Mhariri wa Gazeti la Majira umewaza nini hadi kuja na Kichwa cha hovyo hiki cha Habari leo?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,689
109,117
Rais Samia afikia rekodi ya Mwalimu Nyerere

Yaani Mtu aliyeifanyia makubwa Tanzania na kuwa Statesman kwa miaka 23 leo hii anaweza Kufananishwa na Mtu aliyeingia tarehe 17 Machi, 2021 hadi leo tarehe 11 Oktoba, 2023?

Media ya Tanzania ni kwanini mnapenda sana Kudanganya, Kujipendekeza na kuendekeza Njaa namna hii?

Hivi ukiwa na Akili timamu unaweza Kufananisha Mafanikio makubwa na ya Kihistoria ya Mchezaji Hayati Pele na Mafanikio ya hivi karibuni ( ya muda mfupi ) ya Mchezaji Novatus Dismas na kusema kuwa kamfikia Nguli Pele?

Kumbe GENTAMYCINE ninapoidharau Media ya Tanzania huwa sikosei na huwa nipo sahihi 100%.

Hovyo kabisa......!!

1697004287196.jpeg

=====

Rais Samia afikia rekodi ya Nyerere

Na Mwandishi Wetu

RAIS Samia Suluhu Hassan, amefikia rekodi iliyokuwa imeandikwa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere katika Chuo Kikuu cha India cha Jawaharlal Nehru baada ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa).

Aidha, Rais Samia amekuwa mwanamke wa kwanza nchini kutunikiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (PhD) na Chuo Jawaharlal Nehru cha nchini India na kuitoa shahada hiyo kwa watoto, hususani wa kike wanaoishi katika mazingira magumu nchini Tanzania.

Kiongozi wa kwanza wa Tanzania kutunukiwa Shadaha ya Udaktari wa wa Heshima wa Falsafa na chuo hicho ni Hayati Mwalimu Nyerere, aliyetunukiwa shahada hiyo mwaka 1995.

Taarifa kutoka chuoni hapo zinasema kuwa, Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1969, viongozi wengine wawili ambao wamewahi kutunukiwa shahada hiyo ni Rais wa Russia Vladmir Putin pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan, Hayati Shinzo Abe.

Hafla hiyo ya kumtunuku Rais Samia, Shahada hiyo ilifanyika jana jijini New Delhi, India katika Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru (JNU) kwa kutambua mchango wake katika kuchochea maendeleo ya watu nchini Tanzania.

Rais Samia yuko India kwa ziara ya kitaifa ya siku tatu, ambapo pamoja na mambo mengine alitunukiwa shahada hiyo ikiwa ni pili kwake, ambapo mara ya kwanza alitunukiwa udaktari wa heshima Novemba 30, 2022 na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Akitangaza kumtunuku Rais Samia shahada hiyo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru, Santishree Dhulipudi Pandit amesema;

“Kwa mamlaka niliyopewa mimi Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru, ni heshima kwangu kumtunuku udaktari wa heshima (Honoris Causa) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, sasa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uhusiano wa Tanzania na India na uhusiano wa India – Afrika.”

Baada ya kutangaza kumtunuku shahada hiyo, Pandit amemkabidhi Rais Samia cheti, nishani na vazi maalumu kama ishara ya kumtunuku udaktari wa heshima kiongozi huyo.

Pandit alisema Chuo hicho kimetunuku Rais Samia Shahada hiyo kwa kutambua mchango wake katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na India, Diplomasia ya Uchumi, mchango wake katika maisha ya kila siku ya wananchi wa Tanzania na mafanikio yake kikanda na kimataifa.

Pandit alisema mwaka 1995, chuo hicho kilimtunuku Mwalimu Julius Nyerere udaktari wa heshima, hivyo, Rais Samia amekuwa kiongozi wa pili wa Tanzania kutunukiwa hehima hiyo na chuo hicho.

“Chuo chetu kimetoa washindi wawili wa tuzo za Nobel na wote ni katika uchumi.

Pia, chuo hiki kipo katika nafasi 10 bora ya vyuo vikuu bora duniani katika masomo matano,” alisema makamu mkuu wa chuo.

Akizungumza baada ya kutunukiwa shahada hiyo ya udaktari wa heshima, Rais Samia alikishukuru Chuo cha Jawahalal Nehru kwa kumtunukia shahada hiyo akieleza kwamba hiyo imeongeza kitu katika historia yake.

Alisema siyo mara ya kwanza kwenda India, alikwenda kwa mara ya kwanza mwaka 1998 alipokuwa akisoma katika Chuo cha Teknolojia na Utawala cha Hyderabad, lakini amerudi tena nchini humo akiwa kama Rais wa Tanzania.

“Mmenibadilisha kama familia na kunitunuku shahada ya heshima (honoris causa), sasa nimesimama hapa kama mmoja wa familia ya Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru na siyo kama mgeni wa kawaida. Asanteni sana,” alisema Rais Samia.

Alikishukuru chuo hicho kwa kumpa heshima hiyo na kwamba anaikubali kwa kuwa anathamini uhusiano wa Tanzania na India na pia imeongeza kitu kwenye historia ya maisha yake.

“Shahada hii ya heshima itakuwa daima katika historia yangu kwa kuwa ya kwanza kutolewa kwangu na nchi ya kigeni. Ninayo moja kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam lakini hii itakuwa ya kwanza kupewa na chuo cha nje,” alisema Rais Samia.

Alisema shahada hiyo anaitunuku kwa watoto wa kike wa Tanzania wanaoishi katika mazingira magumu, akiwasihi kutokata tamaa kutokana na mazingira waliyopo na kuitaka jamii kushirikiana kuwawezesha watoto hao kufikia ndoto zao.

