Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa JamiiForums... | Page 40 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa JamiiForums...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyani Ngabu, Mar 4, 2016.

 1. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #1
  Mar 4, 2016
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 67,888
  Likes Received: 22,070
  Trophy Points: 280
  Tarehe na mwezi sivikumbuki. Lakini ninachokikumbuka ni mwaka. Mwaka huo ni 2006.

  Baada ya 'condor dragon' kufanya mambo yake kule bcstimes.com, baadhi yetu tulijikuta hatuna pa kwenda kubadilishana mawazo kama tulivyokuwa tumezoea.

  Mijadala ya bcstimes.com ilikuwa moto kweli kweli. Ingawa ilikuwepo mitandao mingine kama vile Youngafricans.com, tanzatl.org, darhotwire, n.k., bcstimes.com ndiyo ulijipambanua kuwa mtandao ulio makini zaidi kuliko mingine iliyokuwepo kwa wakati huo hususan kwenye vuguvugu la uchaguzi wa 2005.

  Kwa wakati huo mtu kama ulitaka kupata habari moto moto kutoka jikoni basi hukuwa na budi kwenda huko.

  Nakumbuka vizuri kabisa jinsi ambavyo Mzee ES [FMES - Field Marshal Emergency System], ndiye aliyekuwa kinara wa kutupakulia hizo habari moto moto kutoka jikoni.

  'Condor dragon' alipofanya mambo yake wachache tukahamia TEF [Tanzania Economic Forum].

  TEF ikabadilika ikaja kuwa JamboForums mnamo mwezi Agosti 2006. Baadaye [sikumbuki mwaka] JamboForums ikabadilika ndo ikaja kuwa hii JamiiForums tuliyonayo leo.

  Kusema ukweli kama mwaka 2006 ungeniambia kwamba JF itadumu kwa miaka 10 ningekuona majinuni.

  Ningekuona hivyo kutokana na ukweli wa kwamba huko nyuma uhai wa majukwaa kama haya ulikuwa haudumu kwa muda mrefu.

  Mwanzoni mwanzoni kabisa [1996 au 1997] kulikuwepo na Nyenzi.com lakini ikaja kufa. YA nayo ikaja ikadumu kwa miaka 3 au 4 lakini hatimaye ikafa. Tanzatl.org nayo ikafuata mkondo huo huo.

  Kwa hiyo halikuwa jambo la ajabu kudhani kuwa huenda JF nayo ingefuata mwelekeo huo huo.

  Lakini hilo halikutokea. Matokeo yake JF imezidi kuimarika, kukua, kustawi na sasa inajulikana mpaka nje ya mipaka ya Tanzania na naamini kuwa, ingawa mwanzoni wanachama wake wengi walikuwa ni wana-ughaibuni, hivi sasa wanachama wake wengi wako Tanzania.

  Katika hii miaka 10 JF imepitia changamoto nyingi sana. Kuna kipindi wamiliki wake walikamatwa na kuwekwa ndani [@Maxence Melo unaweza kunisadia hapa kama nimekosea].
  LINK: Maxence Melo, Mike Mushi arrested

  Kuna wakati ilifikia ikataka kufungwa kutokana na gharama za uendeshaji kuzidi kuwa kubwa lakini wanachama wakaiokoa kwa michango yao.

  Kuna mijadala ambayo watu walishikana makoo na kurushiana kila aina ya maneno makali.

  Moja ya mijadala hiyo ni kumhusu marehemu Dr. Ferdinand Masau. Nimejaribu kuutafuta huo uzi ili niweke kiunganishi chake hapa lakini nimeukosa. Natumaini Invisible atasaidia.
  *UZI: Sakata la Dr. Masau: Msimamo wa Serikali na Hatima ya Taasisi ya Moyo (THI)

  Mwingine ulikuwa ni ule wa uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka 2008. Huu uzi sitausahau kamwe: US Election Coverage 2008

  Nyuzi ingine ambayo ilivutia watu ni ile iliyohusu kukamatwa kwa aliyedaiwa kuwa ndiye aliyekuwa akiendesha ile blogu ya ZeUtamu.
  UZI: Ze Utamu Blogger under arrest?

  Siwezi kuzikumbuka mada zote motomoto kwani zipo nyingi sana. Zingine na wengine mtaongezea mnazozikumbuka.

  Miaka 10 baadaye, nikiangalia JF ilipotoka na ilipo sasa, licha ya misukosuko ya kila aina ambayo baadhi yetu tumeipitia, kwa ujumla wake nafarijika sana.

