Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar lakini ukweli namna Kassim Hanga alivyouwawa hauwekwi wazi

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
1,126
4,169
Mpaka leo Dunia nzima haijapata ukweli kama alipigwa risasi au kutumbukizwa baharini.

Hanga alikubalika sana kwa uwezo wake wa kudadavua mambo na kuwa na ushawishi mkubwa ndio maana Mzee Karume alimchukia. Hii ni kwa mujibu wa mzee Aman Than

Kwa nini CCM hawaweki ukweli huu?
 
Mpaka leo Dunia nzima haijapata ukweli kama alipigwa risasi au kutumbukizwa baharini.

Hanga alikubalika sana kwa uwezo wake kudadavua mambo na kuwa na ushawishi mkubwa ndio maana Mzee Karume alimchukia. Hii ni kwa mujibu wa mzee Aman Than

Kwa nini CCM hawaweki ukweli huu?
CCM inahusika vipi na mambo ya Zanzibar?. Kiukweli kabisa elimu ya uraia inahitajika sana, CCM ilizaliwa mwaka 1977, Mapinduzi ya Zanzibar yalitokea mwaka 1964!, wapi na wapi?!
P
 
pascal MAYALA, Hanga aliuawa na Karume kwa idhini ya Nyerere CCM kama mnavyosema hawa ni waasisi wa chama basi haikwepi dhambi hii. Kasimu Hanga mwana mapinduzi na wazir na balozi kuuawa baada tu ya Nyerere kumkabidhi karume kinyume na ombi lake la kutopelekwa zanziba baada ya kurudishwa nchini kwa ombi maalumu la NYERERE. Huoni kwamba hizo njama ni za waasisi wa chama?
 
Hiyo bado ni classified tu sio kwamba haijulikani.

Wanamapinduzi "halisi" ilibidi waondolewe ili kuweka utulivu fulani fulani kwenye muundo wa serikali na historia iwekwe baadhi ya watu waliokuwa wameandaliwa kwa ajili ya kuongoza tu na sio kuingia battlefield.

Hii mwalimu wangu mmoja wa kozi fulani aliniambia "wengi wakienda kuwinda na mbwa porini mbwa atafukuza mnyama na atamuua atambeba mdomoni kumletea mfugaji ila mfugaji akishachuna ngozi kuna mawili mbwa anaweza kutupiwa ngozi tu au akafukuzwa kabisa asiambulie hata ngozi huku mfugaji wake akiambulia vyote"
 
Back
Top Bottom