Miaka 2 ya Rais Samia, hakuna barabara mpya iliyojengwa

Miaka 2 ya Rais Samia, hakuna barabara mpya iliyojengwa

Basi bora yule mwizi ata angeiba ajaza pesa gorofa kumi,lakini barabara tulikuwa tunaziona kudadadeki
Hoja ni kujenga mpya kila mwaka au kumalizia zilizoanzishwa? Na priorities ni barabara tu kiasi udhulumu raia wako uwapore ukajenge barabara?
 
Kutokana na report ya CAG, toka mwaka 2021 hadi sasa hakuna barabara mpya yoyote ambayo imejengwa ukiacha zile zilizo achwa na Rais Magufuli.

Je kwa mwendo huu tutafika? Je, kwa kasi kama hii miji mikubwa kama DAR kutakuwa na foleni ya kiasi gani ikizingatia ununuzi wa kasi wa magari?

Mambo ni mengi muda mchache, mabango ni mengi kuliko miradi yenyewe ya maendeleo.

Je, tuseme Serikali imekosa kabisa fedha hadi kushindwa kutenga fedha za barabara.
Magufuli alijenga barabara ipi? Marehemu alimwachia mama mzigo mkubwa sana. Alianzisha miradi mingi hasa kanda ya ziwa. Miradi ya hela nyingi mingi haikufika hata 5%. Aliyejenga barabara na kuajiri nchi hii ni mzee JK tu wengine watu wa sifa za kijinga tu.
 
Waama kama kuna wapumbavu naomba unisamehe nikupe sifa yako, hongera!

Mimi siyo CCM na siipendi lakini sukumagang kwangu naona ndio maadui wakubwa wa taifa hili sababu ya unafiki wenu.

Jibu hela za covid hazijajenga madarasa karibia kila mkoa? Unasema unasema eti nasikia reli ya SGR iko vile vile, maana huna hakika, huna taarifa unasikia upuuzi unauleta mzima mzima. Hujasikia wenye akili husema no research no right to speak? U tube, instagram, hata ripoti ya CAG imeelezea habari ya SGR. Tafuta halafu urudi.

Muda wote ambao muuaji Magufuli alitawala aliongeza mishahara mara ngapi, lini na kwa kiasi gani? Ukinijibu hapo utajiona ulivyo mpungufu.
Unaelewa maana ya sarcasm mkuu?
Elewa kwanza usiwe serious sana chief
 
Jamani Magufuli alifanya ambitious projects zilizodidimiza uchumi wa Nchi.
Mradi wa SGR una 14Trillion,mradi wa umeme ni 6 Trillion mnataka huyo Mama ajigawe vipi
 
Waliuawa kinani?Matajiri gani walinyang'wanywa fedha ushahidi tafadhali maana hii kauli ya watu kuuawa inavumishwa sana leo tuweke ushahidi
Eeheee mwenyezi Mungu weka mahala pena peponi wote waliuwawa Kwa ukatili kisa fedha na dhuluma.
 
Yule mwingine alikuwa akizindua barabara ambazo tayari zilikuwa zimeshazinduliwa ili aonekane kajenga barabara nyingi.
 
Kutokana na report ya CAG, toka mwaka 2021 hadi sasa hakuna barabara mpya yoyote ambayo imejengwa ukiacha zile zilizo achwa na Rais Magufuli.

Je kwa mwendo huu tutafika? Je, kwa kasi kama hii miji mikubwa kama DAR kutakuwa na foleni ya kiasi gani ikizingatia ununuzi wa kasi wa magari?

Mambo ni mengi muda mchache, mabango ni mengi kuliko miradi yenyewe ya maendeleo.

Je, tuseme Serikali imekosa kabisa fedha hadi kushindwa kutenga fedha za barabara.
Barabara ya Omurushaka - Benaco imeanza kujengwa.
 
Yule mwingine alikuwa akizindua barabara ambazo tayari zilikuwa zimeshazinduliwa ili aonekane kajenga barabara nyingi.
Ona Hizi Akili !!
Anaye zungumza na CAG
Wewe unaleta Story za Alnacha
Kwanini CAG Hajasema Hayo?
 
Mimi naona yuko sawa! Utaanzishaje ujenzi wa barabara mpya wakati zilizopo hazishaisha?
 
Hili swali ajiandae kukutana nalo sana majukwaani 2025.

Mtoa mada ameonesha njia tu, ni suala la wahusika kulifanyia kazi na kuwaonesha hizo barabara.

Ila kuna baadhi ya barabara hapo Dsm naona zipo kwenye Construction stages, mtaoneshwa hizo
 
Ila nchi hii ina majitu mapumbavu mengi sana! Hivi jamani hata kwa ajili ndogo hatuoni kabisa jinsi Magufuli alivyokuwa amewafanya ma miradi makubwa makubwa kwa wakati mmoja? Sasa mama angeanzisha mingine kwa fedha gani wakati pesa yote inaelekezwa kwenda kukamilisha miradi mikubwa ya Magufuli! Sasa angeachana na ya Magufuli ili aanzishe ya kwake? Watu tutumie akili bwana! Mama amefanya uamuzi mzuri, amalizane na ya Magufuli kwanza ili awamu yake ya mwisho 2025-2030 ndiyo afanye ya kwake maana hii ya Magufuli mingi atakuwa ameimaliza!
 
Chunya makongorosi imekamilika, katavi kwenda tabora imekamilika, ileje mpemba, mwendo kasi wa mbagala unakamilika, ring road dodoma inajengwa au ulitaka barabara zikamilike za kwenda chooni kwenu
Mkuu kuna majitu mapuuzi hapa nchini! Kabingo-Manyovu kupitia Kibondo, Kasulu na Buhigwe iko inajengwa kiwango cha lami sasa sijui wanataka barabara gani! Daraja la Busisi karibia linakamilika, bwawa la Nyerere karibia linakamilika na SGR inaendelea kujengwa! Mama apewe heshima yake aisee!
 
..Magufuli si alijenga barabara nchi nzima?

..sasa walitaka Maza arudie kazi iliyokamilishwa na Magufuli?
 
Back
Top Bottom