  Na nina imani kwamba, kama tumeweza kudumu kwa mwongo mzima basi bila ya shaka tunaweza kuendelea kuwepo tena kwa mwongo mwingine.

  Sasa, miaka 10 ni mingi. Na katika kipindi hiki kuna wanachama wenzetu ambao hatunao tena hapa duniani. Kwa hao nasema wapumzike kwa amani huko waliko.

  Pia, kuna wengine ambao tulianza nao lakini kwa sababu moja ama nyingine wameacha ushiriki wao humu. Kwa hao nasema, kwanza hongereni kwa kusimama kidete siku za mwanzoni maana bila nyie [au niseme bila sisi] hii JF ya leo isingekuwepo. Ingependeza sana kama walau mngejitokeza kwa ajili ya haya maadhimisho.

  Kuna wakati mtu ulikuwa unajikuta upo mwenyewe tu humu unarandaranda kama kichaa. Lakini watu hatukuchoka wala kukata tamaa.

  Hivyo basi, ningependa kuwatambua na kuwapa heshima zao wanachama wakongwe wote [waliojiunga mwaka 2006 na 2007] waliolianzisha hili jukwaa letu kwani wao ndio walijenga msingi ambao JF ya leo imeukalia.

  Ningependa kuwataja wachache ninaowakumbuka:

  Mzee Mwanakijiji Rev. Kishoka Augustine Moshi Kyoma Mwawado Mkandara Kibunango Steve Dii Mwafrika wa Kike Kichuguu Choveki Masatu Masanja Quemu Mlalahoi Mtanzania Bibi Ntilie Game Theory jmushi1 Zakumi Moelex23

  Na wengineo wote ambao nimewasahau.

  Je, wewe mdau una lipi la kusema kuhusu JF yetu? Una kumbukumbu gani kuhusu JF? JF imekusaidiaje?

  Kwa Maxence Melo na Mike McKee, je, mna mpango wowote ule ulio rasmi kuhusu kusherehekea haya maadhimisho?

  Hongera JF kwa kutimiza miaka 10!!!
   
 2. georgemwaipungu

  georgemwaipungu JF-Expert Member

  #781
  Feb 23, 2017
  Joined: Jul 7, 2015
  Messages: 2,698
  Likes Received: 312
  Trophy Points: 180
  Na cha pili ni wanachama wengi sasa kuingia kwa mfumo wa Chama hata kama mada inahusu Taaluma wataingiza vyama matokeo take inakuwa kama FB
   
 3. A

  Ame JF-Expert Member

  #782
  Mar 6, 2017
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 2,981
  Likes Received: 451
  Trophy Points: 180
  Hivi huu uzi mbona sikuuona...Mimi nilijiunga 2007 muda mfupi kabla haijabadilishwa kuwa jamii forum...Account yangu iliwekwa ban ya milele kwakuchagua mwenyewe kwani nilikuwa naanza mission mpya stage II...My mission was accomplished na si muda mrefu nitakuwa verified user stage III ya mission yangu kabla sijaaga dunia...JF is to me more than a success kwakua imekuwa a tool to accomplish my missions...Humu ndipo vita vyangu hupiganwa kwakua vita hivyo vinahitaji kuamini na kutamka kisha kuvikamilisha in the physical appearance... Thanks Maxcence, Mike, Lemutuz and my personal friend young/big bro penpal pekee wa mimi aliyepatikana humu!
   
 4. m

  mwarya hamadous Senior Member

  #783
  Mar 14, 2017
  Joined: Oct 22, 2016
  Messages: 137
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Mubongo?
   
 5. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #784
  Mar 14, 2017
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,560
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hongera sanaa JF Founder na members wote wakongwe
   
 6. certified mdokozi

  certified mdokozi JF-Expert Member

  #785
  Mar 14, 2017
  Joined: Jan 20, 2016
  Messages: 1,088
  Likes Received: 591
  Trophy Points: 280
  Tz best search Engine
   
 7. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #786
  Mar 15, 2017
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,122
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ndiyo, na mimi pia nawapongeza waanzilishi ...na mimi nilifika humu muda kitambo sana. ..wengine wwenu tumepata uzoefu mwingi kupitia mtandao huu, sijui yuko wapi mzee mwanakijiji ...

  Sitamsahau mtu mmoja alikuwa anajiita wa 16 sitamsahau
   
 8. T

  Tiger JF-Expert Member

  #787
  Mar 21, 2017
  Joined: Nov 30, 2007
  Messages: 1,737
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Nyani ngabu hongera kwa kutuma historia ya miaka kumi iliyopita kwa wakongwe wa JF...
   
Loading...