Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa JamiiForums... | Page 38 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa JamiiForums...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyani Ngabu, Mar 4, 2016.

 1. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #1
  Mar 4, 2016
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 77,846
  Likes Received: 39,867
  Trophy Points: 280
  Tarehe na mwezi sivikumbuki. Lakini ninachokikumbuka ni mwaka. Mwaka huo ni 2006.

  Baada ya 'condor dragon' kufanya mambo yake kule bcstimes.com, baadhi yetu tulijikuta hatuna pa kwenda kubadilishana mawazo kama tulivyokuwa tumezoea.

  Mijadala ya bcstimes.com ilikuwa moto kweli kweli. Ingawa ilikuwepo mitandao mingine kama vile Youngafricans.com, tanzatl.org, darhotwire, n.k., bcstimes.com ndiyo ulijipambanua kuwa mtandao ulio makini zaidi kuliko mingine iliyokuwepo kwa wakati huo hususan kwenye vuguvugu la uchaguzi wa 2005.

  Kwa wakati huo mtu kama ulitaka kupata habari moto moto kutoka jikoni basi hukuwa na budi kwenda huko.

  Nakumbuka vizuri kabisa jinsi ambavyo Mzee ES [FMES - Field Marshal Emergency System], ndiye aliyekuwa kinara wa kutupakulia hizo habari moto moto kutoka jikoni.

  'Condor dragon' alipofanya mambo yake wachache tukahamia TEF [Tanzania Economic Forum].

  TEF ikabadilika ikaja kuwa JamboForums mnamo mwezi Agosti 2006. Baadaye [sikumbuki mwaka] JamboForums ikabadilika ndo ikaja kuwa hii JamiiForums tuliyonayo leo.

  Kusema ukweli kama mwaka 2006 ungeniambia kwamba JF itadumu kwa miaka 10 ningekuona majinuni.

  Ningekuona hivyo kutokana na ukweli wa kwamba huko nyuma uhai wa majukwaa kama haya ulikuwa haudumu kwa muda mrefu.

  Mwanzoni mwanzoni kabisa [1996 au 1997] kulikuwepo na Nyenzi.com lakini ikaja kufa. YA nayo ikaja ikadumu kwa miaka 3 au 4 lakini hatimaye ikafa. Tanzatl.org nayo ikafuata mkondo huo huo.

  Kwa hiyo halikuwa jambo la ajabu kudhani kuwa huenda JF nayo ingefuata mwelekeo huo huo.

  Lakini hilo halikutokea. Matokeo yake JF imezidi kuimarika, kukua, kustawi na sasa inajulikana mpaka nje ya mipaka ya Tanzania na naamini kuwa, ingawa mwanzoni wanachama wake wengi walikuwa ni wana-ughaibuni, hivi sasa wanachama wake wengi wako Tanzania.

  Katika hii miaka 10 JF imepitia changamoto nyingi sana. Kuna kipindi wamiliki wake walikamatwa na kuwekwa ndani [@Maxence Melo unaweza kunisadia hapa kama nimekosea].
  LINK: Maxence Melo, Mike Mushi arrested

  Kuna wakati ilifikia ikataka kufungwa kutokana na gharama za uendeshaji kuzidi kuwa kubwa lakini wanachama wakaiokoa kwa michango yao.

  Kuna mijadala ambayo watu walishikana makoo na kurushiana kila aina ya maneno makali.

  Moja ya mijadala hiyo ni kumhusu marehemu Dr. Ferdinand Masau. Nimejaribu kuutafuta huo uzi ili niweke kiunganishi chake hapa lakini nimeukosa. Natumaini Invisible atasaidia.
  *UZI: Sakata la Dr. Masau: Msimamo wa Serikali na Hatima ya Taasisi ya Moyo (THI)

  Mwingine ulikuwa ni ule wa uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka 2008. Huu uzi sitausahau kamwe: US Election Coverage 2008

  Nyuzi ingine ambayo ilivutia watu ni ile iliyohusu kukamatwa kwa aliyedaiwa kuwa ndiye aliyekuwa akiendesha ile blogu ya ZeUtamu.
  UZI: Ze Utamu Blogger under arrest?

