Kumbukumbu Mapinduzi ya Zanzibar: Kutoka waliopindua na waliopinduliwa (Sehemu 1)

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,913
30,254
KUMBUKUMBU ZANGU ZA MAPINDUZI NA WATU WA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YA 1964 SEHEMU YA KWANZA

Nakumbuka kuangalia gazeti nikasoma na kuona picha za vurugu zilizotokea Zanzibar.

Gazeti hili bila shaka litakuwa ni Ngurumo au Mwafrika kwani haya ndiyo yalikuwa magazeti maarufu yaliyokuwa yakisomwa na watu.
Vurugu hizi zilikuwa za uchaguzi wa mwaka wa 1963 wa Zanzibar baada ya uchaguzi wa mwaka wa 1961.

Chaguzi zote mbili zilikuwa za msuguano mkubwa na damu ilimwagika.
Mwaka wa 1963 nilikuwa na umri wa miaka 11 na niko darasa la tano.

Hii ndiyo kumbukumbu yangu ya kwanza ya Zanzibar kuingia akilini kwangu.

Nakumbuka siku moja niko barazani nyumbani kwa rafiki zangu wawili mtu na ndugu yake, Mohamed Abdulrahman Talib na Ali Hussein (hawa baba zao ni ndugu mtu na kaka yake lakini mmoja ni Muarabu wala huulizi lakini mwingine Mzee Hussein ni mweusi ila nywele zake ndiyo zitakuonyesha kuwa ana damu ya Kiarabu).

Bila shaka yoyote mama yake alikuwa Mwafrika. Hawa ndugu wawili wote asili yao ni Tanganyika.

Leo mimi mtu mzima mwenye akili ya kuchambua mambo naangalia nyuma na nimewataja hapa hawa baba zangu kwa rangi zao hawa ni ndugu, damu moja wote Wazanzibari lakini rangi za ngozi zao tofauti.

Hawa bahati nzuri ni Watanganyika si Wazanzibari.

Rafiki yangu Mohamed Abdulrahman alikuwa na jina lake la utani tukimwita, ‘’Kitunguu,’’ na ndugu yake, Ali tukimwita, ‘’Nakioze.’’

Jina hili Nakioze lilikuwa jina la muuza genge Mtaa wa Kipata ambae ukimwambia mbona anauza vitu ghali anakujibu, ‘’Usinunue nakioze,’’ akiwa na maana hatauza kwa bei hiyo acha kioze atakitupa.

Baba zangu hawa wawili Mzee Abdulrahman na Mzee Hussein laiti kama wangelikuwa ni Wazanzibari tayari pangekuwa na tatizo.

Hadi leo mimi najiuliza imekuwaje mimi sikupata kumuangalia Mohamed kama Muarabu hadi hivi sasa tumekuwa wazee na huwa tunakutana.

Fikra kuwa namwangalia Mohamed kwa rangi yake haijapata kunipitikia.

Siku moja niko barazahni kwa Mzee Abdulrahman Talib na mwanae Mohamed Kitunguu tunacheza Mzee Abdulrahman alitoka ndani amebeba sanduku la nguo akaingia ndani ya taxi anakwenda uwanja wa ndege.

Safari ile alikuwa anakwenda Zanzibar kwenye sherehe za uhuru. Mwaka wa 1963 ndiyo mwaka Zanzibar na Kenya zilipata uhuru.

Sal Davis mwimbaji maarufu wa wakati ule akatunga nyimbo, ‘’Uhuru of Kenya,’’ yaani Uhuru wa Kenya lakini nyimbo hii ikijulikana kwa jina la ‘’Ay Ay Ay Uhuru,’’ na katika nyimbo ile akawataja viongozi wa Afrika ya Mashariki waliokuwa madarakani – Nyerere, Obote, Kenyatta na Mohamed Shamte Waziri Mkuu wa Zanzibar.

Sal Davis alikuwa na miaka 22 kijana mdogo.

Nyimbo hii ilikuwa maarufu ikipigwa sana TBC lakini ghafla yakatokea mapinduzi na serikali ya Mohamed Shamte ikaangushwa.

Nyimbo ikapigwa marufuku ikawa haipigwi tena TBC kwa kuwa Mohamed Shamte hakuwa tena Waziri Mkuu wa Zanzibar.

Sikuweza hata kwa mbali kufikiria kuwa iko siku miaka mingi baadae Sal Davis atakuwa rafiki yangu na atanialika Zanzibar mimi na mke wangu.

Nyumba kama mbili kutoka nyumba hii ya Mzee Abdulrahman ilikuwa nyumba ya Bi. Saada mama yake rafiki yetu Abdul Kigunya.

Hapa nyumbani kwao Mtaa wa Gogo na Mchikichi kulikuwa na baraza kubwa sana ya wazee wakicheza bao.

Hapa ndipo mimi na marafiki zangu tulipomuona Abdullah Kassim Hanga kwa mara ya kwanza.

Hii sasa ilikuwa mwaka wa 1964 na mapinduzi yashafanyika.

Hanga alikuwa akija sana pale kucheza bao akikaa chini kwenye jamvi na watu wa kawaida kabisa na akija pale kwa miguu hakuwa anakuja na gari.

Siku zile mawaziri waliokuwa na magari aina ya Humber. Magari ya Kiingereza.

