Miaka 30 bila mke imekuwa kitu cha kawaida sana

Miaka 30 bila mke imekuwa kitu cha kawaida sana

SanArt

Senior Member
Joined
Oct 14, 2026
Posts
196
Reaction score
427
Hakika zama zimebadilika. Siku hizi vijana wa miaka ya 30 nao bado wanaishi nyumbani, bado wanategemea wazazi wao.

Nilivyo kuwa in my early 20s nilidhani by the end of my 20s Nitakuwa na familia yangu na watoto wawili.

Ila sasa ndo akili zinanijia kuwa it was just a dream, mifumo imebana sana na kutufanya iwe ngumu sana kwa kijana mwenye umri huo, ambaye kwa miaka 20 nyuma tayari angelikuwa na mianya yake mingi ya hela. Nakumbuka kabla hata mzee wangu hajaoa in his mid 20s tayari alikuwa anamiliki Suzuki.

Tayari alikuwa na mshamba, alikuwa na uwezo wa ulisha familia na ndugu pande zote. Yaani najiuliza, why bado tunaishi na mentality za kudhani kuwa ajira inaleta stability wakati hata wages unayo lipwa haiwezi kukufanya uwe stable.

Ndoa hazidumu pia kwasababu hiyo hiyo, ni stress juu ya stress tu. Yaani mtu unalipwa 2m ila bado Ukisema ujenge financial stability inakuwa ngumu maana running cost nazo zinakuitaji, ukinunua kiwanja kuja ukajenge nako mtihani, ukipanga unaishia kuendelea kupanga tu na wazo la kujenga hata haliji maana kila Mshahara unakuta umekaa kila angle.

Sasa hata mkianza kuwa laumu vijana kushindwa kujitegemea mnakuwa mnakosea Hakika maana zama nazo zimebadilika.
 
Hakika ila mimi naona hali ni mbaya kotekote tu.
Kwa kijijini n tofauti kidogo. Nna jamaa yangu alikimbia mjini baada ya kuona hali ya kipato si nzuri karudi kwao kapewa eneo na wazazi. Analima na kajenga boma lake na kaoa na maisha yanaenda ila kwa mjini hali ni tofauti sana. Nyumba tu ya kutosha familia ya watu wanne ni gharama sana, bado kula na mambo mengine.
 
Ni kweli Hakika..
 
nguvu kubwa ya BINADAMU ni kuwa na uwezo wa kua-adapt,...ni kweli maisha yanabadilika, lakini bado kuna fursa ndogo ndogo ambazo vijana hatuna budi kuzitumia to the maximum, pia mabadiliko ya sheria kadhaa za maisha, kama maisha ya ndoa, ni muhimu sana ili kukidhi matakwa ya maisha ya sasa,...
 
Kuna strategy gani ambazo kijana anaweza kuzitumia ku adapt??
 
Back
Top Bottom