Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa JamiiForums...

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
93,490
119,368
Tarehe na mwezi sivikumbuki. Lakini ninachokikumbuka ni mwaka. Mwaka huo ni 2006.

Baada ya 'condor dragon' kufanya mambo yake kule bcstimes.com, baadhi yetu tulijikuta hatuna pa kwenda kubadilishana mawazo kama tulivyokuwa tumezoea.

Mijadala ya bcstimes.com ilikuwa moto kweli kweli. Ingawa ilikuwepo mitandao mingine kama vile Youngafricans.com, tanzatl.org, darhotwire, n.k., bcstimes.com ndiyo ulijipambanua kuwa mtandao ulio makini zaidi kuliko mingine iliyokuwepo kwa wakati huo hususan kwenye vuguvugu la uchaguzi wa 2005.

Kwa wakati huo mtu kama ulitaka kupata habari moto moto kutoka jikoni basi hukuwa na budi kwenda huko.

Nakumbuka vizuri kabisa jinsi ambavyo Mzee ES [FMES - Field Marshal Emergency System], ndiye aliyekuwa kinara wa kutupakulia hizo habari moto moto kutoka jikoni.

'Condor dragon' alipofanya mambo yake wachache tukahamia TEF [Tanzania Economic Forum].

TEF ikabadilika ikaja kuwa JamboForums mnamo mwezi Agosti 2006. Baadaye [sikumbuki mwaka] JamboForums ikabadilika ndo ikaja kuwa hii JamiiForums tuliyonayo leo.

Kusema ukweli kama mwaka 2006 ungeniambia kwamba JF itadumu kwa miaka 10 ningekuona majinuni.

Ningekuona hivyo kutokana na ukweli wa kwamba huko nyuma uhai wa majukwaa kama haya ulikuwa haudumu kwa muda mrefu.

Mwanzoni mwanzoni kabisa [1996 au 1997] kulikuwepo na Nyenzi.com lakini ikaja kufa. YA nayo ikaja ikadumu kwa miaka 3 au 4 lakini hatimaye ikafa. Tanzatl.org nayo ikafuata mkondo huo huo.

Kwa hiyo halikuwa jambo la ajabu kudhani kuwa huenda JF nayo ingefuata mwelekeo huo huo.

Lakini hilo halikutokea. Matokeo yake JF imezidi kuimarika, kukua, kustawi na sasa inajulikana mpaka nje ya mipaka ya Tanzania na naamini kuwa, ingawa mwanzoni wanachama wake wengi walikuwa ni wana-ughaibuni, hivi sasa wanachama wake wengi wako Tanzania.

Katika hii miaka 10 JF imepitia changamoto nyingi sana. Kuna kipindi wamiliki wake walikamatwa na kuwekwa ndani [Maxence Melo unaweza kunisadia hapa kama nimekosea]

Kuna wakati ilifikia ikataka kufungwa kutokana na gharama za uendeshaji kuzidi kuwa kubwa lakini wanachama wakaiokoa kwa michango yao.

Kuna mijadala ambayo watu walishikana makoo na kurushiana kila aina ya maneno makali.

Moja ya mijadala hiyo ni kumhusu marehemu Dr. Ferdinand Masau. Nimejaribu kuutafuta huo uzi ili niweke kiunganishi chake hapa lakini nimeukosa. Natumaini Invisible atasaidia.
*UZI: Sakata la Dr. Masau: Msimamo wa Serikali na Hatima ya Taasisi ya Moyo (THI)

Mwingine ulikuwa ni ule wa uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka 2008. Huu uzi sitausahau kamwe: US Election Coverage 2008

Nyuzi ingine ambayo ilivutia watu ni ile iliyohusu kukamatwa kwa aliyedaiwa kuwa ndiye aliyekuwa akiendesha ile blogu ya ZeUtamu.
UZI: Ze Utamu Blogger under arrest?

Siwezi kuzikumbuka mada zote motomoto kwani zipo nyingi sana. Zingine na wengine mtaongezea mnazozikumbuka.

Miaka 10 baadaye, nikiangalia JF ilipotoka na ilipo sasa, licha ya misukosuko ya kila aina ambayo baadhi yetu tumeipitia, kwa ujumla wake nafarijika sana.

Na nina imani kwamba, kama tumeweza kudumu kwa mwongo mzima basi bila ya shaka tunaweza kuendelea kuwepo tena kwa mwongo mwingine.

Sasa, miaka 10 ni mingi. Na katika kipindi hiki kuna wanachama wenzetu ambao hatunao tena hapa duniani. Kwa hao nasema wapumzike kwa amani huko waliko.

Pia, kuna wengine ambao tulianza nao lakini kwa sababu moja ama nyingine wameacha ushiriki wao humu. Kwa hao nasema, kwanza hongereni kwa kusimama kidete siku za mwanzoni maana bila nyie [au niseme bila sisi] hii JF ya leo isingekuwepo. Ingependeza sana kama walau mngejitokeza kwa ajili ya haya maadhimisho.

Kuna wakati mtu ulikuwa unajikuta upo mwenyewe tu humu unarandaranda kama kichaa. Lakini watu hatukuchoka wala kukata tamaa.

Hivyo basi, ningependa kuwatambua na kuwapa heshima zao wanachama wakongwe wote [waliojiunga mwaka 2006 na 2007] waliolianzisha hili jukwaa letu kwani wao ndio walijenga msingi ambao JF ya leo imeukalia.