  Siwezi kuzikumbuka mada zote motomoto kwani zipo nyingi sana. Zingine na wengine mtaongezea mnazozikumbuka.

  Miaka 10 baadaye, nikiangalia JF ilipotoka na ilipo sasa, licha ya misukosuko ya kila aina ambayo baadhi yetu tumeipitia, kwa ujumla wake nafarijika sana.

  Na nina imani kwamba, kama tumeweza kudumu kwa mwongo mzima basi bila ya shaka tunaweza kuendelea kuwepo tena kwa mwongo mwingine.

  Sasa, miaka 10 ni mingi. Na katika kipindi hiki kuna wanachama wenzetu ambao hatunao tena hapa duniani. Kwa hao nasema wapumzike kwa amani huko waliko.

  Pia, kuna wengine ambao tulianza nao lakini kwa sababu moja ama nyingine wameacha ushiriki wao humu. Kwa hao nasema, kwanza hongereni kwa kusimama kidete siku za mwanzoni maana bila nyie [au niseme bila sisi] hii JF ya leo isingekuwepo. Ingependeza sana kama walau mngejitokeza kwa ajili ya haya maadhimisho.

  Kuna wakati mtu ulikuwa unajikuta upo mwenyewe tu humu unarandaranda kama kichaa. Lakini watu hatukuchoka wala kukata tamaa.

  Hivyo basi, ningependa kuwatambua na kuwapa heshima zao wanachama wakongwe wote [waliojiunga mwaka 2006 na 2007] waliolianzisha hili jukwaa letu kwani wao ndio walijenga msingi ambao JF ya leo imeukalia.

  Ningependa kuwataja wachache ninaowakumbuka:

  Mzee Mwanakijiji Rev. Kishoka Augustine Moshi Kyoma Mwawado Mkandara Kibunango Steve Dii Mwafrika wa Kike Kichuguu Choveki Masatu Masanja Quemu Mlalahoi Mtanzania Bibi Ntilie Game Theory jmushi1 Zakumi Moelex23

  Na wengineo wote ambao nimewasahau.

  Je, wewe mdau una lipi la kusema kuhusu JF yetu? Una kumbukumbu gani kuhusu JF? JF imekusaidiaje?

  Kwa Maxence Melo na Mike McKee, je, mna mpango wowote ule ulio rasmi kuhusu kusherehekea haya maadhimisho?

  Hongera JF kwa kutimiza miaka 10!!!
   
 2. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #741
  Nov 7, 2016
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 26,640
  Likes Received: 14,094
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa bado sijazaliwa
   
 3. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #742
  Nov 7, 2016
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 26,640
  Likes Received: 14,094
  Trophy Points: 280
  Utakuwa ccm wewe
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #743
  Nov 7, 2016
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 77,846
  Likes Received: 39,867
  Trophy Points: 280
  Hmm....mbona kama siamini vile..

  Huwa nahisi wewe ni mkongwe kuliko tarehe ya hii ID yako inavyoonyesha.
   
 5. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #744
  Nov 7, 2016
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 26,640
  Likes Received: 14,094
  Trophy Points: 280
  MI pia naipenda jf mnoooo imenifunza mengi na pia nishapata hasara ya million 2 humu humu naendelea kujifunza
   
 6. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #745
  Nov 7, 2016
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 26,640
  Likes Received: 14,094
  Trophy Points: 280
  Usijitetee
   
 7. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #746
  Nov 7, 2016
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 26,640
  Likes Received: 14,094
  Trophy Points: 280
   
 8. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #747
  Nov 7, 2016
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,599
  Likes Received: 4,763
  Trophy Points: 280
  Pole sana
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #748
  Nov 7, 2016
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 77,846
  Likes Received: 39,867
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa Mpunga....mi wala sio kibabu.
   
 10. Msafiri93

  Msafiri93 JF-Expert Member

  #749
  Nov 7, 2016
  Joined: Jul 11, 2016
  Messages: 432
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 80
  2006 nakumbuka I was std 6 primary school
  Salute kwa wooote mliofanikisha uwepo Wa forum hii since that time

  Mwanza.
   
