mfano haiwezekani Mimi nilipie Visa dola 200 kuja kwako halafu wewe ulipie dola 100 kuja kwangu,hii si sawa,mia kwa mia ndio sawa.

Mzozo wa kiuchumi uliowahi kuingiwa kati ya Tanzania na Kenya uliosababisha Wakenya kuzuia magari kuingia Kenya kuchukua watalii kuwaleta katika mbuga ya Serengeti,nchini Tanzania,Mzozo huo uliibuka baada ya Kenya kuona inapoteza watalii kwenda Tanzania,na sisi tulivyokataza gari zao kuingia Tanzania,walishindwa kuvumilia wakaja mezani na tukatafuta win win situation,Mbuga nzuri ya Serengeti yenye wanyama wote wanaopatikana duniani,hotel nzuri za kisasa tofautisha na hotel za Kenya zilizojengwa miaka ya 1940,Changamoto ya mizozo ya Kenya na Somalia ilifanya watalii kupendelea kuja Tanzania,Mwaka 2018 idadi ya Watalii iliongezeka nchini Tanzania baada ya ununuzi wa Ndege ambazo zimeweza kuwaleta Watalii moja kwa moja nchini Tanzania bila kushukia Kenya,Vivyo hivyo tuliona mzozo mpakani mwa Tanzania na Rwanda ambao madereva wa malori walikuwa wanaishia mpakani halafu wanawapa magari yao madereva wa Rwanda ili waweze kuyaingiza nchini Rwanda hali iliyosababisha hasara kwa Wafanyabiashara wa Tanzania,nasi tukawafanyia hivyo hivyo,wakashindwa kuvumilia wakaja mezani,Jiwe kwa jiwe,vinginevyo wanakunawa maji wanakufanya mtaji,Tanzania ni tajiri kwa kila kitu,hatuwezi kuwa mitaji ya watu.

-Nini tufanye kuokoa Soko la Kariakoo.

China imekuwa msaada kwa nchi za dunia ya tatu ambazo kwa muda mrefu zimekuwa wahanga wa hofu,Magonjwa,unyonyaji,kupuuzwa na ukandamizaji,lakini kujitokeza kwa China na kuwa na sauti kwenye jukwaa la kimataifa, iwe ni kwenye eneo la uchumi au eneo la kidiplomasia, kumefanya hali ya unyonyaji na kupuuzwa kupungua au hata kutoweka,Tukiangalia tangu mwaka 2001 China ilipojiunga na Shirika la Biashara duniani WTO, hali mpya ilianza kujitokeza katika nchi za Afrika, na kwenye nchi za dunia ya tatu. Bidhaa ambazo zamani zilikuwa ni haki ya matajiri, zilianza kuwa za kawaida kwa watu maskini katika nchi hizo,mambo ambayo yalikuwa ndoto tu au yaliyoonekana kuwa haki ya matajiri wa Ulaya na Marekani, yakaanza kuonekana kuwa ni mambo yanayowezekana kwa watu wa nchi hizo. Maendeleo ya viwanda nchini China yakawa ni msaada mkubwa sana kwa watu wa nchi hizo kubadilisha maisha yao,mbali na biashara zilizogusa moja kwa moja maisha ya watu wa kawaida, serikali za nchi hizo zilipata chanzo kipya cha fedha, iwe ni mikopo au mitaji,Kwa muda mrefu, baadhi ya nchi za magharibi zilikuwa zinatumia nyenzo hizo kama njia ya uingiliaji na ukandamizaji wa nchi za dunia ya tatu yaani nchi masikini.

Tumeona ushirikiano kati ya China na Afrika ulipata habari nyingi nzuri,China ilipotengeneza chanjo yake,ilitoa msaada kwa nchi za Ethiopia, Rwanda, Lesotho na Togo zilipata msaada wa chanjo kutoka kwa China; Kenya imeidhinisha matumizi ya chanjo ya Sinopharm ya China, na dozi milioni 2 zinatarajiwa kuwasili Nairobi,hii itakuwa pigo kwa Tanzania,Kenya wataanza kwenda China kuchukua bidhaa bora tofauti tofauti wakichagua wenyewe madukani na kuzileta Tanzania,watatuuzia kwa bei juu,Wizara ya Afya ya Misri itasambaza chanjo ya Sinovac ya China iliyotengenezwa nchini humo kwa kituo cha usambazaji wa chanjo cha taifa ili itolewe kwa umma, na uwezo wa uzalishaji wa chanjo hiyo nchini humo unaweza kufikia dozi milioni 15 hadi 18 kwa mwezi. Hivi sasa, China inaongoza duniani kwa kutoa chanjo kwa wingi zaidi kwa nchi za nje, idadi ambayo imezidi jumla ya chanjo zilizotolewa na nchi nyingine zote kwa nje. Kati ya nchi zilizopokea chanjo za China kama msaada, theluthi moja ni nchi za Afrika,Ukosefu wa chanjo ya China nchini Tanzania,inaathiri soko la biashara nchini Tanzania,kwa kuwa tumeyavulia maji nguo basi hatuna budi kuyaoga,tuagize chanjo ya China ili watu waende China wakauze na kununua, vinginevyo tutingishe kiberiti tuwazuie wasije Tanzania kwa kuwa wao wametukataza tusiende China,jiwe kwa jiwe.

