Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa JamiiForums... | Page 37 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa JamiiForums...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyani Ngabu, Mar 4, 2016.

 1. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #1
  Mar 4, 2016
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Tarehe na mwezi sivikumbuki. Lakini ninachokikumbuka ni mwaka. Mwaka huo ni 2006.

  Baada ya 'condor dragon' kufanya mambo yake kule bcstimes.com, baadhi yetu tulijikuta hatuna pa kwenda kubadilishana mawazo kama tulivyokuwa tumezoea.

  Mijadala ya bcstimes.com ilikuwa moto kweli kweli. Ingawa ilikuwepo mitandao mingine kama vile Youngafricans.com, tanzatl.org, darhotwire, n.k., bcstimes.com ndiyo ulijipambanua kuwa mtandao ulio makini zaidi kuliko mingine iliyokuwepo kwa wakati huo hususan kwenye vuguvugu la uchaguzi wa 2005.

  Kwa wakati huo mtu kama ulitaka kupata habari moto moto kutoka jikoni basi hukuwa na budi kwenda huko.

  Nakumbuka vizuri kabisa jinsi ambavyo Mzee ES [FMES - Field Marshal Emergency System], ndiye aliyekuwa kinara wa kutupakulia hizo habari moto moto kutoka jikoni.

  'Condor dragon' alipofanya mambo yake wachache tukahamia TEF [Tanzania Economic Forum].

  TEF ikabadilika ikaja kuwa JamboForums mnamo mwezi Agosti 2006. Baadaye [sikumbuki mwaka] JamboForums ikabadilika ndo ikaja kuwa hii JamiiForums tuliyonayo leo.

  Kusema ukweli kama mwaka 2006 ungeniambia kwamba JF itadumu kwa miaka 10 ningekuona majinuni.

  Ningekuona hivyo kutokana na ukweli wa kwamba huko nyuma uhai wa majukwaa kama haya ulikuwa haudumu kwa muda mrefu.

  Mwanzoni mwanzoni kabisa [1996 au 1997] kulikuwepo na Nyenzi.com lakini ikaja kufa. YA nayo ikaja ikadumu kwa miaka 3 au 4 lakini hatimaye ikafa. Tanzatl.org nayo ikafuata mkondo huo huo.

  Kwa hiyo halikuwa jambo la ajabu kudhani kuwa huenda JF nayo ingefuata mwelekeo huo huo.

  Lakini hilo halikutokea. Matokeo yake JF imezidi kuimarika, kukua, kustawi na sasa inajulikana mpaka nje ya mipaka ya Tanzania na naamini kuwa, ingawa mwanzoni wanachama wake wengi walikuwa ni wana-ughaibuni, hivi sasa wanachama wake wengi wako Tanzania.

  Katika hii miaka 10 JF imepitia changamoto nyingi sana. Kuna kipindi wamiliki wake walikamatwa na kuwekwa ndani [@Maxence Melo unaweza kunisadia hapa kama nimekosea].
  LINK: Maxence Melo, Mike Mushi arrested

  Kuna wakati ilifikia ikataka kufungwa kutokana na gharama za uendeshaji kuzidi kuwa kubwa lakini wanachama wakaiokoa kwa michango yao.

  Kuna mijadala ambayo watu walishikana makoo na kurushiana kila aina ya maneno makali.

  Moja ya mijadala hiyo ni kumhusu marehemu Dr. Ferdinand Masau. Nimejaribu kuutafuta huo uzi ili niweke kiunganishi chake hapa lakini nimeukosa. Natumaini Invisible atasaidia.
  *UZI: Sakata la Dr. Masau: Msimamo wa Serikali na Hatima ya Taasisi ya Moyo (THI)

  Mwingine ulikuwa ni ule wa uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka 2008. Huu uzi sitausahau kamwe: US Election Coverage 2008

  Nyuzi ingine ambayo ilivutia watu ni ile iliyohusu kukamatwa kwa aliyedaiwa kuwa ndiye aliyekuwa akiendesha ile blogu ya ZeUtamu.
  UZI: Ze Utamu Blogger under arrest?

  Siwezi kuzikumbuka mada zote motomoto kwani zipo nyingi sana. Zingine na wengine mtaongezea mnazozikumbuka.

  Miaka 10 baadaye, nikiangalia JF ilipotoka na ilipo sasa, licha ya misukosuko ya kila aina ambayo baadhi yetu tumeipitia, kwa ujumla wake nafarijika sana.