Ningependa kuwataja wachache ninaowakumbuka:

Mzee Mwanakijiji Rev. Kishoka Augustine Moshi Kyoma Mwawado Mkandara Kibunango Steve Dii Mwafrika wa Kike Kichuguu Choveki Masatu Masanja Quemu Mlalahoi Mtanzania Bibi Ntilie Game Theory jmushi1 Zakumi Moelex23

Na wengineo wote ambao nimewasahau.

Je, wewe mdau una lipi la kusema kuhusu JF yetu? Una kumbukumbu gani kuhusu JF? JF imekusaidiaje?

Kwa Maxence Melo, je, mna mpango wowote ule ulio rasmi kuhusu kusherehekea haya maadhimisho?

Hongera JF kwa kutimiza miaka 10!!!
 
Mimi nilikuwa darhotwire....kule kulikuwa na jukwaa linaitwa 'mapenzi mahusiano na urafiki' 'MMU'

kipindi hiko hata Jamboforums ilikuwa inavuma kwa siasa

kule darhotwire mtu akileta siasa tu anaambiwa 'nenda jamboforums'
tuondolee siasa

ukiingia Jamboforums kulikuwa hakuna jukwaa la MMU bado

mtandao mwingine ulikuwa eastafrican.com kama sikosei...

ilipoanza kufa darhotwire ndo tukahamia huku wengine
na jukwaa la MMU huku likaanzishwa

Moja ya kitu nakumbuka ni jinsi 'wapwaz' walivyoilazimisha JF ianzishe jukwaa la chit chat
kwa tabia ya kuanzisha story hasa kwenye thread ya mtu MMU

nina memory nyingi sana JF....

it has been fun....a lot of fun.....na kujifunza mengi.....
 
Mimi nilikuwa darhotwire....kule kulikuwa na jukwaa linaitwa 'mapenzi mahusiano na urafiki' 'MMU'

kipindi hiko hata Jamboforums ilikuwa inavuma kwa siasa

kule darhotwire mtu akileta siasa tu anaambiwa 'nenda jamboforums'
tuondolee siasa

ukiingia Jamboforums kulikuwa hakuna jukwaa la MMU bado

mtandao mwingine ulikuwa eastafrican.com kama sikosei...

ilipoanza kufa darhotwire ndo tukahamia huku wengine
na jukwaa la MMU huku likaanzishwa

Moja ya kitu nakumbuka ni jinsi 'wapwaz' walivyoilazimisha JF ianzishe jukwaa la chit chat
kwa tabia ya kuanzisha story hasa kwenye thread ya mtu MMU

nina memory nyingi sana JF....

it has been fun....a lot of fun.....na kujifunza mengi.....

Safi sana Bossman.

Nakumbuka DarHotwire kulikuwa na mizaha mizaha mingi.

Na hata huku JF watu tulikuwa tunaambiana hivyo hivyo, kwamba kama unataka udaku nenda DarHotwire.

Lakini kusema ukweli kipindi hicho..2006 - 2008 sikuweza kabisa kudhani kuwa JF ingetimiza miaka 10.
 
Inapendeza sana! Kumbe Wenzetu mmeanza kutumia hizi mambo za mitandao since 1990s huko!

Inapendeza sana, wengine tumeanza mambo haya kipindi cha Miaka ya 2000s..

Hongera Maxence, Hongera Mods wote, Hongera wakongwe wote! Inasikitisha Leo Wakati % ya watanzania wanauwezo wa kuingia mtandaoni Ndio watu wachache kwa maslahi Yao wanataka kupunguza hii kazi.

Together Forever.
 
Safi sana Bossman.

Nakumbuka DarHotwire kulikuwa na mizaha mizaha mingi.

Na hata huku JF watu tulikuwa tunaambiana hivyo hivyo, kwamba kama unataka udaku nenda DarHotwire.

Lakini kusema ukweli kipindi hicho..2006 - 2008 sikuweza kabisa kudhani kuwa JF ingetimiza miaka 10.


Na watu wengi hawajui forums kama JF zilikuwa nyiingi tu
wakati mwingine same moderators wako huku na kule
ziliibuka nyiingi sana kipindi kile JF ime survive a lot
 
I thank God for Jf. Nilianza kuisoma 2009 ila nikajiunga mwaka 2010... Frankly imenipa mafanikio sana... Mke wangu nilikutana naye love connect. Nimepata marafiki...

Long live Jf na ofcourse haiwezi kufa... I have beautiful mama watoto beside me from Jf.
 
Jamani nilijiunga JF nikiwa first year sjui second year.

Nilianza kupata kila taarifa inayotokea Tanzania.

Nimefanikiwa kuuza vitu kupitia jukwaa la matangazo madogo madogo pia nimefanikiwa kupata mfanyakakazi mzuri kabisa kupitia jukwaa la ajira.

Nina mapendekezo madogo kwa uongozi wa JF, naomba muanzishe jukwaa la kila nchi ya afrika mashariki km mlivyofanya kwa Wakenya. Muwape pia nafasi Wanyarwanda, Uganda na Warundi pia.

Afu muongeze pia Jukwaa la Agricultural professionals km lilivyo kwa madaktari ili vijana wale wanaotaka kuingia kwenye kilimo na wanahitaji msaada wa kitaalam specific waende moja kwa moja kwenye jukwaa la wataalam wa kilimo.

Asante, ni mimi Wenyele graduate asiye na makuu
 
Back
Top Bottom