Aysharose Mattembe Aahidi Kutafuta Fursa kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Kuwawezesha Wajasiriamali Mkoa wa Singida

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
SHIRIKA lisilo la kiserikali la Star Entrepreneur General kwa ufadhili wa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Mhe Aysharose Mattembe, limetoa mafunzo kwa wajasiriamali katika wilaya zote za mkoa huu ya namna ya kuendesha biashara zao kwa ufanisi na weledi ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Mafunzo hayo ambayo yalianza tarehe Oktoba 3, 2023 yalihitimishwa juzi Novemba 17, 2023 kwa awamu ya kwanza na yatakuwa endelevu ambapo kati awamu hiyo ya kwanza wajasiriamali walionufaika na mafunzo hayo ni zaidi ya wajasiliamali 1500 na ni kutoka Halmashauri za Wilaya Manyoni, Itigi, Mkalama,Iramba,Ikungi,Singida DC na Manispaa ya Singida.

Meneja wa shirika hilo,Yoel Mwenda akitoa taarifa wakati wa kufunga mafunzo hayo alisema wajasiriamali walifundishwa ufugaji wa kuku, kilimo biashara, usimamizi wa biashara, usindikaji wa mazao ya nafaka, mbogamboga na matunda pamoja na utengenezaji wa sabuni, za miche, utengenezaji wa Batiki na kujibrand(kiswahili chake ni kipi? na utafutaji wa masoko.

Naye Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe, akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo aliziomba halmashauri zote mkoani Singida kutoa kipaumbele cha kuwapatia mikopo ya kuendeshea biashara zao wajasiriamali waliopata mafunzo ya ujasiriamali.

Mattembe alisema pia atafanya utaratibu wa kuonana na taasisi zingine za fedha zinazotoa mikopo ili kuangalia uwezekano wa kutoa mikopo kwa wajasiriamali ili waweze kukuza biashara zao na kujikwamua na umaskini na hatimaye kupiga hatua moja kwenda nyingine

Alisema, ‘’nataka kuona mwanamke wa Singida anayepika mandazi na vitumbua anamiliki kiwanda cha kuokea mikate, nataka kuona wanawake wa Singida wakimiliki migahawa mikubwa na wakimiliki viwanda vikubwa vya kukamua mafuta ya alizeti, inawezekana kabisa!’’

Mattembe aliongeza kuwa mafunzo hayo yatakuwa endelevu na kila mwaka yatakuwa yakifanyika katika wilaya zote lengo likiwa ni kuungamkono jitihada za mhe Rais Dk. Samia Suluhu Hassan za kuona kila mtanzania anakuwa na shughuli ya kujiongezea kipato.

WhatsApp Image 2023-11-20 at 14.14.56(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-20 at 14.14.56(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-20 at 14.14.52(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-20 at 14.14.52.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-20 at 14.14.50(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-20 at 14.14.54.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-20 at 14.14.45(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-20 at 14.14.46(1).jpeg
 
Back
Top Bottom