Alifafanua kwamba ameitoa tuzo hiyo kwa watoto hao kutokana na mazingira halisi aliyopitia tangu akiwa shule ya msingi hadi kufikia nafasi aliyonayo nayo sasa.

"Mimi ni matokeo ya jozi nyingi za macho na mikono ya watu walioona uwezo ndani yangu, wakanilea na kunishika mkono," alisisitiza Rais Dkt. Samia

Pia alisema anawashukuru watu mbalimbali wakiwemo wazazi wake, familia, Chama cha Mapinduzi na wananchi wa Tanzania kwa ujumla kwa mchango wao uliomwezesha kufikia hatua hiyo muhimu katika maisha.

"Shahada hii inanikumbusha mbali nikiwa mtoto mdogo nikienda shule katika kijiji nilichozaliwa cha Kizimkazi huko Unguja, Zanzibar, huku mama yangu akiwa ni mama wa nyumbani na baba mwalimu.

Nawashukuru kwa kunipatia muda ulioniwezesha kufikia ndoto zangu za elimu, siasa na hatimaye kufikia nafasi niliyo nayo sasa" alisema Rais Dkt. Samia.

Awali, Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Subrahmanyam Jaishankar amesema elimu na kujenga uwezo ni moja ya vipaumbele katika uhusiano wa Tanzania na India ambapo zaidi ya Watanzania 5,000 wamepata mafunzo katika taasisi za elimu za India hasa kwenye teknolojia.

Jaishankar alisema wameamua kuanzisha Taasisi ya Teknolojia ya India (IIT) huko Zanzibar na ratiba kwa ajili ya watahiniwa wa kwanza inaandaliwa na mwezi huu wataanza maomo yao. “Taasisi hii (IIT) ina fursa ya kuwa kituo kikuu cha elimu ya teknolojia kwa bara zima la Afrika.

Ni ishara ya ushirikiano wetu na dunia ya kusini na ni farahi kwangu kuwahi kwenda Zanzibar katika shughuli zangu,” amesema. Waziri huyo ameisisitiza kwamba ziara ya Rais Samia ni ya kwanza kwa kiongozi wa Afrika kuitembelea India tangu Umoja wa Afrika (AU) ilipoingizwa kwenye umoja wa mataifa yaliyoendelea kiviwanda duniani (G20).
 
Rais Samia afikia rekodi ya Mwalimu Nyerere

Yaani Mtu aliyeifanyia makubwa Tanzania na kuwa Statesman kwa miaka 23 leo hii anaweza Kufananishwa na Mtu aliyeingia tarehe 17 Machi, 2021 hadi leo tarehe 11 Oktoba, 2023?

Media ya Tanzania ni kwanini mnapenda sana Kudanganya, Kujipendekeza na kuendekeza Njaa namna hii?

Hivi ukiwa na Akili timamu unaweza Kufananisha Mafanikio makubwa na ya Kihistoria ya Mchezaji Hayati Pele na Mafanikio ya hivi karibuni ( ya muda mfupi ) ya Mchezaji Novatus Dismas na kusema kuwa kamfikia Nguli Pele?

Kumbe GENTAMYCINE ninapoidharau Media ya Tanzania huwa sikosei na huwa nipo sahihi 100%.

Hovyo kabisa......!!
Chawa
 
Upo sahih popoma , Ni ujinga mtupu
 
Yaani ishu siyo kwa nyie mnasikiliza na kuperuzi mitandaoni hayo magzeti, ila tatizo la hicho kichwa cha habari kisomwe katika radio aidha TBC, RADIO ONE AU RFA halafu tusikie sisi wa huku Kalambo ndani huku. Sipati picha tutakavo wadharau hawa marais wengine waliotangulia kwa kudhani walishindwa vipi anagalau kumfikia Nyerere kwenye utumishi wao?
 
Rais Samia afikia rekodi ya Mwalimu Nyerere

Yaani Mtu aliyeifanyia makubwa Tanzania na kuwa Statesman kwa miaka 23 leo hii anaweza Kufananishwa na Mtu aliyeingia tarehe 17 Machi, 2021 hadi leo tarehe 11 Oktoba, 2023?

Media ya Tanzania ni kwanini mnapenda sana Kudanganya, Kujipendekeza na kuendekeza Njaa namna hii?

Hivi ukiwa na Akili timamu unaweza Kufananisha Mafanikio makubwa na ya Kihistoria ya Mchezaji Hayati Pele na Mafanikio ya hivi karibuni ( ya muda mfupi ) ya Mchezaji Novatus Dismas na kusema kuwa kamfikia Nguli Pele?

Kumbe GENTAMYCINE ninapoidharau Media ya Tanzania huwa sikosei na huwa nipo sahihi 100%.

Hovyo kabisa......!!
Huenda na yeye alikuwemo ndani ya ndege, hebu nenda ofisini kwake kawaulize kama yupo nchini.
 
Huwa nahusudu sana nyuzi zako ila kwa huu uzi umeteleza!
Rekodi aliyoifikia hujaitaja ili tuipime ni kweli ama si kweli.
Nyerere alitunukiwa PhD huko lndia na huyu kafanyiwa hivyo hivyo je hii yaweza kuwa ndiyo Majira waisemayo?
Sijalisoma gazeti.
Unaweza kuyafananisha Mafanikio makubwa yaliyofanywa na Pele kwa miaka mingi dhidi ya yaliyofanywa / yanayofanywa sasa na akina Simon Msuva na Novatus Dismas?

Acha kunilazimisha nianze pia Kukudharau na Wewe sawa? Acheni kumfananisha Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na haya Maupuuzi Upuuzi yenu sawa?
 
Back
Top Bottom