  Na nina imani kwamba, kama tumeweza kudumu kwa mwongo mzima basi bila ya shaka tunaweza kuendelea kuwepo tena kwa mwongo mwingine.

  Sasa, miaka 10 ni mingi. Na katika kipindi hiki kuna wanachama wenzetu ambao hatunao tena hapa duniani. Kwa hao nasema wapumzike kwa amani huko waliko.

  Pia, kuna wengine ambao tulianza nao lakini kwa sababu moja ama nyingine wameacha ushiriki wao humu. Kwa hao nasema, kwanza hongereni kwa kusimama kidete siku za mwanzoni maana bila nyie [au niseme bila sisi] hii JF ya leo isingekuwepo. Ingependeza sana kama walau mngejitokeza kwa ajili ya haya maadhimisho.

  Kuna wakati mtu ulikuwa unajikuta upo mwenyewe tu humu unarandaranda kama kichaa. Lakini watu hatukuchoka wala kukata tamaa.

  Hivyo basi, ningependa kuwatambua na kuwapa heshima zao wanachama wakongwe wote [waliojiunga mwaka 2006 na 2007] waliolianzisha hili jukwaa letu kwani wao ndio walijenga msingi ambao JF ya leo imeukalia.

  Ningependa kuwataja wachache ninaowakumbuka:

  Mzee Mwanakijiji Rev. Kishoka Augustine Moshi Kyoma Mwawado Mkandara Kibunango Steve Dii Mwafrika wa Kike Kichuguu Choveki Masatu Masanja Quemu Mlalahoi Mtanzania Bibi Ntilie Game Theory jmushi1 Zakumi Moelex23

  Na wengineo wote ambao nimewasahau.

  Je, wewe mdau una lipi la kusema kuhusu JF yetu? Una kumbukumbu gani kuhusu JF? JF imekusaidiaje?

  Kwa Maxence Melo na Mike McKee, je, mna mpango wowote ule ulio rasmi kuhusu kusherehekea haya maadhimisho?

  Hongera JF kwa kutimiza miaka 10!!!
   
 2. M

  Mahmoud Qaasim JF-Expert Member

  #721
  Aug 25, 2016
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 922
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 60
  Dah,tumetoka mbali sana, nakumbuka majukwa yote yalikuwa kwa wote, then tukaanza kuzibagua baadhi zikawekwa ni maalum kwa members na mengine ikawa hadi upewe access ili kuzifikia. vile vile wakati jamboforums ikibadilika kuwa jamii sikuwa aware nikashtukiza siku nataka kuingia jambo nakutana na jamii ilikuwa supprise sana.
  hakika kuna kila 7bu ya kujipongeza kwa kutimiza muongo miaka 10
   
 3. yegella

  yegella JF-Expert Member

  #722
  Aug 25, 2016
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 3,116
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Tumeshinda kesi ya pinga minzi tumejipangaje kwenye kesi ya msingi...
   
 4. M

  Mahmoud Qaasim JF-Expert Member

  #723
  Aug 26, 2016
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 922
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 60
  Ni safari ndefu
   
 5. Infantry Soldier

  Infantry Soldier JF-Expert Member

  #724
  Aug 29, 2016
  Joined: Feb 18, 2012
  Messages: 2,052
  Likes Received: 1,413
  Trophy Points: 280
  Naomba mawazo yako wewe kama mdau wa Tanzania yenye amani, upendo na utulivu
  click here: Maoni: Je, Unafikiri askari polisi wote wanahitaji kufanyiwa upya ukaguzi yakinifu? (full vetting) kama walivyofanya jeshi la polisi la Kenya?
   
 6. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #725
  Sep 3, 2016
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,789
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  mwenzenu leo nalala njaa......Lakini ndivyo Dunia ilivyo........ Hongera JF.....
   
 7. Infantry Soldier

  Infantry Soldier JF-Expert Member

  #726
  Sep 7, 2016
  Joined: Feb 18, 2012
  Messages: 2,052
  Likes Received: 1,413
  Trophy Points: 280
  off topic

  wakuu zangu Bridger Mod 1 Mhariri Moderator Reserved Active JamiiForums official Robot Mod 4 Mod 3 Mod 2 Mod 5 mimi nina ushauri ufuatao;

  jaribuni kuweka time stamp katika hizi threads zinazoanzishwa na comments zinazowekwa ili iwe rahisi kwa siku za usoni iwe kumbukumbu kwa mtu kujua hii thread yake ilinzishwa au comment iliwekwa tarehe gani, muda, ikiwezekana hata siku ionekana kwa pembeni. mfano thread hii inaonesha ilianzishwa (Mar 4, 2016) ila hakuna saa (13:41 GMT) au hata siku (Monday)

  najua nyie ni wataalmu sana wa programming na mtalifanyia kazi hili

  asanteni
   
 8. davidngonde

  davidngonde Senior Member

  #727
  Sep 9, 2016
  Joined: Dec 15, 2013
  Messages: 151
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 60
  hongereni jamii forums
   