 11. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #750
  Nov 8, 2016
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 26,640
  Likes Received: 14,094
  Trophy Points: 280
  Bado nina maumuv makali
   
 12. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #751
  Nov 8, 2016
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 26,640
  Likes Received: 14,094
  Trophy Points: 280
   
 13. kalendi

  kalendi JF-Expert Member

  #752
  Nov 10, 2016
  Joined: Mar 17, 2012
  Messages: 946
  Likes Received: 199
  Trophy Points: 60
  Hongera sana JF!
   
 14. kalendi

  kalendi JF-Expert Member

  #753
  Nov 10, 2016
  Joined: Mar 17, 2012
  Messages: 946
  Likes Received: 199
  Trophy Points: 60
  Nimejifunza mengi sana hapa JF!
   
 15. shiu yang

  shiu yang JF-Expert Member

  #754
  Nov 10, 2016
  Joined: Sep 16, 2016
  Messages: 2,512
  Likes Received: 4,477
  Trophy Points: 280
  Nimejiongezea maarifa sana,
  Na bado naendelea kujiongezea maarifa,
  Yule aliesema anatamani malaika ashuke afunge mitandao
  Wallah...! Siku hiyo sijui itakuwaje???
   
 16. Uchaubana

  Uchaubana JF-Expert Member

  #755
  Nov 17, 2016
  Joined: Jun 16, 2014
  Messages: 3,608
  Likes Received: 6,844
  Trophy Points: 280
  Exactly,nilikuwa siijui JF mwaka 2013.

  Nikimsearch Zitto Kabwe google nikaona JF.

  Kuingia huku nikakuta lile sakata la wakati uleeeeeeeeeee.

  Tangu siku hiyo ikabidi niwe naingia mara kwa mara.

  Nilipenda kuingia kule Jukwaa la Utani,nikiona kichekesho lazima nitambe mtaani.

  Yaani huku ni zaidi ya Darasa.
   
 17. NAHUJA

  NAHUJA JF-Expert Member

  #756
  Nov 17, 2016
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 18,037
  Likes Received: 19,992
  Trophy Points: 280
  Mie nilivutiwa kuingia humu mwezi Agosti, 2007. Mtandao ambao ulikuwa kidogo unatoa habari motomoto ulikuwa mdogoo ambao kwa sasa sidhani kama bado upo www.wapichai.com hahahahahahah mwe! kweli JF imetoka mbali! Nilivyoingia humu nikaona patamu hadi leo
   
 18. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #757
  Nov 17, 2016
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 14,717
  Likes Received: 18,391
  Trophy Points: 280
  Kweli mkuu.

  JF imekuwa kama nyumbani kwetu kwa sasa, ukiwa umetoka zako job huna ishu badala ya kuranda mitaani kunyoosha miguu, mtu ni bora uingie zako humu JF.

  Na bahati mbaya sana ukishaingia huwezi ona mlango wa kutokea.
   
 19. Uchaubana

  Uchaubana JF-Expert Member

  #758
  Nov 17, 2016
  Joined: Jun 16, 2014
  Messages: 3,608
  Likes Received: 6,844
  Trophy Points: 280
  Tee tee hii Forum ni kama asali.
   
 20. Omukitwe

  Omukitwe Member

  #759
  Dec 3, 2016
  Joined: Mar 29, 2016
  Messages: 91
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 25
  Jf ndo kila kitu. Nimejifunza mengi ndani ya jf, nimepata majawabu ya maswali yangu kila nilipouliza, naitumia sana jf na inanisaidia sana ninapokuwa sina cha kufanya. Naipenda jf mpaka kufa. Sema inachoniudhi jf ni kunichukulia hata dakika zangu za kulala.
   
 21. johnsonmgaya

  johnsonmgaya JF-Expert Member

  #760
  Dec 3, 2016
  Joined: Oct 16, 2015
  Messages: 2,805
  Likes Received: 3,610
  Trophy Points: 280
  Ulikuwa hauna cm yenye internet mkuu
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...