Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa JamiiForums...

Kama mtu unajali muda wako huu ni mtandao Tosha... Hakuna haja ya kuwa Kwenye Social Networks zingine

Ethos
 
Tatizo JF siku hizi imeharibiwa na watoto wa secondary.

comment za kitoto kwenye serious discussions zimekuwa nyingi sana.

Na ndio maana members wajuvi wa fani mbalimbali wanapungua siku hadi siku.

JF ilikuwa forum bora kabisa kuanzia 2013 kushuka kabila watoto wa BRN hawajajua kuitumia
 
Miaka zaidi ya minane iliyopita Bw. Maxence Melo na mwenzake Mike Mushi walikamatwa na polisi. Ilikuwa ni tarehe 18 mwezi Februari, mwaka 2008.

Ilisemekana walikamatwa kwa sababu ya tuhuma za kuhisiwa kujihusisha na mambo ya kijinai.

Binafsi nilidhani labda madhila na masaibu kama hayo kwa sasa yalikuwa nyuma yetu. Nilikosea kudhani hivyo. Tena nilikosea sana.

Sikudhani kabisa miaka 10 baada ya JF kuwa hewani kwamba mmoja wa wamiliki na mwasisi wa JF angekamatwa tena na kuwekwa ndani kwa muda wa karibu juma zima kwa tuhuma ambazo hazina mbele wala nyuma.

Kusema ukweli Max umepitia mengi sana kaka. Kusema ukweli una moyo wa kipekee sana.

Ile mara ya kwanza tu miaka 8 iliyopita, ingekuwa ndo mimi nimekamatwa na kuhojiwa na polisi ningeachana kabisa na mambo ya JF.

Lakini si wewe mazee. Uliendelea na JF mpaka kuifikisha hapa tulipo leo. Huko ni kujitoa muhanga. Umejitoa muhanga kwa niaba yetu watu kama sisi.

Kwa hilo nakupongeza sana. Lakini pia nataka nikupe pole nyingi sana kwa yote yaliyokupata juma lililopita. Ni jambo la kusikitisha sana kuwa baada ya miaka 10 ya uwepo wa JF mambo kama hayo ya kinyanyasaji bado yanaendelea.

Pole kwako, pole kwa familia yako, na nakutakia msimu mwema wa sikukuu.
 
Changamoto kubwa ya jamiiforum ni wachangiaji wake wengi waliokuwepo mwanzo wamekuwa domant au kutosikika kabisa.

Enzi zile kulikuwa na uchangiaji ukiambatanishwa na references na kufanya jukwaa kuwa la kiwango cha juu kabisa.

Kuna mwaka jamii forum ilikuwa ranked kwenye 10 bora ya forums Afrika kutembelewa.
 
Jf ndo kila kitu. Nimejifunza mengi ndani ya jf, nimepata majawabu ya maswali yangu kila nilipouliza, naitumia sana jf na inanisaidia sana ninapokuwa sina cha kufanya. Naipenda jf mpaka kufa. Sema inachoniudhi jf ni kunichukulia hata dakika
zangu za kulala.

Hahahahahaaa sawa mkuu
 
Changamoto kubwa ya jamiiforum ni wachangiaji wake wengi waliokuwepo mwanzo wamekuwa domant au kutosikika kabisa.

Enzi zile kulikuwa na uchangiaji ukiambatanishwa na references na kufanya jukwaa kuwa la kiwango cha juu kabisa.

Kuna mwaka jamii forum ilikuwa ranked kwenye 10 bora ya forums Afrika kutembelewa.
Tunajipanga maana sheria zimepitishwa kwaajili yetu...
 
Miaka zaidi ya minane iliyopita Bw. Maxence Melo na mwenzake Mike Mushi walikamatwa na polisi. Ilikuwa ni tarehe 18 mwezi Februari, mwaka 2008.

Ilisemekana walikamatwa kwa sababu ya tuhuma za kuhisiwa kujihusisha na mambo ya kijinai.

Binafsi nilidhani labda madhila na masaibu kama hayo kwa sasa yalikuwa nyuma yetu. Nilikosea kudhani hivyo. Tena nilikosea sana.

Sikudhani kabisa miaka 10 baada ya JF kuwa hewani kwamba mmoja wa wamiliki na mwasisi wa JF angekamatwa tena na kuwekwa ndani kwa muda wa karibu juma zima kwa tuhuma ambazo hazina mbele wala nyuma.

Kusema ukweli Max umepitia mengi sana kaka. Kusema ukweli una moyo wa kipekee sana.

Ile mara ya kwanza tu miaka 8 iliyopita, ingekuwa ndo mimi nimekamatwa na kuhojiwa na polisi ningeachana kabisa na mambo ya JF.

Lakini si wewe mazee. Uliendelea na JF mpaka kuifikisha hapa tulipo leo. Huko ni kujitoa muhanga. Umejitoa muhanga kwa niaba yetu watu kama sisi.

Kwa hilo nakupongeza sana. Lakini pia nataka nikupe pole nyingi sana kwa yote yaliyokupata juma lililopita. Ni jambo la kusikitisha sana kuwa baada ya miaka 10 ya uwepo wa JF mambo kama hayo ya kinyanyasaji bado yanaendelea.

Pole kwako, pole kwa familia yako, na nakutakia msimu mwema wa sikukuu.
Huu ndiyo mwaka nilioanza kuifuatilia JF mkuu,nikawa najiuliza kuna nn huku kwenye huu mtandao kupelekea hawa jamaa kukamatwa,toka kipindi hicho nikawa naingia km guest maana kujiunga ilikuwa ngumu sn tofauti na ss,hv kwa nn kipindi ile ilikuwa ngumu kujiunga jf tofauti na ss mkuu?.
 
Kiukweli Jf ina habari nyingi na nzuri kuliko magazeti na TV zote za Tanzania. Lakini, tofauti na miaka 10 iliyopita, threat sasa ni imminent zaidi. Hakuna wakati JF imeshatishwa kuliko sasa. Kuna watu wanatishwa sana na yanayoendelea JF ingawa na wao wanafika na kutembeza propaganda zao humu humu! ndivyo binadamu tulivyo, ujinga na welevu ni sehemu ya maisha yetu...
 
Changamoto kubwa ya jamiiforum ni wachangiaji wake wengi waliokuwepo mwanzo wamekuwa domant au kutosikika kabisa.

Enzi zile kulikuwa na uchangiaji ukiambatanishwa na references na kufanya jukwaa kuwa la kiwango cha juu kabisa.

Kuna mwaka jamii forum ilikuwa ranked kwenye 10 bora ya forums Afrika kutembelewa.
Na cha pili ni wanachama wengi sasa kuingia kwa mfumo wa Chama hata kama mada inahusu Taaluma wataingiza vyama matokeo take inakuwa kama FB
 
Hivi huu uzi mbona sikuuona...Mimi nilijiunga 2007 muda mfupi kabla haijabadilishwa kuwa jamii forum...Account yangu iliwekwa ban ya milele kwakuchagua mwenyewe kwani nilikuwa naanza mission mpya stage II...My mission was accomplished na si muda mrefu nitakuwa verified user stage III ya mission yangu kabla sijaaga dunia...JF is to me more than a success kwakua imekuwa a tool to accomplish my missions...Humu ndipo vita vyangu hupiganwa kwakua vita hivyo vinahitaji kuamini na kutamka kisha kuvikamilisha in the physical appearance... Thanks Maxcence, Mike, Lemutuz and my personal friend young/big bro penpal pekee wa mimi aliyepatikana humu!
 
Back
Top Bottom