-Tuzingatie vigezo na masharti tunapoagiza chanjo.

Hivi karibuni, makala moja iliyochapishwa kwenye Gazeti la The New York Times imefichua ukweli unaoumiza na kukasirisha watu, pengine chanjo itakayotolewa na nchi za magharibi kwa watu waliomaliza kuchanjwa inazalishwa barani Afrika ambako watu wengi hawajapata chanjo,kwa mujibu wa utafiti wa gazeti la The Times la Uingereza, mwaka huu serikali ya Afrika Kusini ilisaini mkataba usio wa kawaida na kampuni ya Johnson ya Marekani ambao unaitaka Afrika Kusini iache haki ya kuzuia uuzaji chanjo inazotengenezwa ndani ya nchi hiyo kwa nchi za nje. Msemaji wa Wizara ya Afya ya Afrika Kusini Popo Maja, alisema serikali hairidhiki na mkataba huo, lakini haina karata ya kukataa madai hayo. “Serikali haina chaguo lolote, kusaini mkataba ama kutokuwa na chanjo.” alisema katika taarifa moja. Hii imefichua umwamba wa nchi hizo za magharibi, na pia kuonesha hisia za kutokuwa na la kufanya na kukata tamaa kwa nchi hizo za Afrika.

Nimalizie kwa kumuenzi Hayati Rais Daktari John Pombe Magufuli na mfano wa nchi zote zilizojaribu kupambana na Corona kwa kufuata mfumo wa kimagharibi mwishoni wa mwaka 2020 ziliishia kupata ukuaji hasi wa uchumi kwenye nchi zao,Tanzania tu ndiyo iliyopata ukuaji wa uchumi chanya kwenye nchi zote za Afrika mashariki. Sasa kwa nini sisi watanzania tunaona aibu kujivunia hizo mbinu za asili?Mwaka jana tulipambana na Corona kwa kutumia njia tatu.
1. Kumtanguliza Mungu mbele
2. Kufuata mbinu mbalimbali tunazoshauriwa na watalaamu wetu
3.Kuchapa kazi kwa bidii

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.

-Master of Leadership and Management.
Bidhaa nyingi toka China ni za kugushi na low quality.

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Ukimsifu shetani (jiwe) kwenye sifa za nchi, basi sifa zako zote zinakuwa batili
Mungu akusamehe tu kwa sababu hujui ulisemalo!! Kwanza sifa na utukufu wote apewe Mungu!!! Lakini Mungu hutumia watu walio tayari na walio waaminifu!! Katika kuliponya Taifa letu la Tanzania dhidi ya corona, Mungu alimtumia Rais Magufuli!!! Mambo aliyoyasema Magufuli yakakaonekana ni upuuzi ndiyo yanayofuatwa na kukubalika leo!! Magufuli alisema hakuna lockdown, leo mataifa mengi yameachana na lockdown!! Alisema wanadamu wajiandae kupambana na kuishi na corona wala si kama mlipuko wa kuondoka!! Leo mabeberu wameikubali hiyo na wameandaa utaratibu wa kuishi na corona kwa kudungwa chanjo za mara kwa mara wanazoziita booster!!
Magufuli aliletwa na Mungu kwa kazi maalumu ya kutuvusha watanzania kwenye corona kwa njia ya kumtanguliza Mungu!!. Kazi hiyo aliifanya kwa uaminifu sana na alipoikamilisha na kumpa Mungu utukufu akawa amemaliza kazi yake maalumu ambayo kwayo aliumbwa, na Mungu AKAMTWAA!! He completed his special assignment with flying colours!! Tutamkuta mbinguni!!! Ndiyo maana wanapata taabu sana wanaojaribu kubatilisha vitu alivyotuachia Magufuli maana ni kweli za ki-Mungu!! Kwa mfano huwezi ukaipamba chanjo ya corona mbele ya watanzania na wakakuelewa!!
 
Kwa economic analysis ndogo ya nchi yetu ni kwamba JPM amekufa ili kuinusuru nchi yetu hata hayo makato yametokana na uharibifu wa banking system kwa mtindo wake wa kitoto wake wa ku freeze account za wafanya biashara.TATIZO WATANZANIA TUPO KAMA MALAYA HATUELEWI TUNATAKA NINI.Tukipata bwana mwenye pesa tunaanza kulalamika hana nguvu za kiume,tukipata mwenye nguvu za kiume tunaanza kulalamika anatuchubua uk...
Tuache visingizio...JPM had his own vision ambayo haikufanikiwa kufikia mwisho wake...Sisi wengine tuache kuwa matarishi wa mataifa makubwa...JPM could have brought change ambayo dunia ingeishangaa Africa...Watu wasio na maono wala confidence have nothing to tell me...Endeleeni na utopolo wenu ipo siku historia itawahukumu!
 
Back
Top Bottom