Mhe. Aysharose Mattembe Achangia Milioni 20 Kununua Majiko ya Gesi 500 kwa Wanawake wa Mkoa wa Singida.

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

MHE. AYSHAROSE MATTEMBE ACHANGIA MILIONI 20 KUNUNUA MAJIKO YA GESI 500 KWA WANAWAKE WA MKOA WA SINGIDA

SEMINA YA MAFUNZO YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA NA UWEKEZAJI, RC MISSION MJINI SINGIDA

KAULI MBIU: "MAZINGIRA YANGU MTAJI WANGU, YATUNZE YAKUTUNZE"

Mattembe Golden Women Foundation (MGWF) inayoongozwa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Mhe. Aysharose Mattembe wametoa semina ya Mafunzo ya Utunzaji wa Mazingira na Uwekezaji kwa wanawake wa UWT Mkoa wa Singida Katika Wilaya za Singida (M), Singida (V), Ikungi, Manyoni, Mkalama na Wilaya ya Iramba huku wakiwapatia Majiko 500 ya Gesi yenye thamani ya Milioni 20, Aprili 05,2023.

Awali, Aprili 06,2023 Mbunge, Mhe. Aysharose Mattembe amesema kuwa “MGWF imejikita katika masuala ya wanawake, inahusika kuangalia Maendeleo ya wanawake na kujikita kwenye Afya, Elimu, na Mazingira. Hivyo, ameona awaunge mkono wanawake kwani wanapata changamoto mbalimbali ndiyo maana amewapatia elimu ya utunzaji wa Mazingira na Uwekezaji Ili wanawake wajue kuwa Mazingira ni Uchumi wajue namna bora ya kutumia nishati Mbadala na Wafanye shughuli za ujasiriamali ili kujikwamua na hali ngumu ya uchumi. Katika hayo, Mhe. Mattembe amesema ndiyo maana wameweza kuwapa wanawake kutoka Katika Mkoa wa Singida Majiko ya Gesi 500 kuwawezesha kukabiliana na changamoto ya nishati mbadala hususani Katika kipindi cha Mvua”.

Sambamba na hayo, Mhe. Aysharose Mattembe aliongeza kuwa wanawake wamekuwa wakitumia Kuni na Mkaa hali inayopelekea uharibifu wa mazingira pamoja na athari za kiafya hivyo Majiko ya gesi yatawasidia kwa kiasi kikubwa na huu ni mwanzo tuu mambo mazuri yatakuja kwa wanawake hao.

Mhe. Mattembe amewashukuru wanawake kwa kujitokeza kwa wingi na kupata semina hiyo huku akiwataka kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea watanzania Maendeleo.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-04-08 at 11.53.00.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-08 at 11.53.00.jpeg
    40.9 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-04-08 at 11.53.06.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-08 at 11.53.06.jpeg
    34.6 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-04-08 at 11.53.06(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-08 at 11.53.06(1).jpeg
    47.9 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-04-08 at 11.53.05.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-08 at 11.53.05.jpeg
    42.9 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-04-08 at 11.53.03.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-08 at 11.53.03.jpeg
    54 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-04-08 at 11.53.01.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-08 at 11.53.01.jpeg
    45.3 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-04-08 at 11.53.04.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-08 at 11.53.04.jpeg
    52.9 KB · Views: 4
Back
Top Bottom