Nakumbuka kusimama Barabara ya Uhuru na Sikukuu karibu ya duka la Toti kuangalia msafara wa Mwalimu Nyerere na Karume ukipita ndani ya Rolls Royce wamesimama wanapungia watu msafara ukielekea Ikulu kwa shughuli ya kutia saini mkataba wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Wakati ule nikiwa mtoto wa miaka 12 haikunipitikia kama itafika siku nitakuwa na Mzee Aboud Jumbe nyumbani kwake mimi na wenzangu tunaiangalia picha hii aliyotutolea Mzee Jumbe picha ambayo alitaka iwe katika kitabu ‘’The Partnership,’’ alichokuwa ameandika kuhusu Muungano na matatizo yake.

Mimi na wenzangu tulikuwa wahariri na wachapaji wa kitabu hiki. Huu ulikuwa mwaka wa 1994.

Miaka 30 ilikuwa imepita kutoka siku ile nikiwa mtoto mdogo wa miaka 12 nilipokuwa nimesimama pamoja na watu wengi nje ya duka la Toti tukiangalia msafara wa Nyerere na Karume ukienda Ikulu kukamilisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Abdullah Kassim Hanga alikuwa marehemu na Mzee Jumbe alinihadithia chanzo cha ugomvi wa Mzee Karume na ambao pengine ndiyo uliosababisha Hanga kupoteza nafasi yake katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mzee Jumbe alikuwako siku ambayo viongozi hawa wawili wa mapinduzi walipopishana kauli na kutoleana maneno makali.

Kisa hiki Mzee Jumbe amepata kukihadithia kama mara mbili hivi nami nikiwepo.

Hii ni kumbukumbu yangu ya kwanza ya mapinduzi na watu wa mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964.

325133731_1007801390178021_5202700091768843711_n.jpg
324910930_1089952662406261_6172726422001660833_n.jpg
 
Wana bodi, japo tuko kwenye harakati za kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge, kuna swali linanitatiza kuhusu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ambapo majibu yake sahihi, pia yanaweza kuwa ni kiashiria tosha cha mshindi wa urais wa Zanzibar, iwapo uchaguzi utakuwa huru na wa haki.

Swali hili lahusu ukweli haswa kuhusu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, 1964, baada ya kuibuka kwa kitabu kingine kiitwacho "Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru"
View attachment 2077603
kilichoandikwa na Mwanazouni wa Zanzibar, Dr. Harith Ghassany, kama kilivyofanyiwa mapitio na mwandishi Mohamed Said kwenye gazeti la Al-Nuur la leo.

Ghasanny anasema kumbe Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalitekelezwa na askari mamluki wa Kimakonde (Wakata Mkonge) ambao waliongozwa na Mzee Mohamed Omar Mkwawa (Tindo) chini ya Amiri Jeshi wa jeshi la mamluki hao Victor Mkello (RIP). (kumbe amiri jeshi hakuwa Mganda John Okello pekee, bali pia Mkello yumo?!.

Mamluki hao walitumia zana zao za kukatia mkonge, zile sime za makali kuwili, walizisunda kwenye nguo zao za ndani na kusafirishwa kwa mitumbiwi usiku usiku kupitia Kipumbwi. Jee wale mashuhuda wa Mapinduzi yale Matukufu ya Zanzibar, wanayakubali haya?.

Pia mwandishi anamalizia kwa kusema hata mauaji ya Karume, hayakutekelezwa na wapinga Mapinduzi, bali ni miongoni mwa hao hao wanamapinduzi, baada ya kupishana kauli fulani fulani za uendeshaji wa Zanzibar baada ya Mapinduzi.

Nimesoma kitabu cha John Okello kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar,
View attachment 2077618
yeye anasema yake, vitabu kadhaa vya waandishi wazungu wanasema yao, historia tukuka ya Mapinduzi Matukufuya ya Zanzibar nayo nayo inasema kivyake, hivi hakuna any straight line yoyote kuhusu Mapinduzi hayo, ya Zanzibar?.
Jee yalipangwa na nani? Yalitekelezwaje?.
Nini haswa kilichotokea usiku ule wa Januari 11?.
Nani alifanya nini wapi?
Na mwisho tuzungumzie wafaidika wa Mapinduzi hayo Matukufu ya Zanzibar na bila kuwasahau wahanga wa Mapinduzi hayo ambao kwako yatakuwa sio Matukufu, ni kina nani haswa?, na kama kuleta amani na utangamano wa Zanzibar kuhusu Mapinduzi hayo kutahitajika kuundwa kwa Tume ya Ukweli na Upatanisho, "Truth and Reconciliation Commission" ili waliohasimiana kutokana na Mapinduzi hayo, wapatanishwe kwa maslahi mapana ya Zanzibar?.

Majibu ya maswali haya yatasaidia kujua mustakabali wa matokea ya uchaguzi wa Zanzibar kudhirihisha kuwa Wazanzibari ni wamoja, hakuna kundi la walishiriki Mapinduzi ndio wenye uhalali zaidi kuitawala Zanzibar kuliko wasioshiriki, after all kumbe Mapinduzi yenyewe, yametekelezwa na askari mamluki wa Kimakonde, toka mashamba ya mkonge Tanga!.

Pasco
Rejea za Mwandishi huyu kuhusu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
  1. Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Bado Kuna Maswali Bila Majibu -1
  2. Neno "Matukufu" Katika Mapinduzi ya Zanzibar, Lilitoka Wapi, na Yana Utukufu Gani?!,
  3. Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa! Walikimbia Wenyewe - Mzee Sukari
Tarehe kama ya leo 11/01/1964 miaka 60 iliyopita, ndio Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalifanyika!. Alfajiri ya Tarehe 12 Januari, 1964 ilikuwa ni kutangazwa tuu!.

Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Paskali
 
Back
Top Bottom