 9. Alphaking mahena

  Alphaking mahena JF-Expert Member

  #728
  Sep 13, 2016
  Joined: May 20, 2015
  Messages: 1,422
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  Hongera sana Jf
   
 10. cocochanel

  cocochanel JF-Expert Member

  #729
  Sep 13, 2016
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 18,444
  Likes Received: 59,370
  Trophy Points: 280
  Bado namiss enzi za jambo forum
   
 11. mambo

  mambo JF-Expert Member

  #730
  Sep 14, 2016
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 2,377
  Likes Received: 5,013
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka nilijiunga 2007 wakati huo kunashuka mondoz naweza nikaziita za nguvu mnoo na breaking news ukiisoma mpaka unatetemeka.Mzee Es Field Marshall kumkoma nyani giladi,namkumbuka sana Halisi alikuwa analeta very intresting news pia kuna Mkuu Lunyungu hawa watu walinifanya nisibanduke JF.Bila kumsahau Nyani Ngabu na wengine wengii Kweli JF ni kiboko .
   
 12. chisluk

  chisluk JF-Expert Member

  #731
  Sep 26, 2016
  Joined: Jul 27, 2016
  Messages: 230
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 60
  hongera sana kwa miaka 10 hakika imesaidia wengi sana
   
 13. Shindu Namwaka

  Shindu Namwaka JF-Expert Member

  #732
  Sep 26, 2016
  Joined: Sep 22, 2014
  Messages: 4,690
  Likes Received: 2,832
  Trophy Points: 280
  Jf ni usafiri salama kwa watumiaji wenye michango ya aina yoyote iwe ya kijamii hata kisiasa naipongeza kwa kuwa na ulinzi na usalama kwa watumiaji kwa hilo naipa saluti.
   
 14. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #733
  Oct 11, 2016
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  IDUMU JF,ANAEOMBEA JF IFE AFE YEYE KWANZA.

  Game Theory,Es,MMM yani daah...
   
 15. Revolution

  Revolution JF-Expert Member

  #734
  Oct 12, 2016
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 565
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  JF ya miaka ya 2007 hadi 2013 ilikuwa inaongoza kwa breaking news za ufisadi zilizoandamana na supporting documents.
   
 16. j

  jijayetu JF-Expert Member

  #735
  Oct 12, 2016
  Joined: Jul 15, 2016
  Messages: 523
  Likes Received: 312
  Trophy Points: 80
  hili jukwaa lidumu daima...ubarikiwe ww INVISIBLE na team yako
   
 17. Dont

  Dont JF-Expert Member

  #736
  Oct 12, 2016
  Joined: Apr 20, 2016
  Messages: 235
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 60
  Hongera sana..
   
 18. gachuru one

  gachuru one Member

  #737
  Oct 12, 2016
  Joined: Oct 31, 2014
  Messages: 97
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 15
  Happy anniversary to jamii forum (10_year)
   
 19. Gwakukahja

  Gwakukahja JF-Expert Member

  #738
  Oct 12, 2016
  Joined: Sep 26, 2015
  Messages: 773
  Likes Received: 376
  Trophy Points: 80
  Hongereni sana jamii forum kwa mtazamo wangu ndo mtandao wa kijamii bora kabisa maana kwa 90% napata vitu positive zaidi humu ndani nmeelewa na kujifunza mengi.....
  Niwatakie kila raheli katika kazi yenu.....
   
 20. MarkHilary

  MarkHilary JF-Expert Member

  #739
  Oct 22, 2016
  Joined: Feb 8, 2015
  Messages: 963
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 180
  Yaani wakuu huu muswada wa habari ukiwa sheria sijui kama hii forum yetu itasalimika
   
 21. SALOK

  SALOK JF-Expert Member

  #740
  Oct 22, 2016
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 2,675
  Likes Received: 866
  Trophy Points: 280
  Hivi @Faizafox yuko wapi wakuu...
   
Loading...